Yoyo Zhou
Senior Member
- Jun 16, 2020
- 126
- 215
Takwimu zilizotolewa hivi karibuni na Idara Kuu ya Takwimu ya China zinaonesha kuwa, mwaka 2024 pato la Taifa la China lilikua kwa asilimia 5, na kufikia yuan trilioni 134.9, sawa na dola trilioni 18.94 za Marekani.
Katika mwaka uliopita, licha ya changamoto za nje na ndani, China ilifanikiwa kutimiza lengo lake la ukuaji wa uchumi, na kwa mara nyingine tena imethibitisha uwezo wake wa kudumisha maendeleo ya uchumi.
Tangu mwaka 2019, kutokana na kuendelea kudorora kwa uchumi wa dunia, uchumi wa China umekuwa ukidumisha maendeleo tulivu ikilinganishwa na nchi nyingine kubwa kiuchumi duniani, na hasa baada ya janga la COVID-19, China imeendelea kutoa mchango mkubwa zaidi kwa ukuaji wa uchumi wa dunia.
Uchumi wa China kuendelea kukua kwa kasi kunatokana na marekebisho ya muundo wa uchumi. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Takwimu ya China, katika mwaka uliopita, nchini China, sekta ya kilimo ilikua kwa asilimia 3.5, sekta ya viwanda ilikua kwa asilimia 5.3, na sekta ya huduma ilikua kwa asilimia 5. Miongoni mwao, sekta ya viwanda ilikua kwa kasi zaidi, haswa sekta ya utengenezaji wa ubora wa juu ilikua kwa asilimia 8.9.
China imeendelea kuwa nchi yenye nguvu zaidi ya kiviwanda duniani, na uzalishaji wake wa kiviwanda unachukua asilimia 28 ya uzalishaji duniani kote. Kiwango cha sekta ya huduma pia kilichangia ukuaji wa uchumi wa nchini China, na mwaka jana ilichukua asilimia 56.7 ya Pato la Taifa.
Kuendelea kufufuka kwa soko la matumizi pia kulichangia ukuaji wa uchumi wa China. Ili kukabiliana na changamoto mbalimbali, China imetekeleza sera nyingi za kupanua matumizi ya ndani, ikiwemo kupunguza kodi na ada, na utoaji wa ruzuku kwa wateja. Kulingana na takwimu zilizotolewa na Idara Kuu ya Takwimu ya China, mwaka 2024 jumla ya mauzo ya rejareja ya bidhaa za matumizi iliongezeka kwa asilimia 3.5 ikilinganishwa na mwaka 2023, hususan mauzo ya rejareja mtandaoni yaliongezeka kwa asilimia 7.2.
Kwa upande wa biashara ya nje, mwaka 2024, thamani ya biashara kati ya China na nchi za nje iliongezeka kwa asilimia 5, na mauzo ya bidhaa za China kwa nchi za nje yaliongezeka kwa asilimia 7.1. Kati ya bidhaa za China zilizouzwa kwa nchi nyingine, magari yalizidi milioni 6, na thamani ya chip ilizidi yuan trilioni moja. Hali hii inamaanisha kuwa, muundo wa mauzo ya nje ya China umeboreshwa kutokana na maendeleo ya kasi ya sayansi na teknolojia nchini China.
Hata hivyo uchumi wa China unakabiliwa na changamoto mbalimbali, zikiwemo vita, hali tete ya kibiashara, kudidimia kwa uchumi wa dunia, na vikwazo vilivyowekwa na nchi za magharibi. Lakini wakati huo huo, China ina uwezo mkubwa wa ndani, ikiwemo mfumo maalumu wa kijamaa, nguvukazi ya watu bilioni 1.4, soko kubwa la ndani, na mtandao kamili wa viwanda. Hivi vyote ni vyanzo vyenye nguvu vya ukuaji tulivu wa uchumi wa China.