Uchumi wa Kenya unategemea mahusiano ya kibeberu dhidi ya Tanzania

Uchumi wa Kenya unategemea mahusiano ya kibeberu dhidi ya Tanzania

kmbwembwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
10,892
Reaction score
7,780
Ubeberu wa kimataifa umejiundia tangu kale mahusiano ya kiuchumi ambayo wao ni kama bahari. Mito yote kutoka nchi kavu na maziwa lazima yaishie kwao baharini.

Kuna mito huingia kwenye maziwa halafu kuna mito inatoka kwenye maziwa kwenda baharini. Kenya ni kama ziwa kwa uchumi wa tanzania. Wanatunyonya kutokana na uchumi wao mkubwa wa viwanda tangu ukoloni. Kila tanzania ikijaribu kuelekeza baadhi ya bidhaa zake moja kwa moja kwenye masoko ya nje kwa kuziongeza thamani wenyewe bila kuzipitisha Kenya hapo kunatokea kutoelewana. Kenya watatumia kila njia na hila kutukwamisha. Kama ni mifugo kama ni mazao au madini mambo kwa tanzania yanakua magumu kufunga mto wa kiuchumi unaopita kenya kuelekea baharini.

Suala hili la madini ya tanzanite linahitaji ujasiri mkubwa kuwazuia wakenya wasiendelee kunyonya na kuidhulumu tanzania. Tumejenga ukuta lakini unatobolewa tanzanite inafika kenya kwa kiasi kilekile au zaidi. Tumeweka EPZ mererani ubeberu wameweka upofu wa kusudi kwa baadhi ya viongozi kama sendeka alivyomueleza waziri mkuu. Dealers wakubwa wahindi na wakenya wameazimia hatufanikiwi lazima tanzanite iende kua processed kenya na india. Wao ndio wapate faida na watu wao wapate kazi. Sisi tupate makombo na serikali yetu isipate kodi.

Kuna mapambano makali kutoka jirani zetu kuhakikisha licha resources tulizo nazo hatuwi uchumi mkubwa kuliko wao. Yaani sisi tusiwe ziwa kama wao au mto mojakwa moja kuelekea baharini kiuchumi. Lazima tuongeze ujasiri tusiwe wa kuibiwa kwa nguvu uchumi na jirani na huku kimataifa kwenye biashara ubeberu unatukandamiza.

Mahusiano mazuri na Kenya isiwe sisi kukaa kimya huku kila mbinu ya kukuza uchumi wetu uchumi wao unatuhujumu kwa kupitisha madini na bidhaa zetu njia za panya bila wao kutoa ushirikiano kuzuia kwa kua wao ni wanufaika.
 
Haya ndio matokeo HASI ya ujamaa na kjitegemea wa TZ, hakika Kenya ilianza kunufaika na uchumi wa Tanzania baada tu ya Azimio la Arusha, Ile taifisha viwanda na mashamba, makampuni makubwa hawa wamiliki walichokifanya ni kuondoka na mitaji na wengine walihalishia viwanda kenya

Wakaendelea kutumia rasrilami gafi zile zile ila sasa kwa kuvuka mpaka,Ujasriamali, Raw materials, viwanda na watu na mitaji ile ile ya Tanganyika ikavuka mipaka na bidhaa baada ya uzalishaji zilivuka tena mpaka kuja kuuzwa soko lao la asili TANGANYIKA

Tangia hapo nachelea kusema kwamba Tanganyika iligeuka kuwa koloni la KENYA kiuchumi (inauma sana sana) kwa nini ? kila kilichozalishwa TZ kilicho bora kiliuzwa kenya au kiliunzwa Ng'ambo lazima kupitia kenya isipokuwa tu Pamba vingine vyote kenya, Ngombe mnono, ngozi yake, mahindi, kahawa, alizeti,kila mazao Dhahabu, Tanzanite, Samaki, Katani, kila kitu kwa wale watz wanaoshi mipaka ya kenya wanajua na sisi walituletea Sabuni, mafuta kula , mafuta kujipaka, vyombo plastic n.k

Siasa yetu ya UJAMAA ILIUA KABISA UJASRIAMALI(ENTREPRENEURSHIP) Hao Hao Wafanyabiashara tukawachukia tukawaita majina ya ajabu kenya ikawakumbatia ikawawezesha wafanyabiashara wanahamisha wanafyonza RASRIMALI ZOTE toka tz kwenda huko na hadi leo kwa kusaidiwa na serikali hiyo

Siasa ya Ujamaa ina faida nyingi kwenye jamii lakini kwenye Uchumi na maendeleo kwa ujumla wake HAIFAI KABISA hasa private sector usitegemee mafanikio, na hata hiyo jamii hiyo hiyo bado itahitaji au itategemea uchumi ulioimara kuifanikisha ambao kwa hakika unatokana na private sector kimsingi.

Tafuteni Data za uchumi wa nchi zote za East Africa kabla ya Uhuru aidha kuanzia 1955 to 1965 Utagunduka Tanganyika ndio ilikuwa na uchumi mkubwa kuliko zote kwa sababu 1. Sisal 2. Gold 3. Diamond n.k
Ntaendelea . . . .
 
Kwa heshima, naomba nijibu kwa upande wa Kenya;

Hii post ni lame excuse, hakuna ukweli hapo, propaganda ulio aminishwa tokea zamani, sio mara ya kwanza kusikia haya malalamishi yasio kuwa na msingi, serikali ya Kenya haisaidii private sector ama wanabiashara wanao exploit Tanzania, ni uwongo, Kenya ni nchi ya kibepari, mtu ama kampuni yeyote ijitume iwezavyo kibiashara, aidha watoe mizigo na resources zao nje ama ndani, hiyo ni shida yao, Serikali ya Kenya haihusiki!, bora ufuate Sheria na ulipe ushuru. Magendo pia iko pande zote, hilo najua mnafahamu. Wakulima na wanabiashara wa Tanzania wanauza mazao yao Kenya na kuwekeza Kenya kwa sababu faida wanayo pata iko juu ukilinganisha na kuuza Tanzania, hiyo ni capitalism, so mleta mada anaongozwa na blind patriotism, kudanganywa kupitia propaganda, yaani kuongeza chumvi kutokana na historia ya EAC ilivyovunjika na Kenya ilivyo taifisha viwanda kadhaa ambavyo ata vilifilisika kwa wingi chini ya serikali ya Moi na Mzee Kenyatta. Na pia kuamini eti hapa Kenya viongozi wanakaa na kujadili na kufanya mikakati jinsi ya kuzuia Tanzania kukua kiuchumi zaidi ya Kenya 😂😂, hiyo ni fallacy, yaani porojo, kisa Tanzania inashindwa ku compete kibiashara.

Mimi kibinafsi naona ni diplomasia hafifu ya Tanzania. Mfano, hivi majuzi tu, kabla ya Magufuli kuaga, South Africa walichoma maparachichi kutoka Tanzania, haimaanishi eti sasa wao wanampango wa kuhujumu uchumi wa Tz, la hasha, ila kuna Sheria, Tanzania haija ingia kwa mkataba wa bilateral agreement na SA wa kuuza parachichi SA, huwezi kupeleka mizigo yako na kuuza kwa nchi ya wenyewe kama unavyo uza kule Kariokoo market. Kwa mfano Kenya imetia saini ya bilateral agreement na China na UK ili wanabiashara wa Kenya kuweza kuuza parachichi, Tanzania bado, mfanyibiashara wa Tanzania ule mjanja atauzia mKenya parachichi kwa bei nafuu kuliko vile angeuza Tanzania, kisha mwanabiashara wa Kenya anajumuisha na yake na kusambaza nje.

Serikali ya Kenya haiuzi parachichi, yao ni kutengeneza mikataba kwa manufaa ya raiya, wao wapate ushuru. Kwa hivyo Mabalozi wenu na taasisi ya foreign affairs ndio wamelala kazini. Na pia mwendazake yeye hakukua wa kutoka nje kuzunguka ulimwengu kutafutia Tanzania fusra za kibiashara, Rais Uhuru ame sign mikataba kibao na nchi mingi ili Kenya kuruhusiwa kuuza bidhaa huko, ata Nigeria tunapeleka maziwa baada ya kusign bilateral agreement! but tuseme kwa mfano Tanzania wakiona vile na wao wapeleke maziwa yao Nigeria kienyeji kisha ikataliwe na kumwagwa na hizi fikra za mleta mada, si mtasingizia eti ni Kenya inawahujumu kwasababu ya Kenya inakubalika na ya Tanzania inakataliwa?

Hizi fikra zenyu mbona zimechanganyikiwa hivyo? elewa cross border business politics na mpangilio. Viongozi wenu ndio wamelala, policies za CCM ni zile za kijamaa, ambazo hazina tija kwa ulimwengu wa sasa, kama china wamekua capitalist kibiashara Tanzania inangoja nini? Mama Suluhu kachukua mtindo wa kidiplomasia kwa biashara na hapo akiendelea kuingia mikataba na nchi za nje kwa manufaa ya wanabiashara wa Tanzania, Tanzania itashinda na kufaulu kwa ajili ya rasilmali kwa wingi, na mko na airline, mnaeza geuza ikawa ya cargo kwa more than passenger, ili kusambaza mali zenu duniani kwa faida kubwa! Though protectionism mechanism ziko, na ni kawaida especially SA. Hawawezi kukibali banks na supermarkets za Kenya ama nchi zingine Africa kuwekeza kule, but wao wanewekeza huku na nchi mingi Africa kwa wingi. Kenya tumezuia, mayai, sukari na maziwa ya Uganda! Hiyo ni business politics ya mataifa.

Jumapili njema watani.
 
Hehehe!!! Hivi vilio vya Watanzania husababisha nicheke sana, mimi Mkenya hapa nakaa mkao wa kusoma comments tu...miaka nenda miaka rudi mnalialia Kenya hiki Kenya kile, kuanzia kwa mababu zenu kuja mpaka kwa wajukuu kila siku Kenya...Kenya...Kenya....
 
Ok. Mi naona you are partialy right. Ila naamini kwenye capitalism hukosi umafia. Kenya iko vizuri zaidi ndio maana whatever we do tanzanite inaishia nairobi. Thanks ..maoni zaidi wajameni wakenya.
 
Ok. Mi naona you are partialy right. Ila naamini kwenye capitalism hukosi umafia. Kenya iko vizuri zaidi ndio maana whatever we do tanzanite inaishia nairobi. Thanks ..maoni zaidi wajameni wa kenya.
Umafia ndio maisha ya walimwengu., kote kote., dunia hii ukiwa muungwana sana utabaki nyuma, pengine uwe wa imani, basi neema za Maulana zitakuweka kileleni, la sivyo utabaki fukara kwa ungwana wako.

Ni mwenye nguvu mpishe, hakuna Cha tafadhali ala naomba unipishe., unapigwa kumbo na kisukimwa kando! Ndio maana Africa bado sana, kwanza vile tumegawanywa tuko hafifu in the world stage.
 
Umafia ndio maisha ya walimwengu., kote kote., dunia hii ukiwa muungwana sana utabaki nyuma, pengine uwe wa imani, basi neema za Maulana zitakuweka kileleni, la sivyo utabaki fukara kwa ungwana wako. Ni mwenye nguvu mpishe, hakuna Cha tafadhali ala naomba unipishe., unapigwa kumbo na kisukimwa kando! Ndio maana Africa bado sana, kwanza vile tumegawanywa tuko hafifu in the world stage.
Uko sawa ndugu ila viongozi wetu wakichukua hatua kujikwamua msiwaitage dikteta. Huyu jirani kenya inahitaji state intervention ili kula naye sahani moja bila sisi kulala njaa.
 
Kenya wanaona wivu sana tunavyo access soko kwenye jumuiya ya SADCC hasa mahusiano ya kibiashara na SA, nilikutana na mkenya personally akaongelea kuhusu hili la kuwa na bidhaa zinazotoka SA, huo ndo mshono tunaoweza kuwatwanga hawa kunyaland wapunguze majigambo yao.....
 
Sisi kuzima moto tu kwenye soko la kkoo unatushinda ili hali kituo cha FIRE kipo kariakoo haizidi hata dakika 10 kufika kwenye eneo la moto kkoo.

Ndio unaleta ngonjora hapa za ubeberu wa kimataifa shame on you ...sisi kazi yetu kujikweza sn ilihali kichwani ni zero blah blah nyingi sn .
 
Hehehe!!! Hivi vilio vya Watanzania husababisha nicheke sana, mimi Mkenya hapa nakaa mkao wa kusoma comments tu...miaka nenda miaka rudi mnalialia Kenya hiki Kenya kile, kuanzia kwa mababu zenu kuja mpaka kwa wajukuu kila siku Kenya...Kenya...Kenya....
Wewe sema tunalialia ila sisi tunajua tunasonga mbele. Kuzuia bidhaa na madini yetu kuingia kenya kimagendo ni sehemu tu na mipango ya tz ya maendeleo.
 
Back
Top Bottom