Mada kama hii huwa zinaumiza sana.
Mwishowe mtu unajiuliza, hivi hao Kenya wana mvuto gani na Tanzania, kiasi kwamba tumeshikiliwa na sumaku yenye nguvu tusiyoweza kujinasua nayo?
Nilishauliza swali humu, lakini sijawahi kupata jibu juu yake:
Tunao majirani wengi sana tunaopakana nao mipaka, lakini katika majirani wote hao, hakuna nchi hata moja ambayo, sijui kama ni kwa kujua au kutojua, tunao njia nyingi sana za kuingiliana nao ukilinganisha na njia tulizonazo na jirani yetu Kenya, tena njia hizo zinaendelea kuboreshwa kwa kiasi kikubwa, huku majirani zetu wengine ni kama hatuna habari nao.
Kwa nini imetokea kuwa hivyo, ni mipango ya hao wenye bahari yao wanaofanya mambo bila ya sisi kutambua?
Angalia mpaka wetu na Kenya, tuna barabara nzuri kuingiliana pale Namanga, nyingine ipo siyo mbali sana pale Horiri, na nyingine Holoholo, Tanga. Ziwani kuna meli kadhaa, na bado Kenya wanatafuta njia ya moja kwa moja ya kuingilia Serengeti. Pale Sirari kuna barabara nzuri kuingia Mara, Mwanza, Simiyu na maeneo mengi mengine toka Kenya.
Angalia ramani, Namanga na Horiri zimeunganishwa na Mombasa kwa barabara safi kabisa. Barabara hiyo ikitoka Mombasa, kuingia Arusha, inachepuka na kuteremka kwenda Singida kuungana na ile kuu kuelekea Tabora na kwingineko, kama Burundi na hata Rwanda. Barabara hiyo wenyewe waliwahi kusema ni barabara yao ya kwenda Burundi, tokea Mombasa, na muda si muda watadai kupitisha mizigo yao kwenda huko.
Bado hairidhishi, kuna barabara tunachukua mkopo wa AfDB, ijengwe toka pale mpakani Tanga , ikitokea Malindi, iambaeambae kando kando ya bahari ya Hindi ifike Bagamoyo. Tumechukua mkopo tujenge barabara hii, huku ikiwepo barabara nzuri tu toka Tanga hadi Dar.
Hii barabara ni ya nini, kutuletea wakenya pwani kwetu?
Hatuna mahitaji ya barabara nzuri kama hiyo na majirani zetu wengine, kama Uganda, Zambia, Malawi, na hata angalau kuweka meli kadhaa kuvusha ziwa Tanganyika kwenda DRC?
Kenya kuna nini tunachokifuata huko kila mara! Ni viongozi gani wanaotufunga na Kenya kiasi kwamba tunajisahau kuwa tunao majirani wengine tunaohitaji kufanya biashara nao?
Ninakubaliana na mada yako kwa jambo moja.
Kuna njama za namna fulani zinazotuvuta kuwa mkia wa Kenya.