Kwa heshima, naomba nijibu kwa upande wa Kenya;
Hii post ni lame excuse, hakuna ukweli hapo, propaganda ulio aminishwa tokea zamani, sio mara ya kwanza kusikia haya malalamishi yasio kuwa na msingi, serikali ya Kenya haisaidii private sector ama wanabiashara wanao exploit Tanzania, ni uwongo, Kenya ni nchi ya kibepari, mtu ama kampuni yeyote ijitume iwezavyo kibiashara, aidha watoe mizigo na resources zao nje ama ndani, hiyo ni shida yao, Serikali ya Kenya haihusiki!, bora ufuate Sheria na ulipe ushuru. Magendo pia iko pande zote, hilo najua mnafahamu. Wakulima na wanabiashara wa Tanzania wanauza mazao yao Kenya na kuwekeza Kenya kwa sababu faida wanayo pata iko juu ukilinganisha na kuuza Tanzania, hiyo ni capitalism, so mleta mada anaongozwa na blind patriotism, kudanganywa kupitia propaganda, yaani kuongeza chumvi kutokana na historia ya EAC ilivyovunjika na Kenya ilivyo taifisha viwanda kadhaa ambavyo ata vilifilisika kwa wingi chini ya serikali ya Moi na Mzee Kenyatta. Na pia kuamini eti hapa Kenya viongozi wanakaa na kujadili na kufanya mikakati jinsi ya kuzuia Tanzania kukua kiuchumi zaidi ya Kenya [emoji23][emoji23], hiyo ni fallacy, yaani porojo, kisa Tanzania inashindwa ku compete kibiashara.
Mimi kibinafsi naona ni diplomasia hafifu ya Tanzania. Mfano, hivi majuzi tu, kabla ya Magufuli kuaga, South Africa walichoma maparachichi kutoka Tanzania, haimaanishi eti sasa wao wanampango wa kuhujumu uchumi wa Tz, la hasha, ila kuna Sheria, Tanzania haija ingia kwa mkataba wa bilateral agreement na SA wa kuuza parachichi SA, huwezi kupeleka mizigo yako na kuuza kwa nchi ya wenyewe kama unavyo uza kule Kariokoo market. Kwa mfano Kenya imetia saini ya bilateral agreement na China na UK ili wanabiashara wa Kenya kuweza kuuza parachichi, Tanzania bado, mfanyibiashara wa Tanzania ule mjanja atauzia mKenya parachichi kwa bei nafuu kuliko vile angeuza Tanzania, kisha mwanabiashara wa Kenya anajumuisha na yake na kusambaza nje.
Serikali ya Kenya haiuzi parachichi, yao ni kutengeneza mikataba kwa manufaa ya raiya, wao wapate ushuru. Kwa hivyo Mabalozi wenu na taasisi ya foreign affairs ndio wamelala kazini. Na pia mwendazake yeye hakukua wa kutoka nje kuzunguka ulimwengu kutafutia Tanzania fusra za kibiashara, Rais Uhuru ame sign mikataba kibao na nchi mingi ili Kenya kuruhusiwa kuuza bidhaa huko, ata Nigeria tunapeleka maziwa baada ya kusign bilateral agreement! but tuseme kwa mfano Tanzania wakiona vile na wao wapeleke maziwa yao Nigeria kienyeji kisha ikataliwe na kumwagwa na hizi fikra za mleta mada, si mtasingizia eti ni Kenya inawahujumu kwasababu ya Kenya inakubalika na ya Tanzania inakataliwa?
Hizi fikra zenyu mbona zimechanganyikiwa hivyo? elewa cross border business politics na mpangilio. Viongozi wenu ndio wamelala, policies za CCM ni zile za kijamaa, ambazo hazina tija kwa ulimwengu wa sasa, kama china wamekua capitalist kibiashara Tanzania inangoja nini? Mama Suluhu kachukua mtindo wa kidiplomasia kwa biashara na hapo akiendelea kuingia mikataba na nchi za nje kwa manufaa ya wanabiashara wa Tanzania, Tanzania itashinda na kufaulu kwa ajili ya rasilmali kwa wingi, na mko na airline, mnaeza geuza ikawa ya cargo kwa more than passenger, ili kusambaza mali zenu duniani kwa faida kubwa! Though protectionism mechanism ziko, na ni kawaida especially SA. Hawawezi kukibali banks na supermarkets za Kenya ama nchi zingine Africa kuwekeza kule, but wao wanewekeza huku na nchi mingi Africa kwa wingi. Kenya tumezuia, mayai, sukari na maziwa ya Uganda! Hiyo ni business politics ya mataifa.
Jumapili njema watani.