The Sunk Cost Fallacy
JF-Expert Member
- Dec 1, 2021
- 19,582
- 14,167
Bahati nzuri Uchumi sio hisia zako na njaa zako binafsi..Sasa ni dhahiri kwamba maisha ya Watanzania yamekuwa magumu kuliko awamu zote zilizopita , familia nyingi sasa zinakula mlo mmoja tu , huku Maharage yakiwa Chakula Muhimu kabisa .
Ni kweli kwamba Mambo ya Utekaji , kuokota viroba vya maiti baharini na kwingineko na ubambikaji kesi za uongo , zilizoitwa za uhujumu uchumi na Utakatishaji fedha kwa sasa yamepungua (Hayajaisha) , lakini maisha ya Raia yamekuwa kizungumkuti , hali ni mbaya mno ! Mzunguko wa pesa ni kama hakuna , watu wamekuwa masikini mno ! Chakula Kikuu kimekuwa Mihogo na Maharage .
Hata sisi tuliobarikiwa kidogo ni kama tuko matatani , tunapigwa mno mizinga na wenye uhitaji kuliko kipindi chochote kile , shida ya nchi hii ni nini ?
Sasa katika hali kama hii ya sasa nchini Tanzania ni Nani alaumiwe , Ni Rais wa Nchi au Waziri wa Fedha ?
Unapimwa Kwa vitu vidogo Sana ,mosi ni Mwenendo wa mapato ya serikali,ukiona yanaongezeka ujue mambo ni matamu..
Pili sekta ya Ujenzi,ukiona huko mtaani hardware zinauza na watu wanajenga basi wewe jua Uchumi uko mtamu..
Na mwisho nenda Bar saizi harafu uje na jibu..Jiwe aliwahi waambia kama uchumi ni mbaya watu wameacha kwenda kushona nguo kwa mafundi au sherehe zimeacha kufanyika?