robinson crusoe
JF-Expert Member
- Oct 22, 2020
- 762
- 1,236
Nasema kodi tena kwa sababu tulikuwa na kodi ya kichwa, ikaitwa kodi ya maendeleo baadaye Utawala wa Mkapa ukaifuta. Mifugo pia ililipiwa kodi na kwa wale wakongwe, kulikuwa na kodi ya baiskeli mitaani.
Taarifa niliyorushiwa, kuna zoezi la kodi ya mifugo inaendelea wilayani Ukerewe. Mbuzi na Ng'ombe sasa wanalipiwa kodi. Yaonekana, kuna kodi nyingi zinarudishwa lakini kwa ujumla ni ukosefu wa akili kwa wachumi wetu na hasa kipindi hiki ambacho wananchi wanastahili kupunguziwa ugumu wa maisha.
Au ni wizi wa wazi kwa viongozi wa halmashauri wanaojiamulia bila kujali huko juu watasemaje. Aliye na taarifa za wilaya zingine pia tunaomba atuletee taarifa za kadi hizi mpya zilizoanza nchini.