Tetesi: Uchumi wa Tozo sasa wananchi UKEREWE waanza kutozwa kodi ya mifugo tena

Tetesi: Uchumi wa Tozo sasa wananchi UKEREWE waanza kutozwa kodi ya mifugo tena

Nasema kodi tena kwa sababu tulikuwa na kodi ya kichwa, ikaitwa kodi ya maendeleo baadaye Utawala wa Mkapa ukaifuta. Mifugo pia ililipiwa kodi na kwa wale wakongwe, kulikuwa na kodi ya baiskeli mitaani.

Taarifa niliyorushiwa, kuna zoezi la kodi ya mifugo inaendelea wilayani Ukerewe. Mbuzi na Ng'ombe sasa wanalipiwa kodi. Yaonekana, kuna kodi nyingi zinarudishwa lakini kwa ujumla ni ukosefu wa akili kwa wachumi wetu na hasa kipindi hiki ambacho wananchi wanastahili kupunguziwa ugumu wa maisha.

Au ni wizi wa wazi kwa viongozi wa halmashauri wanaojiamulia bila kujali huko juu watasemaje. Aliye na taarifa za wilaya zingine pia tunaomba atuletee taarifa za kadi hizi mpya zilizoanza nchini.
🤔🤔🤔
 
Suala la kulipa kodi sipingani nalo..nalo pingana nalo ni suala la matumizi ya hizo pesa zinazokusanywa na serikali hii ya wezi.

Ndio mnaenda kutajirisha wanasiasa na mafisadi wenzao ila mwanachi anaendelea kuumia kwa kukosa huduma bora na maendeleo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Bei ya hereni ni 1700 kwa Ngombe
1000 kwa Mbuzi na Kondoo

Haiwezekani mfugaji akakosa hiyo hela

Swala la malisho ya mifugo si jukumu la serikali
Dah,

Wwe jamaa naona kichwani hazikutoshi kabisa jinsi unavyotapika humu.

Kama upo huko kwenye Halmashauri au kwenye ngazi yoyote serikalini, sioni utakavyoweza kwenda mbele kikazi na aina hii ya uendawazimu.
 
Mifugo lazima ilipiwe kodi
Kodi ambayo itatumika kurusha helkopta kuonyesha matokeo ya sensa?

Tena afadhari ya hiyo taarifa ya sensa; kodi za aina hii hata haijulikani pesa huishia wapi!
 
Unaandika kama waziri tuliyenaye. Kama unataka kusaidiwa fikra, why don't you request for that instead of grappling with your ignorance?
Acha kujifanya muingereza wewe limbukeni,lete vyanzo tofauti vya mapato,na kwa nini usilipe Kodi ukiwa Kama mfugaji!?
 
Acha kujifanya muingereza wewe limbukeni,lete vyanzo tofauti vya mapato,na kwa nini usilipe Kodi ukiwa Kama mfugaji!?
Sera ya elimu sijui iweje! muingereza ni kitu gani? Tangu 2014 uko JF, lakini huna nafuu ya ufahamu.
 
Kama mwenye mifugo, hana haja mifugo yake ivalishwe heleni, inakuwaje?
Ni sheria itayoanza makali kuanzia 01/01/2023
Faini yake ni 2,000,000/
Hutaweza uza mfugo popote bila hizo hereni
Hutasafirisha popote bila hereni, uchaguzi ni wako.
Kupanga ni kuchagua
 
Nasema kodi tena kwa sababu tulikuwa na kodi ya kichwa, ikaitwa kodi ya maendeleo baadaye Utawala wa Mkapa ukaifuta. Mifugo pia ililipiwa kodi na kwa wale wakongwe, kulikuwa na kodi ya baiskeli mitaani.

Taarifa niliyorushiwa, kuna zoezi la kodi ya mifugo inaendelea wilayani Ukerewe. Mbuzi na Ng'ombe sasa wanalipiwa kodi. Yaonekana, kuna kodi nyingi zinarudishwa lakini kwa ujumla ni ukosefu wa akili kwa wachumi wetu na hasa kipindi hiki ambacho wananchi wanastahili kupunguziwa ugumu wa maisha.

Au ni wizi wa wazi kwa viongozi wa halmashauri wanaojiamulia bila kujali huko juu watasemaje. Aliye na taarifa za wilaya zingine pia tunaomba atuletee taarifa za kadi hizi mpya zilizoanza nchini.
Mifugo ni mali na inaingiza kipato kwa nini usitozwe? Unataka atozwe nani Ili wewe uharibu mazingira na kuletewa maendeleo?

Acheni upuuzi nyie.
 
Acha kuwa mbuzi
Mifugo yote pamoja na wewe inatakiwa kuwekewa hereni ya utambulisho
Hereni husika haitolewi bure
Unajisikiaje heleni kusitishwa? Kama kaluguyeye vile!
 
Ni sheria itayoanza makali kuanzia 01/01/2023
Faini yake ni 2,000,000/
Hutaweza uza mfugo popote bila hizo hereni
Hutasafirisha popote bila hereni, uchaguzi ni wako.
Kupanga ni kuchagua
Kama nawe ulihusika kutunga sheria ya aina hiyo tuna safari ndefu kuelimisha watu. Maana naona unaadika kwa majivuno kabisa, utadhani ni maamuzi ya maana. Na kwa ujinga kabisa unajiamini eti hutaweza kuuza mfugo. Yaani nchi hii ambayo wameshindwa hata kusajili pikipiki ndo isimamie hili la ng'ombe! Hata watendaji mumekuwa kama ng'ombe.
 
Back
Top Bottom