Jacksonmyula
New Member
- Nov 23, 2020
- 3
- 2
UCHUMI WA VIJANA
Nchi ya Tanzania ni nchi ambayo ina amani Tunapaswa kumshukuru Mungu kwa hilo kwa kutupa nchi yenye amani na Watanzania wenye kupenda nchi yao. Leo ningependa kuzungumzia uchumi kwa vijana Watanzania maana nchi yetu ina vijana wengi lakini maisha ya wengi yameishia kuwa duni huku serikali ikisema vijana ndiyo nguzo ya Taifa hili. Kiukweli vijana wengi wa Tanzania Tuna ndoto za kuwa na maisha mazuri kwaajili ya kukuza uchumi wa nchi na kukwamua familia zetu lakini tumekutana na pigo kubwa la kukosa hayo tuliyo yatarajia.
CHANGAMOTO KUBWA KWETU VIJANA
Changamoto ya kwanza ni ukosefu wa ajira kwa vijana walio maliza elimu ya juu. Hatukatai wanao maliza vyuo vikuu ni wengi na hakuna uwezekano wa kuwapa ajira wote walio na elimu hivyo basi wengi huishia mitaani bila ya ajira na huku wakikosa matumaini na ndoto zao hii husababisha baadhi yao kuwa matapeli kwa kutumia elimu yao.
Changamoto ya pili ni mitaala ya elimu wengi wanao maliza elimu ya juu husomea mambo ambayo kiukwel ni vigumu kwao kuishi bila ajira kwa mfano asilimia kubwa ya wanao maliza vyuo vikuu husomea Ualimu, sheria na udactari hiyo ni baadhi ya mifano tu ambayo kiukwel hao watu hawawezi kujiajili kwani walisoma kwa kutegemea ajira hivyo huishia mitaani bila kazi.
Changamoto ya Tatu ni ukosefu wa Elimu ya kujitegemea na hii ndo inaumiza sana maa mtoto ananza shule ya msingi akiwa na miaka sita hadi kuja kumaliza chuo ni miaka kumi na saba yuko shuleni akimaliza chuo anakua na umri wa miaka ishirini na tatu au zaid sasa je ataweza kujitegemea kwa kujiajili au kilimo au biashara angali yeye mda wote ni shule hivyo anakua kama kapoteza muda bure.
Hizo ni baadhi ya changamoto ambazo zina sababisha vijana wengi kuwa na maisha duni..
JE NINI KIFANYIKE ?
Kwa upande wangu natoa ushauri kwa serikali yetu ya Tanzania kuhusu kuwainua vijana kwan vijana wengi nguvu za kuleta maendeleo wanazo lakini changamoto ni ukosefu wa mitaji na elimu ya biashara pamoja na ujasiriamali lakini si wote hawana elimu ya biashara wachache hiyo elimu wanayo lakini changamoto inakuja kwenye mtaji wa biashara kwa kuwa serikali inatoa ajira kwa vijana wachache basi kwa upande mwingine hawa wanao kosa ajira wange angaliwa kwa upande mwingine kwa upande wangu Serikali ingewafadhili vijana mikopo ambayo itawasaidia kuendesha biashara zao lakini najua ni ngumu pia kwa serikali kuweza kufadhili vijana wote ila inawezekena baadhi wakafadhiliwa na serikali na baada ya hao kufanikiwa watasaidia kutoa ajira kwa vijana wengine hii itapelekea miaka ya mbeleni tuwe na vijana wengi wanao fanya biashara kubwa kubwa ndani na nje ya nchi.
Lakin siyo rahisi kwa serikali ya Tanzania kuweza kuwafadhili vijana kwasababu siyo wote watakao fadhiliwa watakua na uwezo wa kufanya biashara na kuzalisha hiyo pesa badaala yake wengine wanaweza kuipoteza hivyo kwa ushauri wangu ni vyema serikali ingeweza kutembelea vyuo vikuu na kuwapa wanafunzi mitihani ya kutengeneza makundi na kila kundi liandae mkakati/ mikakati ya kibiashara ambayo inaweza kuwa na manufaa kwa kuzalisha pesa na baada ya hapo makundi yatakayo shinda yapewe mkopo ili yaweze kufanya kama mikakati yao ya biashara inavyo sema pia makundi hayo yapewe usimamizi wa kiushauri ili kuhakikisha kua wanafanya vizuri nazani hii wakifanya kila mwaka makundi yanayo shinda yakifanikiwa yanalipa hizo pesa walizo fadhiliwa tena makundi mengine yanapewa mitaji ya biashara. Kwa kufanya hivi kwangu mimi naona hata wanafunzi wengi vyuoni watakua na akili ya ziada ya kufikilia mambo mengi zaidi na hii itasaidia uchumi wa ndani kukua kwa kasi.
NYONGEZA
Hii ni kwa upande wa fedha za Tanzania. Tena hii hasa ni kwa fedha za sarafu hizi fedha ni changamoto hasa pale unapo peleka bank alafu zinakataliwa maana kuna baadhi ya watu wengi wanao fanya biashara wanalalamika ukienda na fedha za sarafu bank wanakataa wanataka noti tupu sasa tunashindwa kuelewa kwanini sarafu zililetwa tena kulikua na noti ya shillingi mia tano lakini ikabadilishwa kuwa sarafu je hizi sarafu zina faida gani kwa wafanya biashara?
na kuna baadhi ya wengine wanasema sarafu kwanza ni nzito maana unakuta mtu anakusanya sarafu hadi za milioni moja je hizi atafanyia nin? maana kuna baadhi pia ya wafanya biashara wameanza kukataa sarafu kwani wakizipeleka bank zinakataliwa. Lakin pia wengine wanasema sarafu ni rahisi kupotea kuliko noti.
Kwa upande wangu nineiomba serikali ya Tanzania iweze kubadilisha sarafu kuwa noti tusiwe na pesa za sarafu kabisa ziwe noti tupu. Hii itasaidia sana kwa wafanya biashara wengi kwan sarafu zina onekana kama hazina dhamani kabisa katika biashara laikin pia ni mzigo kwa wafanya bishara mtu hawezi tembea na sarafu za laki moja nakuendelea maana ni mzigo kwake pia ni kero kubwa sana.
Hivyo basi kuanzia sarafu ya shilingi Hamsini hadi mia tano ziondolewe na kuletwa noti za kuanzia hamsini hadi elfu kumi. Hii itasaidia sana tena sana kwa wafanya biashara lakini pia hata bank maan sababu ya bank kukataa fedha za sarafu ni kwamba hakuna kifaa kinachoweza hesabu sarafu bank lakini pia hakuna uwezekana wa ATM kutoa sarafu sasa je bank wakipokea sarafu wanazipeleka wapi?
Kwa namna moja ama nyingine kuna baadhi ya mambo hapa serikali itapata mawazo hivyo baasi ningeomba serikali afanyie kazi haya mawazo kwa maendeleo ya jamii yetu.
Kwa kusema hayo ningependa kuwatakia afya njema na maendeleo ya Taifa letu..
Mungu ibariki nchi yetu Mungu bariki Amani ya Nchi yetu AMEN..

Upvote
0