Uchunguzi: Jinsi watu wanavyoporwa mali zao baada ya mechi kumalizika Uwanja wa Taifa, huku Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikitumbua macho

Uchunguzi: Jinsi watu wanavyoporwa mali zao baada ya mechi kumalizika Uwanja wa Taifa, huku Vyombo vya Ulinzi na Usalama vikitumbua macho

" Nitasema Kweli daima fitna kwangu mwiko "

Zikiwa zimesalia dk 30 mpira kumalizika vijana wezi , vibaka na majambazi kutoka Keko Magurumbasi , Keko Mwanga , Keko torori , keko machungwa na baadhi kutoka Chang'ombe husogea karibu na uwanja wa Taifa , wengi hujikusanya kwenye njia panda ya Taifa kwenye maghorofa ya jeshi karibu kabisa na ofisi za Takukuru Wilaya ya Temeke , wakiwa na visu , bisibisi na mapanga , hii haijalishi kama itakuwa jioni ama usiku ( japo kwa usiku hali huwa mbaya zaidi )

Eneo hili limezungukwa na maghorofa ya Jwtz pande zote , na kwa kiasi kuna maghorofa ya NHC , hatua chache kutoka hapo ni Shule ya msingi Mgulani na kambi kubwa ya Jeshi la polisi inayoanzia Kilwa road , eneo hili pia linapakana na chuo kikuu cha DUCE na kambi kubwa sana ya JKT ambako ndio kuna shule ya Sekondari ya Jitegemee , hili si eneo la vibaka wajinga wa kutoka keko kutamba , lakini kwa sasa hali ni kinyume chake , vibaka wanatamba bila wasiwasi wowote ule .

Baada ya mechi kumalizika mtu yeyote mwenye kitu chochote cha thamani iwe pochi , simu , saa au hata cheni akifika eneo hili huporwa , mara kadhaa magari huvunjwa vioo na watu huporwa mali zao huku waporaji wakikimbia kuelekea Keko machungwa kwa kupita katikati ya maghorofa ya jeshi huku wanajeshi na familia zao wakiangalia kwa macho bila kutoa msaada wowote , waporaji na vibaka hawa wakishapora na kujeruhi hupita pia katikati ya Bar ya Inferno na kukimbilia bondeni kupitia Gesti ya Lyimo na kwenda kujificha uwanja wa mpira wa Keko Juu ambao ni mali ya ccm na ambao uko karibu na kota za polisi za Mchomba line ( kota zilizoleta mgogoro miaka ya nyuma kati ya mwandishi wa gazeti la Mfanyakazi ndugu Joseph Senga na Jeshi la polisi ) , haya yanatendwa huku vyombo vyote vya dola vikiangalia kwa macho bila kuchukua hatua zozote , tena kwa miaka mingi , njia zote wanazopita vibaka hawa polisi wanazifahamu vizuri lakini hawachukui hatua zozote , Askari au mwanajeshi anayeweza kupinga hoja yangu hii ajitokeze hadharani , yanayotendwa na vibaka hawa mbele ya maeneo ya jeshi ni aibu kwa Polisi Mkoa wa Temeke ambao wengi wanajazana Uwanjani wa Taifa ili kutafuta rushwa ya kujikimu na kuwaacha raia wakiumia bila sababu mitaani .

Natoa wito kwa wote wanaoenda Uwanja wa Taifa kwenye mechi ya Simba na Yanga na kufikiria kurudi kwa kupitia njia hii basi WAJILINDE WENYEWE , tena wajihami kwa silaha nzito wakiweza , lakini kama wakitegemea ulinzi wa jeshi la polisi wasije wakalia na kusaga meno.

Uchunguzi wetu huu ni endelevu na utaendelea tena kwa kuangalia usalama wa washabiki wa soka wanaopitia Mandela road , wanaoelekea Mtoni kupitia Uhasibu na wale wanaoelekea Temeke kupitia Wailes .

Naomba kuwasilisha
wizi hauishi
 
Naunga mkono hoja upuuzi unaofanyika baada ya mechi kuisha nashindwa kuelewa vyonbo vyetu vya ulinzi na usalama vina kazi gani? Mbaya zaidi ni sehemu ambayo ndio kuna askari wengi kama polisi wameshindwa na Wakuu wa vikosi wa kambi zile wameshindwa pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wahuni Watoto wa keko kesho watamka na faida
Kutoka kwa walonyalonya

Ova
 
Siku zote kibaka ni mtu hatari na kuua sio kitu kigumu kwake kwa hiyo unapo pita katika maeneo yao nawe vaa hiyo roho

Beba zana nzuri ya kazi ondoa roho ya uwoga Usijali kuhusu kufa na usiogope kuua ukiwa muoga utachagua mwenyew kill or be killed

Then katiza hilo eneo yeyote ambaye atakuletea shobo mtie kisu fasta then kimbia

Pendelea sana holster za kuwekea kisu mguuni maana ukipigwa roba lazima nguvu zitakuisha na utaenda chini kwa hiyo ni rahisi kutoa kisu na kumchoma usoni
dahhh, tulipofika ni pabaya sana asee
 
Mheshimiwa John Pombe Magufuli hapa ndio unaona jinsi gani kuna wahusika hawatimizi wavivu wao hasa hasa wenye vyeo vikubwa
 
Back
Top Bottom