Ili hoja yako iwe na nguvu kuhusu shuhuda za uongo inabidi usimame neutral, usioneshe unaamini madhehebu gani. Vinginevyo hoja hii itaonekana ni propaganda kuzuwia waumini wenu wasiwakimbie baada ya kuwachosha na mafundisho yaleyale kila wakati. Tatueni shida za waumini wenu, fundisheni kweli neno la Mungu. Waumini wenu wamechoshwa na liturujia zenu wanawakimbieni kwenda kutafuta malisho bora kwingine. Njiani wanakutana na mbwa mwitu waliojivika ngozi ya kondoo wanawadaka na kuwararua vibaya, wanabebwa na shuhuda za uongo wakihangaika kutafuta sehemu zenye kufundisha ukweli. Usijumuishe makanisa ya kiroho na hao matapeli waliopata nguvu kwa kusaidiwa na media zao. Injili ya kweli haihubiriwi siku hizi, watu wanataka miujiza na ishara na hawaipati wanaishia kutapeliwa. Fahamu kwanza maisha ya wokovu ndio utaweza kuandika hoja yako vizuri maana utakuwa nuruni na kweli utaijua na itakuweka huru kuliko kuandika hoja hii ukiwa gizani utaonekana unafanya yaleyale unayoyaona si ya kweli. Fahamu makanisa ya kiroho