Baada ya kusikia na kuona malalamiko mengi Sana ya watia nia ndani ya ccm kuwa walioshinda kura za maoni ni wenye fedha nyingi, Sexless unit iliingia majimboni kufanya utafiti.
Tulitaka kujiridhisha juu ya maswali yafuatayo;-
1. Je, rushwa ilitumika ktk mchakato wa kura za maoni ndani ya ccm?
Utafiti wetu umebainisha pasipo shaka kuwa jibu ni NDIYO.
2. Walioshindwa wote hawakutumia rushwa?
Utafiti wetu umebainisha pasipo shaka kuwa jibu ni HAPANA. Bali walioshindwa WALIZIDIWA DAU na idadi ya wajumbe waliowapa hongo. Mtia nia aliewapa wajumbe wengi dau kubwa alipata kura nyingi. Wajumbe ni waaminifu, walimpigia kura aliyetoa dau kubwa bila hiana.
3. Watia nia waliwezaje kuwahonga wajumbe makumi au mamia bila kukamatwa na takukuru?
Watia nia wajanja sana, hivyo walichukuwa tahadhali zote. Waliepuka kumpa mtumwana (messenger) burungutu la fedha ili akawagawie wajumbe. Walihofia kwamba mtumwana huyu anaweza asiwagawie wajumbe fedha ama anaweza akakamatwa na takukuru.
Nini kilifanyika? Watia nia waliomba namba za simu za wajumbe halafu fedha zikagawanywa kwa mawakala kadhaa kisha miamala ikaanza kutembea. Halafu uthibitisho wa kwamba mjumbe kapokea muamala ulitolewa kwa watu maalum walioandaliwa na watia nia. Baasi! Sasa hapa takukuru lazima iangukie pua (haiwezi kubaini)).
Kuna maeneo namba za simu za wajumbe ilikuwa kuzipata ni mbinde. Zilitolewa na kiongozi mkubwa wa chama ktk Jimbo husika (kumbuka huyu ana namba zote za wajumbe kwa ajili ya mawasiliano ya kiutendaji). Namba za simu walipewa watia nia baadhi tu ("waliomuweka sawa" bosi wa chama) wengine walipigwa chenga na zengwe juu. Ikabidi waanze kuswampa kuanza kuzitafuta lkn muda na jiografia ya Jimbo vikawa si rafiki kwao. Wakaangukia pua.
Rushwa ndani ya chama kongwe itaisha lini?