DOKEZO Responded Uchunguzi ufanyike Kituo cha Afya Mbande, kuna matumizi mabaya ya madaraka, uonevu, ukiukwaji wa haki za watumishi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Nyakijooga

JF-Expert Member
Joined
Dec 9, 2018
Posts
524
Reaction score
829
Sisi ni Watumishi wa Umma katika Kituo cha Afya Mbande tunafikisha ujumbe huu kwa jamii tukitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa matumizi mabaya ya madaraka, uhujumu uchumi, maonevu ya kimfumo kwa watumishi, pamoja na ukiukwaji wa taratibu za fedha na maadili ya utumishi wa umma unaomhusisha kituo hicho kilichopo Temeke, Dar es Salaam.

IMG_20260427_155416_181.jpg

Kwa ufupi kuna vitendo vya uonevu, vitisho na uhamisho usiofuata taratibu za kiutumishi

Baadhi ya Watumishi ambao hawana mpango wa kujihusisha ma matendo mabaya wamekuwa wakitengenezewa mazingira ya kushinikizwa kushiriki katika matendo hayo, mfano kuongeza bei za manunuzi ya dawa na vifaa tiba.

MAONEVU YA KIMFUMO KWA WATUMISHI
Mmoja wa Viongozi wa kituo hicho amekuwa akilalamikiwa na watumishi wengi kwa madai ya kuwaonea, kuwanyima haki zao za kiutumishi, na kuingilia maamuzi yao ya kitaalamu na kitabibu bila kufuata mipaka ya mamlaka husika.

Aidha, ndani ya kipindi cha takribani miaka miwili, jumla ya takribani watumishi 12 wenye ajira ya kudumu wamehamishwa au kuondolewa katika kituo hicho kwa mazingira yanayoashiria kuwepo kwa shinikizo, hila na vitisho kupitia ofisi ya Mganga Mkuu wa Manispaa (DMO).

Kuna wezetu ambao wanahamishwa kupelekwa katika kituo kidogo (zahanati) ili kuwakomoa na kuwanyamazisha.

MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA
Kiongozi huyo amekuwa akifanya maamuzi ya peke yake ikiwemo kuleta watumishi wa mkataba, kuwapa vitengo nyeti vya fedha, na kuwalinda wanapofanya makosa, huku akiwatishia watumishi wa ajira ya kudumu kwa uhamisho.

MATUMIZI YASIYO HALALI YA FEDHA ZA UMMA
Kuna viashiria vya matumizi ya fedha za taasisi bila kufuata taratibu, ikiwemo ukarabati na malipo kwa watu wa nje ya kituo bila uwazi, huku haki za watumishi zikipuuzwa.

UCHUNGUZI JENGO LA TB & CHUMBA CHA WANAWAKE KUPUMZIKA
Uchunguzi ufanyike katika matumizi ya fedha zilizotumika katika ukarabati wa Chumba cha Mapumziko cha Wanawake pamoja na ukarabati wa Jengo la TB.

UKIUKWAJI WA MALIPO YA OVERTIME NA CALL ALLOWANCE
Hadi kufikia tarehe 17/04/2026, hakuna malipo yoyote yaliyofanyika kuhusiana na stahiki za overtime na call allowance kwa watumishi, bila kuwepo maelezo ya kuridhisha kutoka kwa uongozi husika.

Aidha, kumekuwepo na matumizi ya lugha za vitisho, kukatisha tamaa na msisitizo wa kuwazuia watumishi kudai au kuhoji stahiki zao za kisheria, ikiwemo kauli zinazoelekeza kuwa wanapaswa kutii mamlaka na kuendelea kufanya kazi bila kuhoji masuala ya malipo kwa kisingizio cha mshahara wa serikali.
IMG_20260427_155416_181.jpg

TAARIFA YA VIASHIRIA VYA TOFAUTI ZA BEI KATIKA MANUNUZI YA UMMA
Jambo lingine ni kuwa uwepo wa viashiria vya tofauti za bei katika mchakato wa manunuzi ya vifaa, nyaraka zinaonesha kuwa kuna tofauti ya bei kati ya Proforma
Invoice na ankara zilizofuata, hali hii inaashiria uwezekano wa kutokuwepo kwa ulinganifu wa gharama katika mchakato husika.

Uchunguzi ufanyike kufuatilia:- Uhalali na uhalisia wa bei zilizotumika, Uzingatiaji wa taratibu na kanuni za manunuzi ya umma, Ulinganifu na uhalali wa nyaraka zinazohusiana na manunuzi hayo.

UPIGAJI KUPITIA NAMBA YA MALIPO
Jambo lingine kuna baadhi ya Watumishi wanaosimamia kitengo cha malipo kuna muda wanasema mtandao umekata, wanafanya makusudi wakati ukiingia kwenye mfumo unaona si kweli, wanafanya hivyo ili waanze kupokea malipo kwa cash, wakitoka hapo wanasema wataingiza malipo kupitia Control Number, jambo ambalo linawanufaisha kwani baadaye kiasi cha fedha wanachoingiza hakiendani na uhalisia.

Majibu ya Serikali ~ Manispaa ya TEMEKE yajibu hoja kuhusu tuhuma mbalimbali katika Kituo cha Afya Mbande
 
Changamoto uyo mzenji chura aka kizimkazi Hana meno ju mkwe wake wizara ya afya. Pia Hana meno kabisa kama CAG katoa ripoti kisha yy kusema hayo sio mambo yake.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Nani yuko tayari kuweka ushahidi mezani bila kujificha nyuma ya anonymous post?
 
Sisi ni Watumishi wa Umma katika Kituo cha Afya Mbande tunafikisha ujumbe huu kwa jamii tukitoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wa matumizi mabaya ya madaraka, uhujumu uchumi, maonevu ya kimfumo kwa watumishi, pamoja na ukiukwaji wa taratibu za fedha na maadili ya utumishi wa umma unaomhusisha kituo hicho kilichopo Temeke, Dar es Salaam.

Kwa ufupi kuna vitendo vya uonevu, vitisho na uhamisho usiofuata taratibu za kiutumishi

Baadhi ya Watumishi ambao hawana mpango wa kujihusisha ma matendo mabaya wamekuwa wakitengenezewa mazingira ya kushinikizwa kushiriki katika matendo hayo, mfano kuongeza bei za manunuzi ya dawa na vifaa tiba.

MAONEVU YA KIMFUMO KWA WATUMISHI
Mmoja wa Viongozi wa kituo hicho amekuwa akilalamikiwa na watumishi wengi kwa madai ya kuwaonea, kuwanyima haki zao za kiutumishi, na kuingilia maamuzi yao ya kitaalamu na kitabibu bila kufuata mipaka ya mamlaka husika.

Aidha, ndani ya kipindi cha takribani miaka miwili, jumla ya takribani watumishi 12 wenye ajira ya kudumu wamehamishwa au kuondolewa katika kituo hicho kwa mazingira yanayoashiria kuwepo kwa shinikizo, hila na vitisho kupitia ofisi ya Mganga Mkuu wa Manispaa (DMO).

Kuna wezetu ambao wanahamishwa kupelekwa katika kituo kidogo (zahanati) ili kuwakomoa na kuwanyamazisha.

MATUMIZI MABAYA YA MADARAKA
Kiongozi huyo amekuwa akifanya maamuzi ya peke yake ikiwemo kuleta watumishi wa mkataba, kuwapa vitengo nyeti vya fedha, na kuwalinda wanapofanya makosa, huku akiwatishia watumishi wa ajira ya kudumu kwa uhamisho.

MATUMIZI YASIYO HALALI YA FEDHA ZA UMMA
Kuna viashiria vya matumizi ya fedha za taasisi bila kufuata taratibu, ikiwemo ukarabati na malipo kwa watu wa nje ya kituo bila uwazi, huku haki za watumishi zikipuuzwa.

UCHUNGUZI JENGO LA TB & CHUMBA CHA WANAWAKE KUPUMZIKA
Uchunguzi ufanyike katika matumizi ya fedha zilizotumika katika ukarabati wa Chumba cha Mapumziko cha Wanawake pamoja na ukarabati wa Jengo la TB.

UKIUKWAJI WA MALIPO YA OVERTIME NA CALL ALLOWANCE
Hadi kufikia tarehe 17/04/2026, hakuna malipo yoyote yaliyofanyika kuhusiana na stahiki za overtime na call allowance kwa watumishi, bila kuwepo maelezo ya kuridhisha kutoka kwa uongozi husika.

Aidha, kumekuwepo na matumizi ya lugha za vitisho, kukatisha tamaa na msisitizo wa kuwazuia watumishi kudai au kuhoji stahiki zao za kisheria, ikiwemo kauli zinazoelekeza kuwa wanapaswa kutii mamlaka na kuendelea kufanya kazi bila kuhoji masuala ya malipo kwa kisingizio cha mshahara wa serikali.
View attachment 3580284
TAARIFA YA VIASHIRIA VYA TOFAUTI ZA BEI KATIKA MANUNUZI YA UMMA
Jambo lingine ni kuwa uwepo wa viashiria vya tofauti za bei katika mchakato wa manunuzi ya vifaa, nyaraka zinaonesha kuwa kuna tofauti ya bei kati ya Proforma
Invoice na ankara zilizofuata, hali hii inaashiria uwezekano wa kutokuwepo kwa ulinganifu wa gharama katika mchakato husika.

Uchunguzi ufanyike kufuatilia:- Uhalali na uhalisia wa bei zilizotumika, Uzingatiaji wa taratibu na kanuni za manunuzi ya umma, Ulinganifu na uhalali wa nyaraka zinazohusiana na manunuzi hayo.

UPIGAJI KUPITIA NAMBA YA MALIPO
Jambo lingine kuna baadhi ya Watumishi wanaosimamia kitengo cha malipo kuna muda wanasema mtandao umekata, wanafanya makusudi wakati ukiingia kwenye mfumo unaona si kweli, wanafanya hivyo ili waanze kupokea malipo kwa cash, wakitoka hapo wanasema wataingiza malipo kupitia Control Number, jambo ambalo linawanufaisha kwani baadaye kiasi cha fedha wanachoingiza hakiendani na uhalisia.
Misukule ya humu itakushambulia wewe mfichua uovu! Ngojea wanakuja soon!
 
Nani yuko tayari kuweka ushahidi mezani bila kujificha nyuma ya anonymous post?
Mzee tuhuma kama hizi yaani wao ndiyo wana mzigo wa kuthibitisha siyo kweli.

Ni kama mwananchi akisema hua tunajibiwa vibaya kazi inakua kwa waliotuhumiwa kuprove hua hawajibu vibaya.

MWananchi hatoulizwa lini, wapi, saa ngapi na ni nani kamjibu vibaya.
 
Ushaidi serikali ikafanye uchunguzi, na huyo anaetuhumiwa asimamishwe kwanza,japo ukute anakula na watu wa juu.
Hili lipo wazi kabisa, ndiyo maana nikauliza nani yupo tayari kuutoa huo ushahidi?

Maana ni tuhuma nzito na mkubwa hawezi kukosekana hapo.
 
Mzee tuhuma kama hizi yaani wao ndiyo wana mzigo wa kuthibitisha siyo kweli.

Ni kama mwananchi akisema hua tunajibiwa vibaya kazi inakua kwa waliotuhumiwa kuprove hua hawajibu vibaya.

MWananchi hatoulizwa lini, wapi, saa ngapi na ni nani kamjibu vibaya.
Hakika, na ndiyo tatizo lipo hapo, kama nyuma ya hayo kutakuwa na mzito yoyote ndo kipengele huwa kipo hapo kwenye kutoa ushahidi.
 
Ushaidi serikali ikafanye uchunguzi, na huyo anaetuhumiwa asimamishwe kwanza,japo ukute anakula na watu wa juu.
Mzee serikali hii hii kabisa?

Binafsi nina amini huyo mtuhumiwa hayuko mwenyewe, ndiyo maana ana kuwa na kiburi cha aina hiyo, ana nguvu ya kumlinda nyuma yake.

Na tatizo ndo liko hapo.
 
Hapana mkuu nimeuliza tu mkuu, siyo kwa ubaya maana ni tuhuma nzito hiyo, na kwa namna moja ama nyingine , lazima kuna mkubwa yupo nyuma yake.
Kama ni tuhuma nzito na zinawachafua basi wakanushe kama kawaida yao
 
Samahani mkuu, hivi hicho ni kituo cha afya au zahanati?
 
Hakika, na ndiyo tatizo lipo hapo, kama nyuma ya hayo kutakuwa na mzito yoyote ndo kipengele huwa kipo hapo kwenye kutoa ushahidi.
TAMISEMI ni miyeyusho.

Mimi ninaamini hayo mashtaka yote washkaji wanaweza wasichomoke hata moja.

Mfano call allowance hua inaletwa na serikali kabisa, sasa mtu akisema hajalipwa inabidi majibu yawe kwamba serikali haikuleta pesa ya call allowance.

Hiyo ishu ya manunuzi ni ile unakuta makadirio na bei ya sokoni haviendani bei ya sokoni imezidi. Sasa ishu inakuja kikao kilikaa cha kuonyesha bei imezidi hivyo mnakubaliana kuongeza bajeti? Bajeti ya nyongeza mliitoa wapi?

Simply kama ilifanyika huyu mtoa malalamiko angekua na taarifa hivyo asingeamsha na hili.

Hapa sasa ndiyo DMO atatafuta wa kumtwisha zigo, DED atashusha lawamankwa DMO. DC ataruka na DED, DMO na MOI.

Kila mmoja atajaribu kujionyesha siyo mzembe, hapa kwenye kuruka na kukanyagana ndiyo watu wanaharibu zaidi.
 
Hapana mkuu nimeuliza tu mkuu, siyo kwa ubaya maana ni tuhuma nzito hiyo, na kwa namna moja ama nyingine , lazima kuna mkubwa yupo nyuma yake.
Hizi lawama hazina haja ya kuwepo mkubwa. Kama umefanya kazi hizi hospitali za serikali za TAMISEMI utamuelewa mleta uzi.
 
Back
Top Bottom