carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 260
- 607
Mbunge wa Australia, Helen Haines amenusurika kifo baada ya kugongwa kwa makusudi na gari nje ya ofisi yake katika mji wa Wangaratta, takribani kilomita 200 kaskazini magharibi mwa jiji la Melbourne, leo Oktoba 19, 2026.
Kaimu Msimamizi wa Polisi wa jimbo la Victoria, Ashley Mason amesema mbunge huyo mwenye umri wa miaka 65 amepata majeraha baada ya kugongwa na gari aina ya Toyota Land Cruiser na kumsababishia majeraha, yaliyomfanya Haines akimbizwe kwa helikopta ya dharura hadi Melbourne kwa matibabu zaidi.
Katika hatua nyingine, dereva aliyemgonga Haines, anashikiliwa na jeshi la polisi nchini humo, ambapo inaelezwa wamemkuta akiwa na kisu ndani ya gari.
Waziri Mkuu wa Australia, Anthony Albanese, amesema tukio hilo linahesabika kama shambulio; na kwamba bado haijafahamika nia ya mtuhumiwa, huku kikosi cha kupambana na ugaidi kikianza uchunguzi mara moja.
Chanzo : Azam tv