UCL Final: PSG Vs Bayern Munich

UCL Final: PSG Vs Bayern Munich

Beckenbauer: "I've watched PSG's games, they're one heck of a team. It'll be the most difficult game of this CL season. I can't find any weak points & I expect them to vary their playing style. I hope both teams don't hold back too much, then we can expect a wonderful final [fcb]
1598178347636.png


"It'll be a match played on equal terms. I'd say it's 50-50. Sometimes you need a bit of luck. If Bayern get that, they'll win the game"
 
Leo katika hisia zangu nayaona maajabu yanaenda kutokea huku ndani ya PSG kukiwa na ahadi nyingi kutoka kwa mwarabu wao kama mmiliki wa club.

PSG kama watashindwa kushinda mechi hii basi wasitarajie tena kufika robo fainal ya UCL.

Maoni yangu:

PSG kama watahitaji heshima ya kuwa club kubwa kama wenzao Bayern au big club ambazo zimewahi kutwaa ubingwa wa mabingwa wa ulaya, basi wanatakiwa kushinda game ya leo japo battle itakuwa kubwa sana.
Hivo basi kama leo PSG atashinda utabiri wangu ni huu

[emoji116][emoji116][emoji116]

Correct score PSG 2:1 Bavaria.

Tuko pamoja kwenye hilo
 
Kwa haya maneno kazi imeisha,
Psg pasi zake apigie huko huko golini kwake,

Bayern wanamkabia juu, yaan wanakuja kukukaba kwenye nusu yako.

Hadi kipa wako ukimpa pasi nae anakabwa.

Sioni psg akitembea game ya leo.

Akijifanya kufunguka, YA Barcelona yatamuhusu.
Kiukweli Bavarian wapo vizuri kwenye kutumia nafasi sio Kama psg
 
Kwa mtiti wa Bayern niliouona kuanzia kwa Arsenal, Tottenham, Chelsea, Barcelona, Lyon, sihitaji kujitesa kisaikolojia kwa kutabiri mambo magumu sana mwisho nikatizame mechi kwa tabu nasotea utabiri wangu utimie ili nipongezwe hapa.
 
Leo jumapili ya 23/08/2020 baada ya watu kumaliza shughuli zao, kazi itakuwa ni moja tu, huko Estadio da Luz, nchini Ureno ambapo kutapigwa Fainali ya aina yake kati ya PSG Vs Bayern Munich.

Ni fainali inayowakutanisha PSG ambao wameingia fainali yao ya kwanza dhidi ya mabingwa mara 5 wa kombe hilo Bayern Munich.

Ni Fainali inayozikutanisha timu zinazocheza mpira wa kushambulia tangu dakika ya kwanza mpaka ya mwisho, hasa Bayern Munich yenye vijana wenye kasi sana!

PSG itaingia uwanjani ikiwategemea zaidi Neymar na Mbappe huku Bayern Munich maarufu kama "The Bavarians" wakiwategemea zaidi Mshambuliaji hatari zaidi kwasasa ulinwenguni Robert Lewandowski na Thomas Muller mzee wa nafasi.

Bayern Munich anapewa nafasi kubwa ya kutwaa ndoo kutokana na soka lao linalotengeneza zaidi nafasi nyingi za magoli.

Mechi itapigwa saa 4:00 Usiku kwa saa za Afrika Mashariki!

Utabiri wangu ni baada ya mechi kuisha namuona Captain Thiago Silva wa PSG akienda kubeba ndoo! PSG atashinda 2-1

Tupia na wewe utabiri wako...
View attachment 1545677
Unaachaje kumtaja Serge Gnabry kwenye attacking ya Bayern na unaachaje kumtaja Ángel Di Mária kwenye attacking ya PSG.

Mkuu huwezi kuwa serious.
 
Back
Top Bottom