Udaktari siyo wito. Tueleweshane hapa.....

Udaktari siyo wito. Tueleweshane hapa.....

Na bado mkuu Tukiwa Tunafanya kazi tunaonekana tuna akili sana na Think tank wa Taifa kwa maswala ya afya lakini ghafla tukistaafu wanasema watutunzie Pesa kwa kuwa hatuna akili katika matumizi ya pesa..

Kingine pesa inakatwa Kodi Payee,
Halafu bado unaitwa kazi ya wito
BAsi Mkuu tupaze sauti kuisemea hii kada adhimu kwa ustawi wa taifa.

Namkumbuka Dkt Ulimboka walichomfanyia serikali hii ni unyama wa hali ya juu.

Tuwasemee hadi kisomeke
 
Huo ujinga wa wito nisha ukataa, ni ajira kama zilivyo ajira zingine. Tusichezeane akili na kunyonyana tukiwa tumejificha kwenye kilemba cha wito, wito my foot!!!
 
nitajie kodi wanazolipa walimu.. zaidi ya PAYE na CWT..
Kama madaktari Wana lalamika walimu je???? Kuishi Africa ni laaana hasa hapa kwetu Tanganyika
Daktari anaye anza kazi.
1. Ana lipa deni alilosomeshwa (wastani ni kama milion 40-60) inatgememeana na chuo.

2 Analipa practicing License kila mwaka 100K ( yaani ile kuuliza umekunywa dawa juzi, vipi leo unaweza kunywa pombe ) jamaa wana sema alipie.

3. CPD points... hizi hazina gharama maalumu.

4. Kodi ya serikali. wastani wa million tatu na ushee kila mwaka.

5. Analipa ada za MAT
6. analipa Ada za TUGHE/TALGWU etc.
7. Ana pigwa vizinga..

At the end.. kila mwenye namba yake ana uliza swali Bureeee
 
Tusipoiambia serikali ukweli tutaangamia bila maarifa.

Tunaambiwa kwamba udaktari ni wito hivyo madaktari wawe kwenye moody hiyo. Lakini hao wanaoambiwa wafanye kazi kwa mode ya wito wanakamuliwa na serikali inayopaswa kuwaatamiza na kuwalinda ili wahudumie wito wao.

Angalia/soma hii screenshot uangalie namna serikali yetu inavyojiendesha kwa UKANDAMIZAJI

View attachment 2921951

Daktari analipia leseni yake kama Wakili anavyolipia leseni. Serikali inafanya biashara na kuvuna kutoka kwenye taaluma ya udaktari. Hata usome vipi udaktari hauwezi kuruhusiwa kufanyakazi nchini bila kulipia Kibali na Kodi ya kupata kibali hiko. Pili utalazimika kulipia leseni kila mwaka. Haya yote ya nini kwa serikali inayojali afya za watu wake?

Haya ni matatizo yatokanayo na kuacha mfumo ulioshindwa kuendelea kushika hatamu za nchi. Sanduku la kura liheshimiwe

Wizara ya Afya Tanzania nawakaribisha mtueleweshe haya mambo yana mantiki gani kisekta? Mnawakamua kisha mnawaambia ni wito. Kwa nini wito huo usianzie serikalini kama mfano?
Kama ni hivi basi serikali inakosea sana.
 
Hi nchi inashida sana Yani Daktali Ili aweze kutibia watu lazima alipie leseni hi serikali inatukosea sana wananchi
Mbona madereva tunalipia leseni? Fani nyeti zote NI lazima uwe na leseñi, ukiona kazi yako huitajiki kuwa na leseñi ujuwe siyo muhimu hiyo.
 
nitajie kodi wanazolipa walimu.. zaidi ya PAYE na CWT..

Daktari anaye anza kazi.
1. Ana lipa deni alilosomeshwa (wastani ni kama milion 40-60) inatgememeana na chuo.

2 Analipa practicing License kila mwaka 100K ( yaani ile kuuliza umekunywa dawa juzi, vipi leo unaweza kunywa pombe ) jamaa wana sema alipie.

3. CPD points... hizi hazina gharama maalumu.

4. Kodi ya serikali. wastani wa million tatu na ushee kila mwaka.

5. Analipa ada za MAT
6. analipa Ada za TUGHE/TALGWU etc.
7. Ana pigwa vizinga..

At the end.. kila mwenye namba yake ana uliza swali Bureeee
Dr Matola PhD
Pitia hapa mkuu
 
Daktari ni kada yenye uelewa sana. Inahitajika akili ya kisomi kubadili mfumo huu kandamizi.

Mtu anakamuliwa kwenye leseni na Kibali kisha anaambiwa haya nenda kafanyekazi ya wito.

Sijawahi kuona popote kazi ya wito imlipishe gharama anayejitolea
Bongo wanatukamua , wanatulipisha leseni kwa ajili ya mapato ,nchi za Wenzetu mfano UK ile leseni unarenew baada ya miaka 5 , USA baada ya 2years na lengo sio mapato ni kwa ajili ya daktari kuwa assesed juu ya perfomance yake kwa ujumla kitaaluma katika interval husika , mshahara mzuri na mazingira ya kufanyia kazi mazuri , sasa njoo bongoland nchi ya ukiwa kamshahara ni kadogo na kanaonekana kakubwa kwenye makaratasi tu..Daktari anachojivunia ni jina tu.
 
Tusipoiambia serikali ukweli tutaangamia bila maarifa.

Tunaambiwa kwamba udaktari ni wito hivyo madaktari wawe kwenye moody hiyo. Lakini hao wanaoambiwa wafanye kazi kwa mode ya wito wanakamuliwa na serikali inayopaswa kuwaatamiza na kuwalinda ili wahudumie wito wao.

Angalia/soma hii screenshot uangalie namna serikali yetu inavyojiendesha kwa UKANDAMIZAJI

View attachment 2921951

Daktari analipia leseni yake kama Wakili anavyolipia leseni. Serikali inafanya biashara na kuvuna kutoka kwenye taaluma ya udaktari. Hata usome vipi udaktari hauwezi kuruhusiwa kufanyakazi nchini bila kulipia Kibali na Kodi ya kupata kibali hiko. Pili utalazimika kulipia leseni kila mwaka. Haya yote ya nini kwa serikali inayojali afya za watu wake?

Haya ni matatizo yatokanayo na kuacha mfumo ulioshindwa kuendelea kushika hatamu za nchi. Sanduku la kura liheshimiwe

Wizara ya Afya Tanzania nawakaribisha mtueleweshe haya mambo yana mantiki gani kisekta? Mnawakamua kisha mnawaambia ni wito. Kwa nini wito huo usianzie serikalini kama mfano?
Hakuna profession ambayo ni wito. Madaktari wamejawa minyoo kichwani. Ohoo Kalaga Baho.
 
Back
Top Bottom