Udalali wa kutisha wa ardhi ya nchi, Profesa Shivji aonya kuwa watawala hawaoni mbali, wanaangalia pafupi sana

S
Shivji hana utofauti na mwanafunzi wake Lissu,wote ni walalamishi,hawana suluhisho,wakosoaji ndio huwa hivyo.
Amekazania kupinga ubepari wakati hawezi kuishi kijamaa,ni mnafiki sana shivji
 
Huyo mzee Shivji nilimtoa maanani kipindi cha kusaka katiba mpya alipokubali kutumika kupotosha umma. Huenda hata sasa anaongea hivyo ili aitwe apewe chochote.
Sasa maoni si huwa yanatofautiana kulingana na mada au jambo husika.

Yaani kama kwenye katiba halikua sawa na wewe kwenye mambo ya ardhi akiwa sawa na wewe basi hafai, ni mbinafsi.

Hii sio sawa, tujifunze kukubali kutokubaliana.
 
Kichwa kimetoa maoni yake..m
 
Na vile visiwa vya znz, vinavyo kodishwa navyo vime kwenye hili dokezo au ndio hivyo hela wapate Sirikali ya mapinduzi, raia wahamie Bara
 
Sasa maoni si huwa yanatofautiana kulingana na mada au jambo husika.

Yaani kama kwenye katiba halikua sawa na wewe kwenye mambo ya ardhi akiwa sawa na wewe basi hafai, ni mbinafsi.

Hii sio sawa, tujifunze kukubali kutokubaliana.
Sina tatizo na alichokisema sasa, bali hata wakati wa nyuma kwenye katiba alikuwa anaongea hivihivi, cha ajabu akapewa kidogo kitu, akaanza kuongea kinyume na alichokuwa anatuaminisha huko nyuma kuhusiana na katiba. Inshort huwa siwachukulii serious watu vigeugeu.
 
Ndio hatari ya nchi kuongozwa na kiongozi asiye na maarifa wala maono. Uwekezaji kama hizo ndio vitu rais anaweza kushauriwa na vigogo serikalini wasio na uzalendo na wapenda rushwa. Ule mfano wa mkataba wa bandari uwe mfano kwa mikataba yote nchi hii inaweza kupatiwa na nchi ya dubai na nchi zingine wakala wa ubeberu duniani. Ni jambo muhimu sana 2025 nchi kuzingatia kupata kiongozi mzalendo mwenye uwezo na maono sahihi kwa mustakabali wa nchi.
 
Kila MTU atakufa,kifo ni Haki...lakini kwanini hawa nguchiro wengine kama shivji wasitangulie KWANZA??
 
Duh,
Silaha kubwa ya wananchi wa kawaida ambao ndiyo wengi katika kujikomboa kutoka kwa makucha ya watawala waovu ni kura zao, lakini bahati mbaya kwa Tanzania sanduku la kura halina tija
Nani kakudanganya kura za wananchi ndio silaha zao?
 
Ccm wanauza tu rasilimali zetu alafu wanaenda kununua nyumba Dubai
Akili za kijinga hizi
 
Huyu jamaa ni mfuasi wa Karl Max ila kwa sasa ideas za kina adam smith ndio zimetamalaki hawezi kueleweka na viongozi wa zama hizi ambao wengi wao wapo zama za kutumia sana (consumerism) kulipo kutafuta, kupigania na kulinda.
 
Shivji ni mpinga uwekezaji,huita kuuza
Yaani kwa akili yako finyu kabisa unadhani kila kinachofanywa na watawala wa serikali ya CCM kuanzia Mwinyi, Mkapa, Kikwete na huyu bibie Samia Suluhu Hassan ni uwekezaji?

Ndiyo maana humwelewi Prof. Issa Shivji kwa akili na mtazamo wako huu. Pole sana...

Rais aliyekuwa kinyume na sera na akili za udalali wa Maliasili za nchi kwa mabeberu alikuwa mwasisi wa Taifa hili pekee mzee Hayati Julius K. Nyerere na baadaye kuja kufuatiwa na Hayati John P. Magufuli pekee.

Hawa wengine wote ni madalali wa mabeberu wa waziwazi.

Na hali ya udalali huu kwa Sasa ni mbaya na hatari zaidi na ukifanyika katika namna ya ulafi na tamaa ya kijinga kabisa ya viongozi wa CCM na ya waziwazi kupita kiasi chini ya huyu Mama Mzanzibari Samia Suluhu Hassan.

Mbaya zaidi tena ni kuwa, maliasili zinazodalaliwa ni za Tanganyika tu huku za Zanzibar zikiwa salama!!
 
Halafu maisha yalikuwaje kipindi Cha Nyerere!?..viraka juu ya viraka,umasikini uliotopea,ukiwa na radio na baiskeli we tajiri,nilimsikia juzi redioni akihutubu,yaani alikua akichukia matajiri na kuwaita wanyonyaji,uwekezaji ni kumpa mtu mwenye mtaji afanye biashara ya bidhaa Fulani nchini kwako,watu wako watapata ajira, serikali itapata Kodi,tofauti na hapo ni akili za kimasikini na roho mbaya tu,huyo magu alilinda rasilimali gani!?
 
Baadhi ya watu mna shida kichwani. Mnajaribu kudokezwa mambo makubwa ya nchi yenu, yanavyokwenda mnampinga anayewajulisha!

HIli Taifa si la kuhoji viongozi wala kusimamia hizi rasilimali. Unamtoa Mmasai kwenye hifadhi, kwamba anaharibu mazingira, unakuja kuingia mkataba upate 10% unamuweka muarabu. Anafanya zaidi ya jamii ya kimasai kujenga mahoteli na kuwinda na tuko kimya!!!

Mimi ule mkataba wa misitu hekta milioni 8, ndiyo nilipochoka. Hii awamu itauza kila eneo. Itafikia wakati kila unapokanyaga utaambiwa huruhusiwi, ni eneo la Mfalme fulani ama nchi fulani, na uko ndani ya nchi yako. Yatafika tu tuombe uzima.
 

Hata mimi nimeshangaa kwa kweli.

Profesa anazungumza mambo makubwa ya nchi, watu wanaleta hoja za "lakini huyu mzee zamani kawahi kuwa na msimamo fulani". Sasa kwani lazima kila ishu tuidump katika kapu moja?. Kama zamani mtu alokosea ndo hivyo basi hana haki ya kupatia kwenye jambo jingine?.

Ndiyo maana Watawala wanaweza kufanya lolote nchini kwa sababu wanajua wabongo hawatajali kivile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…