Udanganyifu wakati wa kununua magari kwenye showrooms

JituMirabaMinne

JF-Expert Member
Joined
May 4, 2020
Posts
3,381
Reaction score
9,744
Hii Case nimeizoea kukutana nayo wa watu na huwa naichukulia kawaida ila leo nimeshangaa kuikuta kwenye moja wapo ya Showroom hapa Dar.

Kikawaida gari nyingi tukitaka kuangalia mwaka ambao gari hiyo imetengenezwa huwa tunaangalia lebo iliyopo kwenye mkanda (yaani seat belt).

Lakini it seems kumekuwa na mchezo wa gari kuwekwa mikanda ya gari ambayo ni ya generation moja ila miaka tofauti.

Mfano Toyota Premio generation ya kwanza zimeanzia 2001 mpaka 2007. Hivyo inaweza ikatolewa mikanda ya premio ya 2006 ikafungwa kwenye premio ya mwaka 2002.

Hapo utaambiwa hiyo gari ni ya mwaka 2006 halafu utapigwa hela. Kwa kulipa bei ya gari ya 2006 wakati ni gari ya 2002.

Bahati mbaya sana sikuipiga picha lebo ya mkanda wa hiyo gari. Ila wakati napima report ilikuja kwamba ni gari ya mwaka 2001 hivyo sikuwa na sababu ya kuangalia mkanda.

IMG_20211113_191114.jpg

Tulikubaliana bei na mtu wa sales Fresh ila shida ikaja kujitokeza alipokuja Boss na akaclaim kwamba hiyo ni gari ya 2004. Na bei akapandisha for almost 1.5m zaidi.

Hapo tukawa tumeshindwana.

Kitu ambacho nimekizoea mara nyingi, mwaka uliondikwa kwenye mkanda huwa unapishana kwa mwaka mmoja tu na mwaka ambao unakuja kwenye Diagnostic report. Hiki ndio kitu ambacho ninakifahamu.

Ila miaka ikishakuwa mingi hapo kuna walakini. Na sielewi kama hii michezo inachezwa hapahapa mjini au huko gari zinakotoka.

Hapo sijagusia suala la Km, Maana Km nilizozikuta mpaka nimeona aibu.

Anyway ukiwa unanunua gari jitahidi kurukaruka na Chasis number ya gari hata mtandaoni labda unaweza kupata taarifa mbili tatu za hiyo gari.

Unaweza pia kusoma 👇🏾👇🏾👇🏾

Thread 'Car diagnostic solutions' Car diagnostic solutions

Alamsiki
 
Sasa kitu kingine cha ajabu ni hizi crown athlete zinazouzwa Kwenye yard nyingi zinauzwa zikiwa zimeshushwa milage.... nilishangaa mwaka Jana nilienda yard Fulani kinondoni kila gari niliyouliza milage haizidi km 70000 kitu ambacho ni uongo.

Hiyo Premio ilikuwa na Around 37k...

Yaani eti kwa wastani kila mwaka imetembea 1600+Km
 
Nilikutana na mpaka gari za 120,000Km kwenye yard za wadosi kule Mwanza na siyo trucks na unaweza kuta na wao wameshusha kuipata hiyo!😁.

Najua kwa Dar huwezi kupata sedan yenye +100K Km kwenye showroom.NEVER.

Hivi hatuwezi kuwa na sheria ya kudhibiti hii kitu au siyo issue sana.
 
I wish hizi taarifa za magari wenzetu wangekuwa wanaziweka somewhere mtandaoni wakati gari inauzwa huko ili hata mtu akinunua gari huku basi akiingiza hata Chassis number mtandaoni awe anaweza kuona kila kitu.
 
Hii Case nimeizoea kukutana nayo wa watu na huwa naichukulia kawaida ila leo nimeshangaa kuikuta kwenye moja wapo ya Showroom hapa Dar.

Kikawaida gari nyingi tukitaka kuangalia mwaka ambao gari hiyo imetengenezwa huwa tunaangalia lebo iliyopo kwenye mkanda (yaani seat belt).

Lakini it seems kumekuwa na mchezo wa gari kuwekwa mikanda ya gari ambayo ni ya generation moja ila miaka tofauti.

Mfano Toyota Premio generation ya kwanza zimeanzia 2001 mpaka 2007. Hivyo inaweza ikatolewa mikanda ya premio ya 2006 ikafungwa kwenye premio ya mwaka 2002.

Hapo utaambiwa hiyo gari ni ya mwaka 2006 halafu utapigwa hela. Kwa kulipa bei ya gari ya 2006 wakati ni gari ya 2002.

Bahati mbaya sana sikuipiga picha lebo ya mkanda wa hiyo gari. Ila wakati napima report ilikuja kwamba ni gari ya mwaka 2001 hivyo sikuwa na sababu ya kuangalia mkanda.

View attachment 2009304

Tulikubaliana bei na mtu wa sales Fresh ila shida ikaja kujitokeza alipokuja Boss na akaclaim kwamba hiyo ni gari ya 2004. Na bei akapandisha for almost 1.5m zaidi.

Hapo tukawa tumeshindwana.

Kitu ambacho nimekizoea mara nyingi, mwaka uliondikwa kwenye mkanda huwa unapishana kwa mwaka mmoja tu na mwaka ambao unakuja kwenye Diagnostic report. Hiki ndio kitu ambacho ninakifahamu...

Ila miaka ikishakuwa mingi hapo kuna walakini. Na sielewi kama hii michezo inachezwa hapahapa mjini au huko gari zinakotoka.

Hapo sijagusia suala la Km, Maana Km nilizozikuta mpaka nimeona aibu.

Anyway ukiwa unanunua gari jitahidi kurukaruka na Chasis number ya gari hata mtandaoni labda unaweza kupata taarifa mbili tatu za hiyo gari.

Unaweza pia kusoma [emoji1484][emoji1484][emoji1484]

Thread 'Car diagnostic solutions' Car diagnostic solutions

Alamsiki
Km mbona 0 mkuu?
 
Hata wajapapani wakikupiga nao watakuona mkolomije....
Bora nipigwe na mjep kuliko kupigwa na hawa maboya wa mjini.

Mwaka wa 14 sawa naagiza na sijawahi kupigwa,unaagizaje Gari chini ya grade 5 na utegemee ukute imetembea chini ya 60,000km?

Gari nilizowahi kuagiza mostly Ni 4.5 grade na nikiagiza ya 4 najua itahitaji repair kidogo,ceteris peribus.
 
I wish hizi taarifa za magari wenzetu wangekuwa wanaziweka somewhere mtandaoni wakati gari inauzwa huko ili hata mtu akinunua gari huku basi akiingiza hata Chassis number mtandaoni awe anaweza kuona kila kitu.
Nilinunua Ford Everest 2003 model kutoka US,Kuna jamaa wanaitwa CARFAX wanatoa huduma ya kukupa history ya Gari(waliowahi kuimiliki, original miles,Kama ilishawshi kupata accidents etc).Unawatumia VIN tu, report yote unatumiwa.Niliwalipa $100 tu.
 
Mileage halisi inapatikana kwenye invoice ya gari husika wakati wa importation hivyo ukinunua gari dai invoice ya imoortation kwa magari yalioingia TZ kabla ya April 2021 dai inspection certificate ya Japan ile pia ina OG mileagr ila kwa gari za Singapore hua hawaandiki mileage kwenye report yao
 
Back
Top Bottom