Udhaifu wa Ripoti ya CAG 2021/2022

Ww unowasema ccm hivi hao chadomo wakipewa Nchi hawawezi lolote na wizi utazidi maradufu
 
Unatokwa povu bure tu, relax. Wizi au ufisadi wowote lazima uwe na wahusika au watuhumiwa walioiba na waliofanikisha, haiwezi kuwa ofisi nzima au yeyote tu.
CAG bila kupendekeza wahusika wa kuwajibishwa kwa kuhusika moja moja katika wizi au kushindwa kutimiza wajibu haisaidii kitu, zinakuwa kelele tu na mashindano ya kuonyesha nani anazo hasira zaidi.
 
Unataka watajwe kwa majina ama??

Sikutegemea kama uzi wako utaandika kiwepesi hivi wakati tittle yake ni heavy namna hiyo.
 
Kuwataja majina wahusika inaweza kuwa walihusika katika wizi moja kwa moja au walishindwa kuwajibika katika nafasi zao husika hadi wizi husika ukafanyika.
Kama sio part ya ToR yao inabidi iwe huko mbeleni. Wizi ukitokea lazima kuna wahusika mahususi au watu wanaopaswa kuwajibishwa . Ukaguzi lazima uwataje na usema bayana ni kina nani ili mamlaka za uteuzi, TAKUKURU na Polisi waendelee nao.
Wawataje kwa majina? Report? Sidhani kama ni part of ToR yao! Hio nadhani inaenda kwa TAKUKURU na Polisi, Wale sidhani kama Wana investigate.

Sometimes wanachoonyesha ni ile Hali ya watumishi kutokufuata taratibu sahihi za manunuzi
 
Sio lazima awe mtuhumiwa, mfano CAG anafanya ukaguzi na anagundua mhasibu wa taasisi husika sio competent au mkurugenzi ni mtupu kichwani katika mifumo ya pesa na kwa udhaifu huo unachangia wizi lazima awake bayana hilo katika ripoti kwa kuwataja ili kusaidia mamlaka za uteuzi na uajiri.
CAG ametaja alipo kagua akakuta mambo yameenda mrama, kwahivyo sio kazi CAG kufanya upelelezi ili kubaini mtuhumiwa ni nani.
Kwahivyo alipo ishia yeye basi mamlaka inayo fuata itekeleze wajibu wake.
 
Watajwe kwa majina kabisa au ofisi/cheo husika. Ripoti iseme Mkurugenzi Mtendaji, Katibu mkuu au afisa fulani ndio wanawajibika kwa wizi wa kiasi fulani.
Unataka watajwe kwa majina ama??

Sikutegemea kama uzi wako utaandika kiwepesi hivi wakati tittle yake ni heavy namna hiyo.
 
Sio lazima amtaje mtu kwasababu muongozo wake wa kazi haujamuelekeza ķufanya hivyo.
Labda sasa tupaze sauti ili bunge lifanye marekebisho ya sheria zinazo muongoza CAG
 
Siyo kazi ya Audit hiyo bali ni ya vyombo vya uchunguzi
 
Auditor hazuiwi kuonyesha mahali pesa zimepotelea, aliyemtuma anaweza kumuelekeza kufanya hivyo pia.
Siyo kazi ya Audit hiyo bali ni ya vyombo vya uchunguzi
 
Ignorance sio povu, hata wewe ni ignorant mwingine! Suala la CAG kutaja wahusika inategemea anafanya aina gani ya ukaguzi. Kama ni uchinguzi/investigation hapo ni lazima ataje wahusika kwa sababu amethibitisha hio wizi. Ila kama ni ukaguzi wa kawaida utaonyesha viashairia na kuwasilisha ripoti pccb wafanye uchunguzi.

Fahamu kwamba ripoti zilizo public ni general au summary kitu ambacho hazina details including majina. Nenda kasome kitu kinaitwa Management Letter ndio utakuta hayo majina kama alikuwa anafanya uchunguzi.

Kwa hiyo sio kosa lako ila ni ignorance tu..Shida ni ujuaji badala ya kuuliza unajifanya eti lazima, lazima.kwa standards zako au za tasnia?
 
Inawezekana kusiwe na tofauti kama mifumo na taasisi vitakuwa havijaboreshwa.
Ww unowasema ccm hivi hao chadomo wakipewa Nchi hawawezi lolote na wizi utazidi maradufu
 
Ss mtu kawaambia kakagua na hajaona source ya deni mnamlaumu? Ukute kuna block figure limepostiwa sehemu halina maelezo mtajuaje?

Kama TTCL ama wakaguliwa wengine wote wanasingiziwa si wajitokeze kukanusha walichoandikiwa kwani kuna anaye wazuia?
Mbona hakuna ambaye huwa anasema kasingiziwa?
 
Ripoti ya CAG haionyeshi viashiria vya wizi bali imethibitisha kabisa wizi kutokea na kiasi cha pesa kilichoibiwa au kupotea. Wewe ndio unabumba vi-theory vyako uchwara hapa visivyo na mbele wala nyuma.
 

Unaelewa lakini maana ya ukaguzi wa mahesabu?

Mfano halmashauri imepata hati chafu, pengine pia imekutwa na upotevu wa pesa ama matumizi ambayo sio sahihi, wewe kwa akili yako hapo ni nani anayepaswa kuwajibika?

Kila unit inakiongozi wake, anything goes wrong anaanziwa yeye.

Sasa wewe ulitaka CAG aanze kukutajia majina kwenye ripoti.

Huo unakuwa tena sio ukaguzi wa hesabu, ni ukaguzi mwingine kbs.
 
Nalewa point yako lakini kama ni hivyo itabidi waanze na wale wanaowafanyia Performance Appraisal (sijui serikalini wanaitaje)
 
Ni vigumu mtu kujitokeza katika hizo ofisi kuzungumzia hizo hoja za CAG kwa sababu hakuna watu mahususi waliolengwa na hayo madai katika ripoti ya CAG na wanajua kelele zitapigwa baada ya muda mfupi kutatulia na mambo yataendelea kama kawaida. Kama majina au vyeo vya wahusika vingetajwa ungeona jinsi watu wanatoka mashimoni kama panya waliomwagiwa maji moto.
 
Ripoti ya CAG haionyeshi viashiria vya wizi bali imethibitisha kabisa wizi kutokea na kiasi cha pesa kilichoibiwa au kupotea. Wewe ndio unabumba vi-theory vyako uchwara hapa visivyo na mbele wala nyuma.
Itakuwa najadili na mtu asiye na taarifa rasmi. Tafuta ripoti kasome kisha uje tujadili. Nimeogopa uliposema ripoti nzima inazungumzia wizi.
 
Kwamba wewe unajua kuliko CAG?
CAG sio Mtu ni Ofisi kubwa yenye watu wengi wanaopitia, kuwauliza wahusika hadi wanakuja andika na kuileta hadharani washafatilia sana.

Swala la TTCL vitabu havifutiki, CAG yeye kafatilia vitabu, kawahoji hili deni litalipwaje, wao wakajibu hawajui wanamdai nani, na ndo maana TTCL wakatoa pendekezo la kufuta 7.5bil kama deni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…