Haiko hivyo na sio kazi ya CAG kufanya kazi ya u - polisi..
Na pendekezo lako, basically linajikita kwenye utamaduni ule wa kipuuzi na wa kijinga wa miaka yote wa wenye mamlaka na maamuzi kukwepa kutenda wajibu wa kuwajibika na kuwajibishana..
Kazi ya CAG ni kumwonesha mwenye fedha (sisi wananchi kupitia tuliowapa dhamana - serikali yetu), kwamba;
1. Ulitenga kiasi hiki kwenye shirika au taasisi fulani Kwa mwaka wa fedha huu
2. Zikafika kiasi hiki kwenye shirika au taasisi hiyo ya umma.
3. Na:
✓ Zikatumika hivi au vile;
✓ Vibaya au vizuri.
✓ Kuna tija au hasara? Na kama ni hasara basi, CAG ataeleza na sababu za fedha kutumiwa vibaya pasipo kuleta tija Kwa mpango husika..
✓ Sana sana CAG anaweza kushauri na kupendekeza hatua za kuchukua pale palipo na matumizi mabaya. Na bila shaka hili hufanya kwenye kila ripoti yake ya ukaguzi..
## Kama pesa zimetumika kinyume na utaratibu, hilo ni jukumu la mwenye fedha kuchukua hatua dhidi ya watu wake. CAG yeye ni mbwa tayari alishabweka na wewe mwenye nyumba, amka angalia wezi na uchukue hatua..!