Udhaifu wa Ripoti ya CAG 2021/2022

VOTE 20 huwa haihojiwi, huko ndo kuna TISS, JW, Ikulu na wengine wasiojulikana wao hawahojiwi na hawakaguliwi
 
Ukaguzi ndio unatakiwa useme pesa zimepotelea wapi, sio kudhani au kufikiri, kama huo ukaguzi hauwezi kuonyesha muhusika anayewajibika katika huo upotevu unakuwa hauna maana sana.
 
Thank you! Kuna jingine rais alisema fedha za Plea Bargain hazijulikani zilipo zingine zimeenda China. Report inasema fedha zimewekwa kimakosa akaunti ya DPP (plea bargain) badala ya... Hakuna pahala popote Akaunti ya China inazungumziwa ndani ya report hiyo.
 
Decision makers(Bodi za Wakurugenzi, za ushauri, za udhamini, Mawaziri) na Maafisa Masuhuli(Makatibu Wakuu, Wakurugenzi Wakuu, Watendaji Wakuu, Wakuu wa Taasisi).
 
Yaani wanajulikana kwa mujibu wa Sheria ya Utumishi wa Umma, Kanuni za Utumishi wa Umma na Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma.
 
Soma ripoti vizuri.
 
Hiyo ni kazi ya DCI. Hana mamlaka ya kumtaja mtu. Yeye anataja alichokiona kwenye hesabu. Hesabu hazina jina. Wakija DCI na TCCB wanaingia ndani kuchunguza na kuchukua hatua stahiki.
 
Sio porojo,hayupo field hiyo na haelewi chochote anga hizo! Ni kusaidia na kumweleza tu
 
Haiko hivyo na sio kazi ya CAG kufanya kazi ya u - polisi..

Na pendekezo lako, basically linajikita kwenye utamaduni ule wa kipuuzi na wa kijinga wa miaka yote wa wenye mamlaka na maamuzi kukwepa kutenda wajibu wa kuwajibika na kuwajibishana..

Kazi ya CAG ni kumwonesha mwenye fedha (sisi wananchi kupitia tuliowapa dhamana - serikali yetu), kwamba;

1. Ulitenga kiasi hiki kwenye shirika au taasisi fulani Kwa mwaka wa fedha huu

2. Zikafika kiasi hiki kwenye shirika au taasisi hiyo ya umma.

3. Na:
✓ Zikatumika hivi au vile;

✓ Vibaya au vizuri.

✓ Kuna tija au hasara? Na kama ni hasara basi, CAG ataeleza na sababu za fedha kutumiwa vibaya pasipo kuleta tija Kwa mpango husika..
✓ Sana sana CAG anaweza kushauri na kupendekeza hatua za kuchukua pale palipo na matumizi mabaya. Na bila shaka hili hufanya kwenye kila ripoti yake ya ukaguzi..

## Kama pesa zimetumika kinyume na utaratibu, hilo ni jukumu la mwenye fedha kuchukua hatua dhidi ya watu wake. CAG yeye ni mbwa tayari alishabweka na wewe mwenye nyumba, amka angalia wezi na uchukue hatua..!
 
CAG inatakiwa aonyeshe mahali au mikono husika pesa zimepotelea ili serikali kupitia mamlaka za uteuzi na vyombo vya dola vichukue hatua. Kama CAG haonyeshi hivyo ndio habari za uchunguzi wa miaka hadi mitano unaanzia hapo na mwisho wa siku mambo yanapotelea hewani tu.
 
Sidhani kama hilo ni jukumu la CAG kuandika kuwa 'fulani ameiba shilingi kadhaa', kwa vile ukaguzi wake unahusu matumizi ya taasisi. Hiyo itakuwa nje ya hadidu rejea zake.
 
Amefanya hivyo mara zote ktk ripoti zake za Kila mwaka...

Na labda uwe husomagi tu. CAG huonesha Kila ikiwemo matundu zilipovujia pesa..

Mathalani, CAG anaposema "Chama Cha Mapinduzi - CCM kimetumia billion 20 pasipo kuonesha zimelipwa kwa nani na kwa kazi ipi" inakuwa haieleweki kuwa hapo kuna wizi..? Unataka aandikeje labda? Aseme Chongolo wa CCM katumia billion 20 na haieleweki zilienda wapi ndo utajua mmeibiwa????

Tatizo haliko Kwa CAG. Tatizo liko kwenye udhaifu wa mfumo wetu wa kuwajibika na kuwajibishana..!
 
Kama Chongolo ndiye aliyehusika na ulipaji huo usioleweka inabidi iwekwe wazi, kama ni muweka hazina inabidi ripoti iseme. Chama cha Mapinduzi ni kikubwa sana, ukiacha hivyo hewani tu nani sasa atachukuliwa hatua??
 
Sio kazi Yao, CAG sio Mahakama yeye anajenga hoja wahusika wakishindwa kujibu basi DPP atatumia hiyo taarifa kama ushahidi.

Wakijibu hoja inafutika.Kazi ya CAG ni kuangalia compliance
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…