Son of Gamba
JF-Expert Member
- Oct 26, 2012
- 4,720
- 6,957
Baada ya ile video ya binti wa Yombo akibakwa na wanaume 5 kusambaa mitandaoni, watu walipaza sauti na wanaendelea kupaza sauti kudai haki itendeke.
Lakini, kuna video nyingine inasambaa mitandaoni na ilikuwepo kabla hata ya ile ya yule binti kusambaa, ikimuonesha jamaa mmoja akidhalilishwa kwa madai ya kutembea na Mke wa mtu.
Inasikitisha sana, maana jamaa anaonekana uso umevimba, anavuja damu, yuko uchi wa mnyama na analazimishwa kucheza taarabu huku akikata mauno. Jamaa anaomba maji, lakini ananyimwa huku akitukanwa matusi ya nguoni.
Soma Pia:
Najiuliza swali, Je, ni sahihi Mwanaume kudhalilishwa lakini siyo sahihi mwanamke kudhalilishwa?
Kwanini tunakuwa na double standards ?
Kama tunataka haki, basi haki hiyo iwanufaishe wote pasipo kupendelea jinsia moja.

- Polisi yaanza kufuatilia tukio la Binti aliyebakwa na wanaume watatu
- Jeshi la Polisi lawakamata watuhumiwa 4 kati ya 6 waliofanya tukio la kumlawiti binti wa 'Yombo'. Wasema binti yupo salama