Udhalilishaji: Video ya PNC akimuomba msamaha Ostaz Juma na Musoma

Daah kweli hii nayo imebuma, poyee sana pnc umebuuuuma dogo
 
NAPITA tafadhali tutambulishe tusiofahamu. Aliyepigiwa magoti ni nani na anayepiga magoti ni nani? Wana mahusiano gani?

Msanii wa kundi la Mtanashati Intertainment Pnc,akimuomba msamaha Big boss wa kundi hilo Ostaz Juma Namusoma.
 
Kwa kitendo kile PNC,naamini kajishusha sana sio heshima yake tu hata kimuziki nadhan ndo kajimaliza kbisa.pole sana mdogo wangu lakini bado unayo nafaxi maana una saut nzur sema hujajijua.halafu sikuhiz naona unaimba komedy sijui mchiriku,kwan ujuz wa kutunga nyimvo za maana kama mbona na ile ya mwanzo mama eenda wapu??,angalia tena washur wako kijana
 

Sijasema naunga mkono kwa video hii kuwekwa hadharani, la hasha....mimi nimepingana na wanaombeza ustaadhi kwa jukumu alilojipa la kudili na wasanii.

Ingawa pia nashawishika kuhoji ni mazingira/sababu gani haswa zilizopelekea video hii kuwepo hapa.

Kwa uzoefu wangu juu ya wasanii wetu, huwa kweli wana tabia za "kisanii", kwa mfano....kufanya jambo fulani nyuma ya pazia na anapokuja hadharani (kwenye media) anaongea ya kwake..hasa kwa lengo la kuonekana yeye ni msafi na meneja ndio tatizo.....kwa mtindo huu hata wewe na mimi sidhani kama linapendeza....na wasanii kama kina Dogo janja ni mfano mzuri wa wakoroga mambo kwa mtindo huo....

Pili, ni hulka tuliyojijengea kuwa kuomba msamaha ni kujidhalilisha.....hizi ni hisia potofu ndio maana mnaona pnc amedhalilishwa/amejidhalilisha.......mimi sioni hivyo, na hii video haina tatizo lolote.

Anayempiga mwenzake picha ya uchi kwa maridhianao na baadae kuiweka mtandaoni, kwangu huo ndio udhalilishaji....lakini mtu kuomba msamaha ni jambo la kawaida.
 
Mnaomponda PNC hamjui tu shida wanazopata wasanii wa bongofleva. dah.
Hawa majamaa wakina Ustaadhi Juma, Fella, Babu Tale, etc sio watu wazuri ata kidogo kwa matumizi ya nyumbani. Yaani ni wanyonyaji zaidi ya wewe unavyodhania.

PNC hana kismart tu. Jamaa anajua sana sema mashabiki ndio hawana nyota nae. Ebu kumbushie kazi zake tokeaga Mbona (ft Mr Blue) hadi Imebuma. Dogo hakati tamaa anazidi kukaza tu. Nishawahi mkuta PNC anafanya show Ifakara, sijui niseme disco vumbi au floor vumbi (No offense). Yaani washabiki ata hawaoneshi kuguswa nae, jamaa anajitahidi kuimba LIVE ila wapi. Alifunikwa na wasanii local wa palepale ambao walikua wanaimba kwa playback. PNC ni jembe (Kwa wale wanaotambua music) na jamaa anajituma sana aisee.

Wasanii wa bongo wengi elimu hakuna. Sio lazima ile ya darasani, ata ile ya maisha tu (Elimu dunia). Wao wakishine siku 2 tu basi wanajiona wao ndio wao. Ni kweli kama mnavosema wangeweka kamshikamano flani kisha wamuondoe mnyonyaji. Sasa tatizo wengine masnitch kati yao, wanazidi jipendekeza kwa matajiri wao. Mfano hai ni TMK family kipindi kile, Juma Nature alitaka kufanya mapinduzi, ila Masnitch Tembele na Chege wakaongwa na kuhaidiwa vinono wakazingua. Unadhani woote wangeondoka pale ingekuaje? Cheki pia wakina MB Doggy, Pingu na Desso, Z Anthon wa Tip Top Connection. Dah.. Nyie acheni tu.

Hivi serikali ikisema iwasaidie hawa si itaanza kuwadai na kodi katika mauzo yao? Utasikia TRA wanawapa mashine za EFD wasanii wote Tanzania. Hapo sasa ndio hali itakavokua worse.
 
Challenges katika maisha can be like stepping stones,its just a matter of how u view them,tatizo hawa wasanii wetu wanashindwa kabisa kuhandle challenges mwishowe ndo wanaishia kujidhalilisha hivi...very sad!
 
Alichokifanya Ostaz Juma siyo sahihi kabisa ila wasanii nao wajifunze kuwa na adabu

Haya ni maneno ya PNC baada ya kuzinguana na Ostaz

Fuatilia hapa kwa habari kamili

Picha: PNC kumpigia magoti Ostaz Juma ni mfano wa jinsi wasanii wengi wanavyodhalilishwa - Bongo5
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…