Sijasema naunga mkono kwa video hii kuwekwa hadharani, la hasha....mimi nimepingana na wanaombeza ustaadhi kwa jukumu alilojipa la kudili na wasanii.
Ingawa pia nashawishika kuhoji ni mazingira/sababu gani haswa zilizopelekea video hii kuwepo hapa.
Kwa uzoefu wangu juu ya wasanii wetu, huwa kweli wana tabia za "kisanii", kwa mfano....kufanya jambo fulani nyuma ya pazia na anapokuja hadharani (kwenye media) anaongea ya kwake..hasa kwa lengo la kuonekana yeye ni msafi na meneja ndio tatizo.....kwa mtindo huu hata wewe na mimi sidhani kama linapendeza....na wasanii kama kina Dogo janja ni mfano mzuri wa wakoroga mambo kwa mtindo huo....
Pili, ni hulka tuliyojijengea kuwa kuomba msamaha ni kujidhalilisha.....hizi ni hisia potofu ndio maana mnaona pnc amedhalilishwa/amejidhalilisha.......mimi sioni hivyo, na hii video haina tatizo lolote.
Anayempiga mwenzake picha ya uchi kwa maridhianao na baadae kuiweka mtandaoni, kwangu huo ndio udhalilishaji....lakini mtu kuomba msamaha ni jambo la kawaida.