Wanabodi,
Katika karibu kila jambo, kuna mazuri na mabaya yake, kama ilivyo kwa ukoloni, japo wakoloni walitunyonya, pia kuna mazuri, walituachia, ikiwepo elimu, maendeleo na dini ya Kikrito, vivyo hivyo pamoja na mazuri ya Waarabu kuvivamia visiwa vya Zanzibar na Pemba na kuvitwaa kama mali yao, miongoni mwa mazuri waliyoyaleta Waarabu hawa, ni Dini ya Kiislamu. Lakini pamoja na mazuri haya, sio vibaya kama wasiofuatilia historia, wakayajua madhila yaliyowakuta ndugu zetu Wamatumbi, wakati wa utawala dhalimu wa Sultani, kwenye visiwa vya Unguja na Pemba.
Naomba kukiri, nimekuwa inspired kupandisha bandiko hili kutoka na mada hii
Sultani gani aliye na shutuma za mauaji Zanzibar
ya Mkuu Maalim
Mohamed Said
yenye lengo la kuonyesha kuwa Yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ndio pekee yaliyosababisha mauaji Zanzibar, simply because aliyeuwawa kwenye Mapinduzi yale, ni Mwarabu, yaani ndio binadamu, lakini Wamatumbi wote waliouwawa vifo vya kikatili chini ya mokono ya Waarabu, wao sii kitu!.Mkuu Maalim
Mohamed Said
, kwa heshma na taadhima, nakuomba kwanza acha chuki zako na wamisionari, pili hata kama lengo lako ni kuutetea Uislamu, lakini mara moja moja kuwa mkweli toka ndani ya nafsi yako, kwa sababu naamini kabisa unayajua fika madhila yaliyowapata ndugu zetu Wamatumbi wakati wa kipindi chote cha utumwa chini ya Wavamizi Waarabu na utawala wao dhalimu!.
Hizo picha japo ni za kuchorwa, kiukweli kilichowapata ni kibaya kuliko hata hicho kilichochorwa!. Chini ya utawala dhalimu wa Waarabu, watumwa wote wanaume walihasiwa!, lengo la kuwahasi wanaume ni ili kuzuia wasizaane, kitendo cha mwanamke kubeba ujauzito miezi 9 kisha kuzaa mtoto na kumsubiri hadi akue, itakuwa ni hasara, na hivyo kupunguza kasi ya mahitaji ya watumwa wapya!.
Watumwa wa soko la Zanzibar waliouzwa Arabuni na Bara Hindi, ambapo baada ya kufika kule, wanaume wote walifanyiwa ukatili wa ajabu kwa kuhasiwa ili wasizaane, na walifanyishwa kazi za shokoa. Wanawake walifanywa wajakazi, kazi za wajakazi zinajulikana, wenye bahati zao, walifanywa masuria, wasio na bahati waliuliwa na wengine kujifia, ndio maana hakuna kizazi cha watu weusi India na Arabuni, hao machotara, ni kwa baadhi ya Waarabu wenye utu na roho nzuri, lakini the rest ni unyama unyama tuu!.
Idadi kubwa kizazi chotara cha machotara, ni Wanaume dhalimu wa Kiarabu, kuwaingilia kwa nguvu watumwa wa kike ambao walinunuliwa mahsusi kama wajakazi, na pale waliposhika ujauzito, wamiliki walikuwa huru, kuwafanya chochote watumwa wao, ikiwepo kuwatesa, kuwapiga hadi kuwaua kwa ukatili wa hali ya juu!. Mtumwa mwanamke baada ya kuingiliwa ki nguvu, yaani kubakwa, ikitokea akashika ujauzito, mwanamke yule aliuwawa kwa kuwatoboa tumbo, kutoa, kiumbe ambacho ndicho kilizikwa kama binadamu, na mwili wa mtumwa ulifukiwa tuu kama mzoga!.
Jee wajua kuwa hata baada ya kupigwa marufuku kwa biashaa haramu ya watumwa duniani kote, biashara hii iliendelea kufanyika Zanzibar kwa siri?!. Jee wajua kuna njia za chini kwa chini zimechimbwa Bagamoyo na Zanzibar ambapo watumwa walifichwa kwenye mapango na kupitishwa chini kwa chini hadi baharini?
Jee ulikuwa unajua kuwa kila Sultani, wake zao na watoto zao, walipokufa, walizikwa na watumwa hai?!. Jee wajua kwenye jengo la Beit Al Ajab, kwenye kila milingoti hapo, ndani walimuweka mtumwa hai mwanamume?!.
Jee wajua waliofanikisha kukomesha biashaa ya Utumwa Zanzibar ni akina nani?!. Kwa kusaidia tuu, waliokomesha biashara hii dhalimu Zanzibar ni wamisionari, ambao waliingia kabisa mkatataba na Sultani dhalimu wa Zanzibar, ndipo ikukubaliwa kuwa watumwa wote wenye kutaka kuwa huru, lazima wagombolewe kwa wale matajii wao kulipwa fedha, ambapo hao wamisionari, waliwalipia fedha kuwagomboa, na ndipo wakaanzisha kanisa la kwanza kabisa Afrika Mashariki, lilianzia Zanzibar, na waumini wa kwanza, ni watumwa waliogombolewa!.
Jee wajua kitu walichofanyiwa Waarabu dhalimu hawa baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, ilikuwa ni katika kujibu tuu au payback ya "what goes around, comes around?!", ila hapa naomba kukiri wazi, kuwa sio Waaabu wote kabisa walikuwa madhalimu kwa kuwatenda vibaya watumwa wao!, wako Waarabu ambao waliwatendea wema watumwa wao, na wamisionari walipotaka kuwagomboa, watumwa hao walikataa kwa ridhaa zao, hivyo wakaendelea kubaki utumwani kwa ridhaa zao wenyewe!.
Wako Waarabu, waliwapenda watumwa wa kike, japo waliwanunua kama vijakazi kwa ajili ya kuwafanya watumwa wa mapenzi, lakini wapo waliotokea na kuwapenda kwa mapenzi ya dhati, wengine wakawaoa na kuwa masuria, na wakawazalia watoto!. Namfahamu mmoja wa watoto wa Sultani ambaye alizaliwa na suria, na yungalipo hai hadi leo!.
Hii ni Ripoti ya aliyetumwa na utawala wa Waingereza kufuatilia kilichokuwa kinafanywa na serikali dhalimu ya Sultan, baada ya kupigwa marufuku biashara ya utumwa.
Pitia hapa
A report on slavery and the slave trade in Zanzibar, Pemba ...
Na kwa vile wengi wetu ni wavivu, hatupendi kusoma kujiongezea maarifa bali tunapenda kupikiwa, kupakuliwa, kulishwa, kutafuniwa, sisi kazi yetu ibaki kumeza tuu, hivyo na mimi nitawatafunia sehemu chache chache za ripoti hii na kuzitafasiri kwa ajili ya wale wenzangu na mimi!.
"They complained that the Arabs treated them harshly", yaani Waarabu wanawatesa!.
In Zanzibar a good many people had been telling me how slaves were suffering in the handa of Arabs!. At Chaki Chaki I walked into a tumble-down I found a number of slaves male and female, heavily chained and fettered". Nilikuta makundi ya watumwa wake kwa waume wamefungwa minyororo!".



Hizi picha wajemeni sio picha ya kuchorwa, ni picha za kweli na halisi zilizopigwa na kamera za wadhungu!.
Lengo la uzi huu sio ubaguzi, au kuwakumbusha machungu ya Waarabu, bali ni kujikumbusha tuu, na kuwaelimisha baadhi ya wenzetu, wasiowajua hawa Waarabu wa Unguja na Pemba waliwafanya nini mababu zetu!.
Ila pia naomba kutoa Maangalizo muhimu yafuatayo.
1. Tuwe makini sana na watu waliofilisika kiakili ambao watachanganya Uarabu na dini ya Kiislam simply because, Dini ya Kiislamu inatumia lugha ya Kiarabu!. Masikini muflisi hawa, hawajui kuwa hata Ukiristo umeanzia Arabuni. Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mwanae wa kwanza Ismail, aliyezaa na mjakazi wa ki Misri, na Wakristo ni uzao wa Isaka aliyezaa na mkewe Sara. Hata Yesu Kristo, licha ya kuzaliwa Isael, alikulia Misri na alizungumza lugha ya Kiarabu!. Hapa mimi nazungumzia udhalimu wa Waarabu kama jamii na sio dini ya Kiislamu.
Udhalimu ni udhalimu tuu hauna dini, wala kabila, wala jamii, kwa sababu kwenye udhalimu sio Waarabu tuu peke yao ndio madhalimu, watu wa mataifa mbalimbali wamefanya udhalimu kwa watu wa mataifa mengine, na mfano mzuri ni udhalimu wa Wajerumani kwa Mayahudi chini ya Hitler ulioitwa Halocust ambapo Hitler aliwaua Wayahudi zaidi ya milioni 6 kwa ukatili wa ajabu!, ila kwenye biashara ya Utumwa Unguja, Pemba, na Arabuni, watumwa hawa walihasiwa hivyo kufanyiwa genoside na wahusika sii wengine bali ndugu zetu hawa hawa Waarabu ambao leo tunakula nao, tunakunywa naa na kufurahi nao kwa vile tumeishasahau, yaliyopita sii ndwele!.
2. Kwenye biashara ya utumwa, waliokuwa wakikamata watumwa, sio Waarabu, Waarabu wao walikuwa ni wafanyabiashara ya watumwa kwenye soko kuu la watumwa la Zanzibar, wakitokea Bagamoyo, na wanunuzi wakuu wa watumwa toka soko la Zanzibar kwa ajili ya kuwasafirisha kuwauza Uaabuni na India, ambako kote huko baada ya kufika, watumwa wanaume walihasiwa!. Waarabu pia ndio walikuwa wamiliki wa watumwa katika mashamba ya Zanzibar na`Pemba, ambapo nako watumwa wanaume walihasiwa, wanawake walifanywa vijakazi na ndio wazazi wa machotara wa Zanzibar na Pemba, wengi ni baba Mwarabu, mama uzao wa watumwa wanawake wenye bahati, ambao hawakutumbuliwa mimba za Waarabu!.
Upatikanaji wa watumwa kutoka bara pia ulihusisha baadhi ya watawala wakiwemo machifu ambapo baadhi ya wahalifu waliostahili adhabu za vifo katika jamii zao, badala ya kuuliwa na kuwa hasara jumla, waliuzwa, utumwani, lakini watumwa wengi ni watu tuu wa kawaida wasio na hatia yoyote ambao waliwamiwa na kukamatwa kwa nguvu, wakiwemo wanawake na watoto!. Zoezi la ukamataji watumwa pia lilihusisha vitendo vya ukatili, ambapo wengi watumwa hawa, waliuawawa katika purukushani, na wengine wengi walifia njiani na miili yao kuachwa ikioza, miili yenye bahati ilifanywa vitowea vya wanyama wa porini. Kwenye misafara hiyo, ndugu zetu waliteswa sana mateso ambayo hayazungumziki walioishiwa nguvu, walipigwa hadi kifo ila hakukuwepo na kamera ya mzungu wa kutupigia picha kuja kutuleta humu!.
3. Waarabu ninaowazungumza hapa, ni wale Waarabu madhalimu na makatili wa wa enzi zile za utumwa ambao wengi wao, mwaka 1964, walifurushwa kutoka Unguja kwenye yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964!, ila waliofurushwa ni wale tuu waliokuwa Zanzibar. Waliokuwa Pemba hawakuguswa. Hawa Waarabu wa leo, ni vizalia vya Waarabu wale wale, ila hawa wa sasa, ni Waarabu wema,wastaarabu kama Waarabu wa sasa, wenye roho nzuri, sio wakatili, sio wadhalimu na wanawapenda watu weusi na kuwaoa kwa mapenzi, huku wanawake wao, wakiwapenda weusi na wakiolewa nao japo mwanzo ilikuwa ni kwa kulamishishwa na Karume, hivyo nashauri, kwa siku zijazo, hata Waarabu hawa, ama machotaa wao, wakishiriki tena uchaguzi, wakashinda kwenye uchaguzi kwa haki, wapewe tuu nchi watawale kwa sababu Waarabu hawa sii wale!, wasinyimwe kutawala eti kwa sababu tuu ni Waarabu wale wa mwanzo na wa enzi za utumwa, walikuwa madhalimu, hivyo kuendelea kudhani hata hawa wazaliwa wao pia lazima ni madhalimu!, kwa kanuni ya mwana wa nyoka ni nyoka!.
Mwana wa nyoka sii lazima awe nyoka, kwa sababu hata shetani mwanzo alikuwa malaika!, hivyo Waarabu hawa wa sasa ni Waarabu wema, ni wenzetu na ni sehemu yetu!, ukifanyika uchaguzi tena, wakishinda, wapewe tuu nchi!.
Paskali
Wakristo Wanapanga Biashara Ya Utumwa
Watumwa walikuwa wanachukuliwa kutoka hata katika wakati wa Ufalme wa Kirumi, lakini “biashara halisi ya Utumwa” ilianza mnamo karne ya 16 baada ya ujio wa mataifa ya Kikristo ya Ulaya. Edward A. Alpers wa Chuo Kikuu cha Dar-es Salaam, anaandika kwamba; “kama tunavyoleta utofautisho baina ya biashara inayoambatana katika watumwa ambayo ilichuruzika katika sahara kutoka magharibi mpaka kaskazini ya Afrika kuanzia siku za nyuma sana za wakati wa utawala wa Ufalme wa Kirumi, kwa upande mmoja, na kioja tunacho kiita The West African Slave Trade kwa upande mwingine, kwa hiyo lazima tulete tofauti hiyo hiyo kwa Afrika ya Mashariki.”
1
Walter Rodney pia wa Chuo, Kikuu cha Dar es Salaam, anaanza kuandika kijitabu chake “West Africa and the Atlantic Slave-Trade kwa maneno yafuatayo: - Wakati wote lazima ikumbukwe kwamba biashara ya utumwa iliyo;fanyi- ka katika bahari ya Atlantiki” lilikuwa ni tukio katika histo- ria ya dunia, iliyo husisha mabara matatu – Ulaya, Afrika na Marekani.
Watu walio toka kwa dhamira ya kutafuta watumwa walikuwa Wazungu waliotoka katika kila nchi kati ya Sweeden kwa upande wa Kaskazini na Ureno kwa upande wa magharibi. Wareno walifika Afrika ya Magharibi muda mfupi kabla ya kuingia nusu karne ya kumi na tano. Mara moja na kwa haraka sana walianza kukamata (watumwa) Waafrika na kuwapeleka kufanya kazi Ulaya kama watumwa, hususan katika Ureno na Hispania. Lakini maendeleo muhimu sana kwa biashara hii ya utumwa yalikuwa katika karne ya kumi na sita, ambapo mabepari wa Kizungu walitambua kwamba wangepata faida kubwa sana kwa kutumia nguvukazi ya Waafrika kuujenga na kuuendeleza utajiri wa nchi zote za Amerika.
Matokeo yake, Waafrika walipelekwa Amerika ya kaskazini, Amerika ya kati, Amerika ya kusini na Visiwa vya Caribbean kwa ajili ya kukidhi haja ya nguvukazi ya watumwa kwenye machimbo ya dhahabu na shaba, na kwenye mashamba ya kilimo cha mazao ya miwa, pamba na tumbaku. Biashara hii mbaya ya kununua na kuuza binadamu ilidumu kwa kipindi cha miaka (400) mia nne, kwani Atlantic slave-Trade (Biashara ya Utumwa wa kupitia bahari ya Atlantiki) ilikoma mwishoni mwa miaka ya 1870.
“Mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu jinsi Biashara ya Utumwa katika bahari ya Atlantiki ilivyopangwa huko Ulaya, na kuhusu faida kubwa iliyokusanywa na nchi kama Uingereza na Ufaransa. Mambo mengi yanaweza kusemwa kuhusu safari za kutisha kutoka Afrika hadi Marekani kuvu- ka bahari ya Atlantic. Waafrika walipangwa kama dagaa kwenye meli za kubeba watumwa, na matokeo yake walikufa wengi sana.”
2
Na dagaa walioje! Kwa maelezo zaidi kuhusu upakiaji huu wa watumwa kwenye meli, soma taarifa ifuatayo: - Moja ya hati yenye kuuvunja moyo sana katika nyaraka zote zinazotisha ni “Plan of the Brookes,” mpango mbaya sana wa karne ya kumi na nane wa kupanga watumwa kwenye meli ya kubeba watumwa ‘Brookes’… Kwa mahesabu sahi- hi, teknolojia ya kushtua ilitengenezwa - futi na inchi, chumba cha kusimama na nafasi ya kupumua iliwekwa kwa matumaini ya faida kubwa. Mtu mmoja Bwana Jones anapendekeza kwamba wanawake watano wahesabiwe kama wanaume wanne, na wavulana watatu au wasichana watatu wafanywe kuwa sawa na watu wazima wawili … kila mtumwa mwanaume aruhusiwe futi sita kwa futi moja na inchi nne (1’4”x6’) kama nafasi ya chumba chake, kila mwanamke alipewa nafasi ya upana wa futi tano na inchi kumi na futi moja na inchi nne…. (5’10”x1’4”); na inaendelea hivyo mpaka kila mtu anapata nafasi – watumwa 451.
Lakini Muswada wa Bunge unaruhusu watumwa 454. Kwa hiyo hati hiyo inahitimisha kwamba kama watumwa watatu zaidi wangeweza kuwekwa kwa kubanwa katikati ya wale waliotamkwa kwenye mpango, mpango huu ungeweza kuchukua idadi ile ile ambayo imeelekezwa kwenye muswada.
3
Mara Waafrika walipofikishwa upande mwingine wa bahari ya Atlantic, kwa hakika walikuwa katika “Dunia Mpya”, iliyojaa ukandamizaji na ukatili. Taarifa ifuatayo inaweza kusaidia kuelewa hali ilivyokuwa wakati huo. Rodney anaandika:
“Kuanzia wakati walipofika (Wakristo) Wazungu hadi 1600, takriban Waafrika milioni moja (1, 000,000) walichukuliwa kwenye meli za kubeba watumwa. Wakati wa kipindi hicho, Wareno walikuwa ndio wafanya biashara wakuu wa biashara ya watumwa huko Afrika ya Magharibi. Ama wali- wapeleka Waafrika huko Brazil, ambayo nchi hiyo ilikuwa koloni lao, au vinginevyo waliwauza kwa waloezi wa Kihispania huko Mexico, Amerika ya kati, Amerika ya Kusini na visiwa vya Caribbean. Mnamo karne ya kumi na saba, kiasi cha Waafrika wapatao milioni saba hadi nane kutoka Afrika ya magharibi walivushwa bahari ya Atlantic.
Wadachi walijumuika na Wareno kama wafanya biashara wakuu wa biashara ya utumwa mnamo karne ya kumi na saba, na karne iliyofuata Waingereza wakawa wafanya biashara wakubwa kushinda wote wa biashara ya utumwa. Wakati biashara ya Utumwa katika bahari ya Atlantiki ilipofikia kileleni mnamo karne ya kumi na nane, meli za Kiingereza zilikuwa zinachukua zaidi ya nusu ya jumla yote ya watumwa na idadi iliyobaki iligawanywa baina ya Wadachi, Wafaransa, Wareno na Wadane (Danish).
“Ilipofika karne ya kumi na tisa, palikuwepo na mabadiliko mengine ya watu ambao walishika nafasi mbele katika kuinyonya Afrika. Nchi za Ulaya zenyewe hazikushiriki kikamilifu kwenye biashara ya utumwa, lakini badala yake Wazungu ambao waliloea Brazil, Cuba, na Amerika ya Kaskazini ndio ambao walipanga sehemu kubwa ya biashara. Waamerika (U.S.A) ndiyo katika kipindi hicho hicho tu walipata uhuru kutoka kwa Waingereza, hili lilikuwa taifa jipya (U.S.A.) ambalo lilikuwa na mgawo mkubwa kabisa kuliko wote katika biashara ya watumwa katika biashara ya Atlantiki katika kipindi cha miaka hamsi- ni ya mwisho, kwa kuchukua kiwango kikubwa zaidi cha watumwa kuliko ambavyo imewahi kufanya huko nyuma.
“Ilipoanza “biashara ya watumwa ya Atlantiki kwenye pwani ya Afrika ya Magharibi, ilichukua utaratibu wa kutu- mia nguvu moja kwa moja wa Wazungu kuwashambulia Waafrika waliokuwa wanaishi karibu na pwani. Mabaharia wa kwanza wa Kireno walipofika kwenye pwani inayoju- likana leo kama Mauritania, waliacha meli zao na kuanza kuwawinda watu waitwao, Moors watu walioishi katika jimbo hilo. Kwa kweli, hii haikuwa biashara hata kidogo – ilikuwa uvamizi wa nguvu. Hata hivyo, baada ya mashambulizi kadhaa ya kushtukizwa, Waafrika wa pwani wakawa na kawaida ya kulinda kwa zamu na walijilinda kwa nguvu dhidi ya washambuliaji wao Wazungu.
Katika kipindi kifupi tu, Wareno walitambua kwamba uvamizi haikuwa mbinu inayofaa na iliyo salama katika kujaribu kuwapata watumwa. Zaidi ya hayo, pia walitaka dhahabu na bidhaa zingine za Kiafrika, ambazo wangeweza tu kuzipata kwa njia ya kununuliana na kuuziana kwa amani. Kwa hiyo badala ya kuvamia, Wareno waliona afadhali kutumia bidhaa zilizo tengenezwa kiwandani ili kuwatia moyo Waafrika kubadilishana na bidhaa zao na hata kuweza kuwafikisha mateka wa Kiafrika kwenye meli za Wazungu kwa urahisi. Mpango huu haukufanywa na Wareno pekee, lakini hata wazungu wengine wote walitambua na kukubali kwamba huo ulikuwa mpango mzuri zaidi wa kupata bidhaa hapa Afrika; na ilikuwa kwa njia hii waliweza kupata mamilioni mengi ya Waafrika.”
4
Akifafanua juu ya kipengele hiki cha biashara ya watumwa, mwandishi anasema: “Moja ya vitu muhimu sana ni kutambua jambo liumalo sana na lisilo pendeza kwamba walikuwepo Waafrika ambao waliwasaidia na kushirikiana na Wazungu katika kuwafanya Waafrika wenzao kuwa watumwa. Maana yake ni kwamba hatuwezi kuchukua msimamo dhaifu na kusema kwamba watu weupe walikuwa wabaya sana na watu weusi walikuwa waathirika (katika kuangamia). Mfano unaofaa na sambamba ambao ungeweza kusaidia kuelewa yale yaliyotokea katika Afrika ya Magharibi wakati wa kipindi cha karne za biashara za watumwa unaweza kuonekana hapa Afrika leo, ambapo viongozi wengi wanashirikiana na mabeberu wa Ulaya na Marekani (U. S. A.) kwa lengo la kuwanyonya na kuwakan- damiza Waafrika walio wengi.
Hatimaye, Waafrika wa Afrika ya Magharibi walifikishwa kwenye hali ya “uza au uuzwe.” Hapa suala la bunduki lilikuwa na umuhimu maalum. Kuwa na nguvu, serikali ili- hitaji bunduki, lakini ili kupata bunduki kutoka kwa wazungu, Waafrika ilibidi kuwapa Wazungu watumwa na wao kupewa bunduki. Watawala wa Kiafrika walijikuta wenyewe wanawauza watumwa ili wapate bunduki ambazo ziliwawezesha kuwakamata raia wao na kuwauza kama watumwa ili wanunue bunduki nyingi zaidi. Hali hii inaweza kuelezewa, kama “ubaya juu ya ubaya (mzunguuko unaoashiria kukwama).” Watawala wa Kiafrika ambao waliwasaidia wazungu hawasameheki moja kwa moja, lakini inafafanua jinsi gani mwishoni hawakuwa washirika halisi wa Wazungu bali walikuwa watumishi au vibaraka wa Wazungu.”
5
Na kanisa lilikuwa linafanya nini wakati wote huo? Msikilize mwandishi huyu huyu anasema; “Kwa sababu faida kubwa sana ilikuwa inapatikana kwa kuwachukua watumwa kutoka Afrika, Wazungu walikataa kuzisikiliza dhamiri zao. Walifahamu kuhusu mateso yaliyo wapata watu katika Afrika, ndani ya meli za kubebea watumwa na kwenye mashamba yaliyokuwa yanalimwa na watumwa ya Waamerika, na walitambua kwamba kuwauza binadamu wenzao ni jambo ambalo halingethibitishwa kimaadili. Hata hivyo kanisa la Kikristo lilijitokeza na kutoa sababu nyingi likijitetea kuingia kwake katika biashara ya watumwa.
Wachungaji wengi walifanya biashara ya watumwa, hasa katika Angola, na wengine wengi walimiliki watumwa, katika nchi za Amerika. Sababu moja tu ambayo ilitolewa na kanisa Katoliki kuhusu vitendo vyake ilikuwa kwamba lilikuwa kinajaribu kuziokoa roho za Waafrika kwa kuwabatiza watumwa. Waprotestanti walikuwa wabaya zaidi, kwani wala hawakuweka wazi kwamba walikubali kwamba Waafrika walikuwa na roho.
Badala yake, walikubaliana na fikira kwamba mtumwa wa Kiafrika alikuwa sehemu ya rasilimali kama fenicha au hayawani wa kufugwa. Hakuna sehemu ya historia ya Kanisa la Kikristo ambayo inafedhehesha zaidi kuliko kusaidia “Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki.”
6
Kwa mujibu wa orodha ya Lloyd, iliamuliwa kwamba watumwa walikuwa ni bidhaa, na wenye thamani sana. Hati za bima zilizochukuliwa kutoka Lloyd waliwakatia watumwa hati za bima hadi kufika kiasi cha pauni za Kiingereza 45 kila mtumwa kiasi hicho cha fedha ni kikubwa katika kipindi hichi cha mwanzoni mwa karne ya 18 huko Uingereza.
Ili kuwazuia watumwa wasitoroke, au kuwaadhibu, nyenzo zisizo za kawaida kama zilivyoorodheshwa hapa zilitumiwa katika Afrika ya Magharibi na katika visiwa vya West Indies.
7
Siku zote kulikuwepo watu wachache ambao walipinga Biashara ya Utumwa katika Bahari ya Atlantiki. tangu mwanzo; lakini serikali mbalimbali na wafanya biashara hawakuwajali, wakati wa karne ya kumi na tano, kumi na sita na kumi na saba. Haikuwa hivyo, hadi mwishoni mwa karne ya kumi na nane wakati majaribio ya dhati yalifanywa kwa lengo la kukomesha biashara hii.
James Boswell, akijaribu kukana hoja za watu waliotaka biashara ya watumwa ikomeshwe, anaandika katika kitabu chake kiitwacho “Life of Johnson.” Kwamba: Jaribio la kinyama na la hatari ambalo kwa muda fulani limeendelea kuwepo kwa lengo la kupata sheria ya bunge letu, ili kukomesha tawi la maana sana na muhimu la faida kibiashara, lazima lingekwisha amuliwa mara moja, kama isin- gelikuwa kundi lisilo na maana la washabiki waliokuwa msitari wa mbele kwalo bila kufaulu, ndilo ambalo linaunda kundi kubwa la Wakulima, Wafanya biashara na wengineo ambao rasilimali yao imetumbukizwa na kuhusishwa kwenye biashara hiyo, kwa sababu zao kujikinaisha, hufikiria kwamba hapangekuwepo na hatari.
Ujasiri ambao jaribio hilo limepata msisimko mshangao wangu na hasira, na ingawa watu fulani wenye uwezo mkubwa wameliunga mkono, ama kwa sababu ya kutaka umaarufu wa muda mfupi, wakati wanao utajiri, au kupenda kujumuika kwenye fitina, wakati hawana kitu, maoni yangu hayatetereki.
Kukomesha hali ya kuwepo utumwa ambayo katika zama zote, MUNGU ameruhusu, na binadamu akaendeleza, haingekuwa unyang’anyi tu kwa tabaka la raia wetu wasio hesabika; lakini pia ingekuwa ukatili mno kwa Washenzi wa Kiafrika, ambao sehemu kutoka miongoni mwao inaokolewa kutoka kwenye mauaji ya kinyama, au kutoka kwenye utumwa isiyovumilika katika nchi yao wenyewe, na huwaingiza kwenye maisha ya hali ya furaha zaidi, hasa zaidi sasa kupita kwao kwenda katika visiwa vya West-Indies na wanavyotendewa huko katika hali ya udhibiti wa kibinadamu. Kukomesha biashara hiyo itakuwa sawa na kufunga milango ya huruma kwa binadamu.”
8Marekebisho ya takrima ya kibinadamu wanayofanyiwa na huruma, hujionyesha yenyewe kwenye maelezo ya kina na picha iliyoonyeshwa hapo juu!
- 1. Alpers, Edward A., East Africa Slave-Trade (Dar-es-Salaam: The Historical
Association of Tanzania, 1967)
- 2. Rodney, Walter., West African and the Atlantic slave-trade (Dar- es-Salaam: The
Historical Association of Tanzania, 1967)
- 3. Newsweek (March 15, 1965) uk. 106
- 4. Rodney, op. cit., uk.4-5
- 5. Ibid, uk. 7f.
- 6. Ibid uk.22.
- 7. Lloyd’s list, 250th Anniversary (1734-1984) April 17, 1984, London, uk. 149.
- 8. Boswell, J, Life of Johnson (N.Y. Modern Library Edition, 1965) Uk. 365