Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Udhalimu wa Utumwa Zanzibar na Pemba: Mababu zetu waliteswa, walihasiwa, walibakwa, na kuuawa kinyama

Hivi pamoja na uhuru wetu tumeona ukatili wa kiasi gani Nchi hii watu wakipigwa kwa marungu kisa maandamano tena ya amani kupigwa kwa marungu, mabomu hata kuuwawa kwa risasi na vipigo vibaya kabisa tena na askari wetu weusi kwa raia wasio na jiwe wala kisu! HAPA UNASEMAJE PASCO?
 
Jibu lako na ufafanuzi uliotoa inatosha kabisa kuonyesha Udhaifu wa Uzi huu na maneno yoote uloandika hapa.

Km wewe ni msomi huwezi kufanya hitimisho na kusema ( nakariri) "Ripoti hii ilipotoka wahusika walikuwepo, hakuna tafiti nyingine au chapisho lilitolewa kupiga ripoti hii, hivyo nachukulia yaliyosemwa humu yote ni kweli tupu, "!!

Leo Unatubebea Habari ya Mzungu Kisha unatuletea hapa na kutoa Hitimisho kuwa ni KWELI TUPU?

Elimu ni kitu muhimu Pasco. Hizo Copy and Paste zinafanyika kila mara lkn Kutoa HITIMISHO km Lako Ni Kuonyesha Udhaifu wako wa elimu na maono ya kawaida kabisa.

Wapi ktk Hii Historia UNAYOITA YA KWELI TUPU imeonyesha WAZUNGU WALIOBEBA BABU ZETU na Kwenda KUWAUZA HUKO LIVERPOOL na Virginia USA?
Unataka kunambia MZUNGU HAKUSHIRIKI KTK BIASHARA YA UTUMWA HUKO ZANZIBAR?

Watanzania wa namna Yako Mnatutukanisha kwa wasomaji wa nje Kuona maneno km haya ktk Public Forum ya namna hii!

Ni bora ukasema Hiki ndicho walichoandika WAZUNGU kuliko kusema NI KWELI TUPU.

we Ukisimamishwa Mahakamani UNAWEZA KUAPA Kwa kusema Historia Hii NI KWELI TUPU?

Au hujui maana ya "KWELI TUPU"?!
!
Mkuu Bill, kubishana kwa hoja ndio healthy ya mjadala wowote!, thanks for this!. Biashara ya watumwa Indian Ocean ilifanywa na Waarabu na sio wazungu. Wazungu wao walifanya Trans Atlantic Slave Trade, na baada ya kupigwa marufuku biashara hiyo, watumwa walikokuwa tayari kurudishwa Afrika, walirudishwa. Watumwa wa USA walirudishwa Liberia na wale wa UK wakapelekwa Siera Leone.

Watumwa waliopelekwa Arabuni na Bara Hindi, wote walihasiwa kwa ukatili wa genocide type hakuwepo mtumwa wa kumrejesha!. Wamiliki wa watumwa Zanzibar ambao ni Waarabu, waligoma kuwaachia watumwa wao, ndipo Kanisa la Uingereza wakatoa fedha kuwafidia wamiliki ndipo Mwarabu akawaachia huru watumwa, na soko likafungwa na kujengwa kanisa pale Mkunazini.

Mada hapa sio utumwa in general, taarrifa ni utumwa Pemba na Unguja!.

Andiko likiishakuwepo na halikukanushwa popote, then andiko hilo linasimama mahakama yoyote kama ushahidi halali na usio tia shaka yoyote kuwa yote yaliyoelezwa humu A report on slavery and the slave trade in Zanzibar, Pemba, ni kweli tupu!.

Inawezekana serikali ya dhalimu ya uvamizi ya Sultani, waliikanusha taarifa hiyo lakini kanusho hilo halikuchapishwa, hivyo hata kama utafiti huo ni uwongo, uwongo ukisemwa sana bila kukanushwa, hukeuka kuwa ndio ukweli wenyewe, hivi hapa tunapozungumza, kuhusiana na biashara ya utumwa Unguja na Pemba, dhalimu ni Mwarabu!.

Pasco
 
Kama hao waarab waliwapa mimba kisha kuwaua hao wamatumbi na kuzika mama na mtt hao machotara walitka wapi??au walishushw mbingun?
Soma tokea juu ameeleza vzr kuwa machotara walitokana na wanawake wa kiafrica kuzalishwa na wanaume wa kiarabu...endelea kusoma acha woga!
 
Mkuu Bill, kubishana kwa hoja ndio healthy ya mjadala wowote!, thanks for this!. Biashara ya watumwa Indian Ocean ilifanywa na Waarabu na sio wazungu. Wazungu wao walifanya Trans Atlantic Slave Trade, na baada ya kupigwa marufuku biashara hiyo, watumwa walikokuwa tayari kurudishwa Afrika, walirudishwa. Watumwa wa USA walirudishwa Liberia na wale wa UK wakapelekwa Siera Leone.

Watumwa waliopelekwa Arabuni na Bara Hindi, wote walihasiwa kwa ukatili wa genocide type hakuwepo mtumwa wa kumrejesha!. Wamiliki wa watumwa Zanzibar ambao ni Waarabu, waligoma kuwaachia watumwa wao, ndipo Kanisa la Uingereza wakatoa fedha kuwafidia wamiliki ndipo Mwarabu akawaachia huru watumwa, na soko likafungwa na kujengwa kanisa pale Mkunazini.

Mada hapa sio utumwa in general, taarrifa ni utumwa Pemba na Unguja!.

Andiko likiishakuwepo na halikukanushwa popote, then andiko hilo linasimama mahakama yoyote kama ushahidi halali na usio tia shaka yoyote kuwa yote yaliyoelezwa humu A report on slavery and the slave trade in Zanzibar, Pemba, ni kweli tupu!.

Inawezekana serikali ya dhalimu ya uvamizi ya Sultani, waliikanusha taarifa hiyo lakini kanusho hilo halikuchapishwa, hivyo hata kama utafiti huo ni uwongo, uwongo ukisemwa sana bila kukanushwa, hukeuka kuwa ndio ukweli wenyewe, hivi hapa tunapozungumza, kuhusiana na biashara ya utumwa Unguja na Pemba, dhalimu ni Mwarabu!.

Pasco
Narejea ktk maelezo yangu ya awali.
Na ningependa Unijibu km nilivyokuuliza. Historia ilioandikwa na Mzungu huyo huyo inasema KABLA YA 1807 legislation Ndani ya Miaka 300. wazungu walifanikiwa KUBEBA WATUMWA WA KIAFRIKA ZAIDI YA 12,000,000 kutoka Pwani ya East africa na Savannah area of Africa (which includes countries such as Mali, Niger, Chad and Sudan) and the Horn of Africa (which covers Djibouti, Somalia and Ethiopia).

Sasa Swali ni kwamba! Je MZUNGU Hapa HAKUHUSIKA HATTA KIDOGO ktk BIASHARA HII ya WATUMWA WA Huko EAST AFRICA Including ZANZIBAR?

Nadhani wewe ni Mswahili km mimi ktk matumizi ya Lugha. Na neno "KUHUSIKA" nina imani maana yake unaijua.
Ntakupa mfano hai hapa.

During the second half of the 18th century, France opened up larger sugar plantations on the islands of Reunion, Mauritius and in the Indian Ocean. na Hapa WAFANYAKAZI WOTE Walikuwa WATUMWA WA KIAFRIKA.

Mfano wa Pili.

Je! Umeshawahi Kumsoma Napoleon 1 of France ktk Mswada wa Sheria alioupitisha Mwaka 1802 kuhusu UHALALI WA WATUMWA?
Baada ya Hapo NINI KILIWATOKEA WAZEE WETU wa EAST AFRICA?

Sasa Naomba Jibu lenye USHAHIDI na udadavuzi ulio wazi. Sio Jibu la Mitaani.
 
Wengi wetu hatufahamu uhusiano kati ya Oman na Zanzibar/Mombasa/Kilwa Na Pwani hii ya Mashariki..wengi tunafundishwa kuwa Wa Oman walikuja kutawala Znz Na pwani yake....Tukumbuke Wa Oman walifika Znz kitambo kwa biashara na Makaazi ya kawaida. Zile Pepo za bahari ziitwazo Moonson zilianza hata kabla ya Yesu...visiwa hivyi na pwani hii ilikua tayari imeshavuka na kufikia dunia nyengine.

Tusome Makala hii ambayo ni nadra kwa vijana wa leo kusomeshwa mashuleni na tumekua wavivu wa kusoma na kufanya tafiti za maana . Tumekua tukiamini kama Pasco anavo amini propaganda za kisonge kuhusu kufagia kwa matiti...

tuone vipi wa Oman walifika mashariki na kuhamia Znz nz Mombasa..namna gani walisaidia kuondoa ukoloni wa kireno walotawala Znz kwa miaka 200. Wareno walifanya ushenzi na hujuma kubwa na mateso lakini haya husomeshwi shule ..kwani tume chaguliwa ya kufundishwa ..

Lakini moja walo liacha Pemba ni Mchezo kufukuzana Na Ngombe !

Uvamizi Zanzibar Msumbiji na kilwa mombasa na Mogadishu na Wareno
Wareno waliivamia Oman na Zanzibar katika karne ya kumi na sita 16.

lakini baadaye wa Omani walifanikiwa kujikomboa kutoka kwa wareno Ukombozi wa Omani ndio ulioleta tija ya kukombolewa kwa zanzibar, kwani ni wa Oman hawa hawa ndio walioikomboa zanzibar Oman ilivamiwa mwaka 1508.
Chini ya Aifonso Albuqueque ambaye aliishambulia Sohar, Maskat, na karyat na kuziweka chini ya Himaya yake wakati Zanzibar Unguja ,ilivamiwa mwaka 1503. chini ya Lawrenco Ravasco na baadaye ilishambuliwa pemba na Francisco da Seixas De'Cabrera.kama ilivyokuwa Kilwa ilivamiwa Fransisco De Almeida akishiriana na vasco Da Gama Mwaka 1505,)
kushambuliwa Unguja kuanzia mwaka 1503 Unguja ilishambuliwa Miezi Miwili Mfululizo na Wareno chini ya Laurenso ravasco hata ilipofika mwaka 1508, Don Duarte Delemos, Gavana Wa Kireno Nchini Ethiopia Alifika Unguja ili kukusanya Kodi, akakataliwa

watu wa Unguja wakapambana Kiume wakishirikiana na wenzao kutoka visiwavywa Pemba na katika mwaka 1631 Francisco de sexas Cabreira alipiga Bomu kasri ya Malkia Mwana wa Mwana na kuifukia kama ilivyopigwa bomu Kiilwa na bagamoyo.

Malkia Mwana wa Mwana alikimbilia na kuhamia Yenen na hakufanikiwa kurudi tena Mpaka Umauti ulipomfika akiwa Jiddah Saud Arabia Mwaka 1638.)

Kasri yake wakaivamia Wareno na kuifanya kuwa kanisa dogo la mwanzo, lakini baadaye kanisa hilo lilivunjwa na I mamu Seif wa Oman alipokuja kuikomboa Zanzibar ' ngome kongwe ndio ilokuwa ikulu ya Malkia Mwana wa mwana hapo zamani ,

katika Unguja baada ya tukio hilo watu wengi sana walikimbilia Oman ili kwenda kujipanga vizuri na kufundishwa mbinu na kupambana na mreno, mwaka 1632 Yusuf bin hassan bin Ahmed kutoka pemba aliishambulia ngome ya Wareno Mombasa,

kushambuliwa pemba kwamara ya mwanzo,kwa mujibu wa waraka wa Jamba Ngome ulioandikwa mwaka 1606 na Mmoja kati ya wazee wa pemba chini ya usimamizi maelekezo wa Sharif bin yusuf bin burhan

waraka huo ulikutwa katikati ya Msahafu (Qur an) na Shekh Theniya bin Khalfan ambaye aliupiga Copy nakala kisha ukatafsiriwa kwa kiingereza na Shekh Abdur rahman bin muhammad bin Jidawy wa kahkama kuu ya Zanzibar na kuhifadhiwa katika makumbusho ya taifa ya beitul Aman. waraka huo unasema hivi,
Baada ya Francico De sexas Cbreira kuivamia Pemba akiwa na kisoni bin jojo ambaye aliingia pemba na meli tano na wanavita wa msalaba wa kireno kutaka kulipwa kodi.

wenyeji wa pemba walikusanyika pamoja na maalimu Juma bin ko
mbo na kiongozi wa pemba akasema tazama hapa wewe kisoni hatutakupa chochote,hatukujui wewe ni nani? sisi sio watumwa wako, kwanza wewe ni nani?

kwa sababu hii kisoni akatangaza Vita lakini wenyeji wa pemba wakapambana kwa muda wa siku 32 kisoni akashindwa kwa mshikamano huo akakimbia na kuondoka katika mwaka 1652, kisoni alirudi tena na meli 65 za wana vita kudai kodi kutoka kwa wenyeji wa pemba lakini walikataa kata kata na walipigana kwa muda wa siku 60, waliua Wareno 1304 na wenyeji 364 walikufa mashahidi, Kisoni hakupata kitu akarudi na watu wake,'
katika mwaka 1656. Kisoni alikuja na Meli 70 za kijeshi zikatua Ras-Mkumbuu zikajipanga kwa mapambano ya siku saba wenyeji wa pemba walijikusanya kutoka kona zote za pemba,ilikuwa ni maadalizi ya kujitolea muhanga zidi ya wareno kufa kupona,

wakati kisoni alipotaka kodi majlis Shura iliyowajumuisha maalimu juma kombo Shsme bin ali, Mfalme haruna bin hassan bin ali na Mwinyi bin Sharif bin Qutb bin mahaz Al Baalawy ,

maalim juma kombo alimwambia Kisoni tumekubaliana kwamba hatukulipi kodi yoyote Kisoni akasema Mkubali msikubali Mtalipa kodi kama kawaida maalim akasema hatuogopi sieee'...
Waraka unaendelea kusema kuwa mwisho walikubaliana kiujanja kuwa watalipa Dirham 12000 na baadaye wataongeza Dirham 16000, lakini zitaanza kulipwa mwaka utakaofuatia

waraka huo unabaini kuwa walifanya hivyo ili bwana kisoni aondoke wapate kujipanga zaidi kwa mapambano, na alipoondoka walisoma Ahlal badri kumuomba mwenyezi mungu kwa tawasul ya watu waliopigana vita vya badr ndani ya wakati mgumu wa mwezi wa Ramadhan...pamoja na nyiradi mbanimbali

husemwa kuwa hiyo ndio dua iliyoombwa kuwa asipatikane Mzanzibar yeyote kuritadi kutoka katika Uislamu ikiwa ataritadi apatwe na madhara na hii imetokezea mara nyingi katika vizazi vya zanzibar,
Mwisho ilishambuliwa pemba na wareno kutamalaki Hollings Worth anahitimisha kwa kusema
hakuna shaka yeyote wala ubishi kkkkwamba wareno walikuwa na hamu kubwa ya ajabu kuhakikisha kuwa wanausambaratisha Utawala wa kiislamu na Ustaarabu wake katika kisiwa cha pemba

na katika Mwaka 1651 Oman ikiongozwa na imamu nasir bin murshid al yaaroud ambapo alifanikiwa kuukomboa Mji wa ormuz mwaka 1622 na Mwanawe imam seif ibm nasir ibn murshid alyaarod alifakiwa kuwatowa kabisa wareno katika mwaka 1631/
Lakini zanzibar ilikaa chini ya Utawala wa kireno tena mpaka mwaka 1696 baada ya kushindwa kwa majaribio mengi ya kutaka kujikomboa, yaani mwaka 1585 waliposaidiwa tena na Utawala wa Uturuki Ottoman Empire/ na kupitia kwa Shambulizi kubwa alilofanya yusuf Ahmed mwaka 1630 ambalo halikuzaa matunda/
Lakini ilipokombolewa Oman mwaka 1632 ndio Chachu ya kukombolewa kwa Zanzibar kwani machifu wa kizanzibar kutoka tumbatu na peeemba wakishirikiana na watu wa Kilwa

waliteua wajumbe kwenda Oman jahazi lilichogwa chwaka Uguja nakwenda kukutana Imam seif ili afanye Ukombozi wa kuwasaiidia zanzibar nae alikubali pale alipokusanya majeshi na kutangaza vita dhidi ya mreno kuanzia mwaka 1696-1698 alipofanikiwa kuikamata Ngome kuu ya mombasa

wakati huo zanzibar katika kasr ya Fatma na Mwinyi Mkuu tayari wareno walishajenga kanisa digo ndani ya ngome kogwe , unaweza kuyaona makombora aliyotumia Imam seif kumtowa mreno yamewekwa mbele ya ndome hiyo kogwe na sasa mengine mbele wa forodhani ikiwa kama kumbukumbu ya tukui hilo,

baada ya kumaliza kuikomboa Zanzibar Imamu seif bin murshid alikuwa tayari kuyarejesha majeshi yake nyumbani kwake oman kama walivyofanya waturuki Ottoman Empire mwaka 1585. lakini Wazanzibar walijikushanya nakuweka shura ya kukubaliana kwamba majesshi ya oman yasirudi kwanza

hivyo kwa kuhofia kwamba wareno watarudi kama walivyorudi mwaka 1586 baada ya waturuki Ottoman empire''walivyorudi kwao, walimsihi imamu sei ayabakishe majeshi yake hapo na washirikiane katika Uamuzi wa zanzibar hivyo basi imamu seif alikubali tena maombi ya ndugu zake katika iman akabakisha majeshi yake hapo, bali akiwa oman aliteua magavana mbali mbali wenye kufanya kazi katika mwambao wa Africa mashariki kupitia Zanzibar na pia wapo Wazanzibar waliteuliwa kwenda kufanya kazi oman chini ya mashirikiano hayo,.

kadhalika alianza kuitumikia zanzibar kwa misaada kuendeleza kilimo bora cha minazi ni yeye ndio aliyeanzisha ukarabati wa njia na kuttawenya visima vywa maji safi na kufanya rutuba iliyowezesha zao la minazi na miti mingine
imamu seif alifariki mwaka 1711, akateuliwa imam seif II kushika Uimamu, lakini naye alifariki mwaka 1728)
akaja Inan said ibn Ahmed ibn ssultan ibn said al Busaid
(sayyid said)
Uchaguzi wa mwaka 1741ulimuweka madarakani imam Ahmed bin said bin sultan al busaid Ambaye naye alishika Uimamu yeye alibadili mfumo wa Utawala na kuwateua magavana (maliwali) wapya na huko mombasa ambayo ilikuwa chini ya uliwali wa Mazrui na huko pate walikuwa ma- al harth

katika mwaka 1746 imam Ahmed alimteua Addullah bin Djad kuwa Liwali Mpya wa Zanzibar, na mombasa na pate,ndipo mazrui wa mambasa na ma-al harth wa pate walipokataa na kujitangazia utawala wao (mombasa Sheikhdom)
katika mwaka 184 sayyd said alikamata madaraka ya Oman na Zanzibar kwa taratibu za kisheria kwa mujibu wa dhehebu lake la ibadhi ni yeye aliyefanikiwa kuumaliza mzozo wa mombasa na pate lakini baadaye mwaka 1826 aliwapa tena indhar
wakati yote yanatendeka mwinyi mkuu wa zanzibar Hassan ambaye ndio Mtawala wa kienyeji aliyewakaribisha wa- Oman zanzibar akimsihi sana sayyid said bora ahamishe makao makuu kuyatoa Oman aje kuishi zanzibar ili ijengeke kama makao makuu au mji mkuu sayyid said hakufanya khiyana aliitikia wito wa nduguye katika iman hatimaye mwaka 1833 alianza kuikarabati Ngome kongwe na 1840 kuhamia ambapo mwanzo aliitumia Mwinyi Mkuu mara baada ya kuondoka wareno
john middleton na jane Campbell wanalezea vizuri tukio hilo la kiungwana kinyume na wale wanaosema sayyid said amekuja kuteka nchi ya zanzibar
sayyid said bin sultan hakuwa ni mwenye kuteka lakini kuitikia wito wa ndugu zake wa iman
Ndio hapo ukaimbwa wimbo wa kibuzi buzi, kuwa ni fumbo la kuimbwa na watoto kueleza
(Njama za kwenda manga omaaan uitwae fumo mkuki na Upanga huku sinba mreno karegea karegea kongwe Mzee hajiwezi)''
mwinyi Mkuu akajenga dunga bweni na kuhamia huko ili kumpisha sayyid said.
mwinyyi mkuu wa zanzibar hassan bin sultan bin Alawy Mtoto wa Mwinyi Mkuu wa kwanza kuhamia hapa Unguja alikuwa Mfalme mwwwaka 1710... na mwinyi mkuu hassan bin Ahmed ndie wa kwanza kuhamia Dunga, kaskazini ya dunga Bweni akimpisha Sayyid said bin sultan mjini,.
kwani fahari wawili hawakai zizi moja ingawa akija sana Mjini kumtembelea na wakisikilizana na akipendwa sana na wananchi mpaka Nyimbo ya kkumbembelezea Mtoto ikimbwa kwa jina lake
karatasi nakupeleka
kwa Mfalme Hassani
na fimbo ya Henzirani,
makosa niliyokosa
nina muombeazi kweani,
Mwombezi wangu nyota
na baraka ramadhani...'''
Lakini pia viongozi hawa walikuwa ni viongo muhimu katika baraza la mawaziri wa sayyid said

Tuwashukuru wa Oman kwa kuwatoa Wareno..

askari wa Malkia baada ya vita ya saa dakika 38.....

znz08.jpg
 
Pasco hiv ndiyo kusema kwamba umekimbia umandee au?

Kwanza kabisa nikupe elimu ya kwamba miongon mwa agents of colonialism kulikuwa na Traders..Explorers and Missionaries...waarabu hawapo katika vitanguliz vya ukoloni...

Mzungu alipokuja huku kufanya ukolon tayar alishamkuta mwarabu akifanya mambo meengi ma waafrika...na kadhalika

Pia waarabu siyo waislam...wapo waarabu weengi vile vile ambao si waislam believe me hata christians wapo ambao ni arabs...

Uislam as a religion unakataza utumwa in the first place katika mafundisho yake...infact ni uislam huo huo kwa huko uarabun uliokuja kupiga marufuku biashara ya utumwa kupitia mafunzo ya qur an na sunnah za mtume wetu Muhammad rehma na aman ziwe juu yake...

Kwaiyo kama kuna vitu hujui...uwe unauliza kwanza kuliko kujivua nguo

Ni kweli unachosema lakini uko nje ya mada. Hatuzungumzii historia ya ukoloni au ya dini ya Kiislamu. Kinachojadiliwa hapa ni uhusika wa waarabu katik biashara mbovu kabisa ya utumwa wa mwafrika. Tiririka katika hili au anzisha mada na wewe kwa mfano unaweza kuiita 'Mchango wa Uislamu katika kukomesha biashara ya utumwa, Au Uhusiano baina ya umishonari na kushamiri kwa ukoloni Africa n.k
 
Mkuu The big empty show, mara nyingi huwa sikujibu, sio kwa sababu sina majibu, bali kutokana na nyingi ya hoja zako kuwa ni debe tupu!, hupiga kelele!.

Aliyekimbia umande ni yule anayeleta habari za colonialism kwenye hoja za slavery!. Sometimes mtu unaweza kujikuta umeficha upumbavu wako kwa kukaa kimya!, kuna mijitu mijinga ajabu, ambapo ikitulia kimya huwezi kuijua, ila ni pale inapofungua mabakuli yake!.

Pasco

Sasa Pasco...!

Jazba za nin Mkuu?

Kwaiyo wewe unataka kusema Slavery na Colonialism hazina nasaba?

After Scramble and partition of African Continent huko berlin ni kwamba kusema hujui nin kilifuatia?..

Hujui ni kina nan walihusika katika kuwabeba wazee wetu na kuwapeleka North America..Brazil..Carribean islands na kwingineko kama watumwa?

Hivyo wewe ndie wajiita ni mwandish wa habari?teh teh teh...

Sasa unaandikaga nin huko..au utakuwa ni mhariri wa lile gazeti la Udaku la Dira wewe siyo bure...!

Jitu la hovyo kbs yaani wewe unawezaje kusimama na kuwatukuza wazungu pamoja na yoote mabaya waliyokufanyia bado unasimama na kuwatukuza?
 
Jibu lako na ufafanuzi uliotoa inatosha kabisa kuonyesha Udhaifu wa Uzi huu na maneno yoote uloandika hapa.

Km wewe ni msomi huwezi kufanya hitimisho na kusema ( nakariri) "Ripoti hii ilipotoka wahusika walikuwepo, hakuna tafiti nyingine au chapisho lilitolewa kupiga ripoti hii, hivyo nachukulia yaliyosemwa humu yote ni kweli tupu, "!!

Vipi utoe hitimisho km hili kwa Kusoma habari ya Muingereza amabe aliendesha Biashara hio hio ya UTUMWA Zaidi ya miaka 300? (Refer to Trans Atlantic Slave Trade ikiongozwa na Captain John Hawkins who made the first known English slaving voyage to Africa, in 1562, in the reign of Elizabeth 1.
Na huyu Hawkins made three such journeys over a period of six years. He captured over 1200 Africans and sold them as goods in the Spanish colonies in the Americas. na huu ndio uliokuwa Mlango mkuu kwa Waingereza Kuendeleza Biashara hii kwa miaka mingine 300 mbele.

Hii habari Sikuandika mimi Bali ni HAO HAO WAINGEREZA.

Leo Unatubebea Habari ya Mzungu Kisha unatuletea hapa na kutoa Hitimisho kuwa ni KWELI TUPU?

Elimu ni kitu muhimu Pasco. Hizo Copy and Paste zinafanyika kila mara lkn Kutoa HITIMISHO km Lako Ni Kuonyesha Udhaifu wako wa elimu na maono ya kawaida kabisa.

Wapi ktk Hii Historia UNAYOITA YA KWELI TUPU imeonyesha WAZUNGU WALIOBEBA BABU ZETU na Kwenda KUWAUZA HUKO LIVERPOOL na Virginia USA?
Unataka kunambia MZUNGU HAKUSHIRIKI KTK BIASHARA YA UTUMWA HUKO ZANZIBAR?

Watanzania wa namna Yako Mnatutukanisha kwa wasomaji wa nje Kuona maneno km haya ktk Public Forum ya namna hii!

Ni bora ukasema Hiki ndicho walichoandika WAZUNGU kuliko kusema NI KWELI TUPU.

we Ukisimamishwa Mahakamani UNAWEZA KUAPA Kwa kusema Historia Hii NI KWELI TUPU?

Au hujui maana ya "KWELI TUPU"?!!

Kwani kuhusika kwa wazungu kunaondoa kuhusika kwa waarabu? Kwani kunukuu andishi na kuweka msimamo wako kuhusu kuamini au kutoamini andishi hilo ni kosa? Usomi ni nini? Hivi hii historia unaweka ya Captain John Hawkins hujaisoma mahali wewe? Kwa nini na wewe unaiweka humu ili tuiamini lakini unaona ni kosa mwenzio kunukuu utafiti?

Hebu njooni na hoja za maana kuhusiana na kuhusika au kutohusika kwa WAARABU katika kile kinachoitwa East African Slave Trade.
 
Sasa Pasco...!

Jazba za nin Mkuu?

Kwaiyo wewe unataka kusema Slavery na Colonialism hazina nasaba?

After Scramble and partition of African Continent huko berlin ni kwamba kusema hujui nin kilifuatia?..

Hujui ni kina nan walihusika katika kuwabeba wazee wetu na kuwapeleka North America..Brazil..Carribean islands na kwingineko kama watumwa?

Hivyo wewe ndie wajiita ni mwandish wa habari?teh teh teh...

Sasa unaandikaga nin huko..au utakuwa ni mhariri wa lile gazeti la Udaku la Dira wewe siyo bure...!

Jitu la hovyo kbs yaani wewe unawezaje kusimama na kuwatukuza wazungu pamoja na yoote mabaya waliyokufanyia bado unasimama na kuwatukuza?

Duh, mkuu Big Show, usiingie kichwakichwa kwenye hii mada, Pasco amekupa ushauri wa bure, usipuuze la sivyo unaenda kuumbuka muda si mrefu. Kwa mfano unataka kuhusisha scramble and partition of Africa huko Berlin na biashara ya utumwa ya Trans -Atlantic Slave Trade? Utachekesha ishia hapohapo au njoo na hoja nyingine
 
Transatlantic slave trade ni jambo moja..berlin conference ni jambo jingine ila yoote yanahusika katika underdevelopment of african continent today...

Hoja ambayo Pasco mimi nilikua namueleza ni kwamba hawez kusimama katika kuliaddress suala la utumwa kwa kutumia hoja za waarabu huku akiwaacha pemben hao wazungu ambao wamewafanya wazee wetu kwa miaka mingi...

Nilikua namuambia hapo kuwa. Agents wa kuwafanya wazee wetu watumwa walikuwamo wamissionary pia...na baada ya kugawanywa kwa bara hili ni hawa hawa wazungu waliwabeba wazee wetu na kuwapeleka america na sehem zingine huko kama labour force sasa mimi nichekeshe kwa lipi na hilo jambo liko wazi tuh?
 
Mkuu mjukuu wa Baraghashia, Pasco sio kipofu wala makengeza, bali katika biashara ya utumwa kuna hatua mbalimbali na zote zina udhalimu wake ikiwemo ukamataji. Kwenye bandiko langu nimeeleza hivi kuhusu ukamataji. " Kwenye biashara ya utumwa, waliokuwa wakikamata watumwa, sio Waarabu, Waarabu wao walikuwa ni wafanyabiashara ya watumwa kwenye soko kuu la watumwa la Zanzibar, wakitokea Bagamoyo, na wanunuzi wakuu wa watumwa toka soko la Zanzibar kwa ajili ya kuwasafirisha kuwauza Uaabuni na India, ambako kote huko baada ya kufika, watumwa wanaume walihasiwa!. Waarabu pia ndio walikuwa wamiliki wa watumwa katika mashamba ya Zanzibar na`Pemba, ambapo nako watumwa wanaume walihasiwa, wanawake walifanywa vijakazi na ndio wazazi wa machotara wa Zanzibar na Pemba, wengi ni baba Mwarabu, mama uzao wa watumwa wanawake wenye bahati, ambao hawakutumbuliwa mimba za Waarabu!.

Upatikanaji wa watumwa kutoka bara pia ulihusisha baadhi ya watawala wakiwemo machifu ambapo baadhi ya wahalifu waliostahili adhabu za vifo katika jamii zao, badala ya kuuliwa na kuwa hasara jumla, waliuzwa, utumwani, lakini watumwa wengi ni watu tuu wa kawaida wasio na hatia yoyote ambao walivamiwa na kukamatwa kwa nguvu, wakiwemo wanawake na watoto!. Zoezi la ukamataji watumwa pia lilihusisha vitendo vya ukatili, ambapo wengi watumwa hawa, waliuawawa katika purukushani, na wengine wengi walifia njiani na miili yao kuachwa ikioza, miili yenye bahati ilifanywa vitoweo vya wanyama wa porini. Kwenye misafara hiyo, ndugu zetu waliteswa sana mateso ambayo hayazungumziki walioishiwa nguvu, walipigwa hadi kifo ila hakukuwepo na kamera ya mzungu wa kutupigia picha kuja kutuleta humu!."

Mfanyabiashaa mkuu wa Watumwa, Tipu Tipu, hakuwa Mnyamwezi bali ni chotara wa Kiarabu baba yake ni Mwarabu na mama yake ni mjakazi, jina lake halisi ni Hamad bin Muḥammad bin Jum'ah bin Rajab bin Muḥammad bin Sa‘īd al-Murjabī, hivyo kama kawaida ya wajakazi wote, mama yake alibakwa!, ila baada ya kubakwa sio unajua tena mambo ya wanawake wa Kinyamwezi!, hivyo baba akampenda mjakazi huyo!, ndipo Tipu Tipu akazaliwa!. Na asili ya kuitwa tipu tipu ni milio ya risasi za bunduki ya tipu tipu, ile tip, tip, watu walisikia kwanza milio ya risasi ndipo wakamuona tipu tip mwenyewe!.

Utmwa nao umekuwa na udhalimu wa aina nyingi, ili kubwa kuliko yote ni kitendo cha madhalimu hawa Waarabu kuwa hasi babu zetu, na kuwaingilia kinguvu bibi zetu!. Kati ya ukatili wote aliofanyiwa binadamu, ukatili huu wa kuhasi ndio ukatili mkubwa zaidi kuliko hata kifo!. Afadhali wangewaua tuu tujue moja, lakini kitendo cha kuwa hasi ni genocide!. Watumwa waliochukuliwa na wazungu pia walifanyiwa ukatili wa hali ya juu lakini sio kama huu wa Waarabu!.

Ni kweli kulikuwa na utumwa katika jamii zote, na watumwa walifanyiwa vitendo vya kikatili, lakini mada yangu iliyoko mezani, inatokana na taarifa hii ya utafiti, A report on slavery and the slave trade in Zanzibar, Pemba, sasa kama na nyinyi wengine mnazo taarifa za utafiti wa ukatili wa jamii nyingine, leteni taarifa hizo humu, zianzishieni threads, tuzijadili!.

Pasco
PASCO
Baraghashia ni kofia na Baraghash ni jina.

Nimekubali kuwa PASCO si kipofu lakini ana makengeza yasiorekebishika. Anauona ukweli kwenye pembe ya mra ba uliopinda. Haduthi ulioiandika hapo juu haitafauyani na Alfu- leila ulela

Mjakazi wakati ule alijuulikana kama suria, na si MTUMWA. Baba yake TipTip alikuwa Gavana wa Sultan wa Zanzibar kule Tabora. Baba yake huyu alioa katika ukoo wa chifu Fundikira ( si mama wa TipTip) na kuishi nae uhai wake wote.

TipTip ni mfanya biashara ambae alikuwa anachukua pesa kutoka matajiri wa kiarabu na wakihindi kuja kuwa nunulia watumwa na meno ya tembo. Tiptip alikuwa anachukuwa wapagazi wa kinmyamwezi kumbebea meno ya tembo kwa ujira na watummwa hawakutumika kwa kazi hiyo kwa vile walitakiwa wafike Zanzibar kamili na afya bora ili wapate soko na kwa mauzo na bei ya juu. Wakati mwengine Tiptip ilibidi aiaharishe safari ya kurudi pwani mpaka msimu wa mavuno umalizike kwa vile inakuwa si rahisi kupata wapagazi wa kinyamwezi kubeba meno ya tembo mpaka Bagamoyo. Hapa ndipo ulipopatikana ule usemi maarufu wa " mzigo mzito mpeni mnyamwrzi"

Pasco elewa kwamba Mnyamwezi sawa na mzanzibari hawajawahi kufanywa watumwa. Tabora ilikuwani sehemu ya himaya (Mamlaka) ya Sultan wa Zanzibar. Wanyamwezi tokea karne hizo wanaingia Zanzibar na kabila lake ndio paspoti yake. Mpka hii leo kabila linalokubalika kutoka Zanzibar kutoka bara ni wanyamwezi tu.

Mateso na madhila waliopata watumwa ni wakati wa ukamataji na huo ulikuwa wanafanyiana watanganyika kwa watanganyika. Ukiangalia michoro yako ho juu watumwa wote walikuwa wamevishwa nguo za kujistiri mwili. Nani aliwapa nguo zile wakati huo bara walikuwa hawavai nguo na walikuwa wanakamatana uchi na vigozi au ukindu kiunoni tu.

PASCO ukibahatika kuja Zanzibar pitia museum na kusoma kitabu alichoandika mwenywe umelewe Tippu tip na utumwa. Tatizo utakalolipata na kiswahili kilichotumika, nia cha kale na fasaha na tofauti kabisa na kiswahili hiki cha kitanganyika tunachowasiliana. Ima kitafute kitabu kinachoitwa "TIPPU TIP The story of his career in Zanzibar & Central Africa"
 
Kwani kuhusika kwa wazungu kunaondoa kuhusika kwa waarabu? Kwani kunukuu andishi na kuweka msimamo wako kuhusu kuamini au kutoamini andishi hilo ni kosa? Usomi ni nini? Hivi hii historia unaweka ya Captain John Hawkins hujaisoma mahali wewe? Kwa nini na wewe unaiweka humu ili tuiamini lakini unaona ni kosa mwenzio kunukuu utafiti?

Hebu njooni na hoja za maana kuhusiana na kuhusika au kutohusika kwa WAARABU katika kile kinachoitwa East African Slave Trade.
Sasa na wewe ndo umeandika nini teba hapa?
Sio lzm kila uzi uchangie mkuu. Unaweza kujiabisha namna hii.

Wapi nimesema au kuandika kuwa HAIFAI kuleta habari Ulizosoma hapa? Au kiswahili kinakupa tabu km Pasco.!

Nisome Vizuri kijana.
 
[QUOTE ="Bill Cosby, post: 15962964, member: 168096"]Sasa na wewe ndo umeandika nini teba hapa?
Sio lzm kila uzi uchangie mkuu. Unaweza kujiabisha namna hii.

Wapi nimesema au kuandika kuwa HAIFAI kuleta habari Ulizosoma hapa? Au kiswahili kinakupa tabu km Pasco.!

Nisome Vizuri kijana.

Usijisahaulishe. Hebu rudia kusoma ulichokiandika katika post #265 unamaanisha nini kama sio kukosoa wenzio kunukuu walichosoma na kuchukua msimamo kulinganana uelewa wako[/QUOTE]
Hakuna sehemu nimesema ni kosa kuandika Unachokisoma. Makosa ni pale mtu anapokuja kudai kwamba kile alichokisoma NI KWELI TUPU! Km alivyodai huyo Pasco.

Vipi mtu asome stori ilioandikwa NA MZUNGU ambae alishiriki ktk BIASHARA YA UTUMWA kuhusu uovu wa Waarabu? Halafu msukuma wa Huko Shinyanga Aje kidai Historia Hio ni KWELI TUPU?
Uchache wa Elimu ni shida kubwa sana kwa wengi wenu. Lkn hamtambua kuwa hamjui!
 
PASCO
Baraghashia ni kofia na Baraghash ni jina.

Nimekubali kuwa PASCO si kipofu lakini ana makengeza yasiorekebishika. Anauona ukweli kwenye pembe ya mra ba uliopinda. Haduthi ulioiandika hapo juu haitafauyani na Alfu- leila ulela

Mjakazi wakati ule alijuulikana kama suria, na si MTUMWA. Baba yake TipTip alikuwa Gavana wa Sultan wa Zanzibar kule Tabora. Baba yake huyu alioa katika ukoo wa chifu Fundikira ( si mama wa TipTip) na kuishi nae uhai wake wote.

TipTip ni mfanya biashara ambae alikuwa anachukua pesa kutoka matajiri wa kiarabu na wakihindi kuja kuwa nunulia watumwa na meno ya tembo. Tiptip alikuwa anachukuwa wapagazi wa kinmyamwezi kumbebea meno ya tembo kwa ujira na watummwa hawakutumika kwa kazi hiyo kwa vile walitakiwa wafike Zanzibar kamili na afya bora ili wapate soko na kwa mauzo na bei ya juu. Wakati mwengine Tiptip ilibidi aiaharishe safari ya kurudi pwani mpaka msimu wa mavuno umalizike kwa vile inakuwa si rahisi kupata wapagazi wa kinyamwezi kubeba meno ya tembo mpaka Bagamoyo. Hapa ndipo ulipopatikana ule usemi maarufu wa " mzigo mzito mpeni mnyamwrzi"

Pasco elewa kwamba Mnyamwezi sawa na mzanzibari hawajawahi kufanywa watumwa. Tabora ilikuwani sehemu ya himaya (Mamlaka) ya Sultan wa Zanzibar. Wanyamwezi tokea karne hizo wanaingia Zanzibar na kabila lake ndio paspoti yake. Mpka hii leo kabila linalokubalika kutoka Zanzibar kutoka bara ni wanyamwezi tu.

Mateso na madhila waliopata watumwa ni wakati wa ukamataji na huo ulikuwa wanafanyiana watanganyika kwa watanganyika. Ukiangalia michoro yako ho juu watumwa wote walikuwa wamevishwa nguo za kujistiri mwili. Nani aliwapa nguo zile wakati huo bara walikuwa hawavai nguo na walikuwa wanakamatana uchi na vigozi au ukindu kiunoni tu.

PASCO ukibahatika kuja Zanzibar pitia museum na kusoma kitabu alichoandika mwenywe umelewe Tippu tip na utumwa. Tatizo utakalolipata na kiswahili kilichotumika, nia cha kale na fasaha na tofauti kabisa na kiswahili hiki cha kitanganyika tunachowasiliana. Ima kitafute kitabu kinachoitwa "TIPPU TIP The story of his career in Zanzibar & Central Africa"
Pasco na Wanamajlis,
Nakuombeni mchukue muda kusikiliza hii audio.

Naamini yapo mambo tunaweza kujifunza kuhusu
historia ya utumwa:
Mohamed Said: MASULTANI WALIPATAPO KUUA ZANZIBAR?

DSCN0218.JPG
 
Wanabodi,

Lakini pamoja na mazuri haya, sio vibaya kama wasiofuatilia historia, wakayajua madhila yaliyowakuta ndugu zetu Wamatumbi, wakati wa utawala dhalimu wa Sultani, kwenye visiwa vya Unguja na Pemba.
.

Sorry but the whole post is pile of garbage. Someone with his right mind will never copy and paste another person work or research. Most research were done in biased.
Kwa Kiswahili mabaya waliyo yafanya wazungu wa Magharibu hutoyasoma hadharani.
Africa ilitawaliwa kinguvu na Wazungu, waArabu walikuja kama kibiashara. Yes Utumwa waliufanya.
Lakini usisahau, Bible ilitangulia mwanzo 6000yrs before Islam. Na Bible imeeleza utumwa na maauji mengi yaliyofanywa na mitume iliyopita.
In FACT, utumwa ulikuwepo even before the Jesus was born. Utumwa ulikuwepo wakati wa Roman Empire to Vikings.

Naomba uandike maisha kabla ya mapinduzi 1964.
Shida gani zilikuwepo? Madawa hospitalini, Kazi, MAISHA kwa wananchi, Elimu?
Mapinduzi yamefanywa, je Zanzibar imegain kitu gani?
As far as I am concern ZANZIBAR IS DEAD country. Ni mkoa katika Tanzania.
Hakuna maendeleo hata katika jambo moja. Watoto wanamaliza school hawajui hata kiswahili wacha kingereza.
Mahospitali hakuna dawa, Barabara mbovu, Mitaro yote inavuja maji machafu. Kunanuka.
Yapi ni matunda ya Mapinduzi????
 
Sasa Pasco...!

Jazba za nin Mkuu?

Kwaiyo wewe unataka kusema Slavery na Colonialism hazina nasaba?

After Scramble and partition of African Continent huko berlin ni kwamba kusema hujui nin kilifuatia?..

Hujui ni kina nan walihusika katika kuwabeba wazee wetu na kuwapeleka North America..Brazil..Carribean islands na kwingineko kama watumwa?

Hivyo wewe ndie wajiita ni mwandish wa habari?teh teh teh...

Sasa unaandikaga nin huko..au utakuwa ni mhariri wa lile gazeti la Udaku la Dira wewe siyo bure...!

Jitu la hovyo kbs yaani wewe unawezaje kusimama na kuwatukuza wazungu pamoja na yoote mabaya waliyokufanyia bado unasimama na kuwatukuza?
Mkuu The Big Show, umeweka jina kubwa na jitu kubwa kumbe wewe ni kubwa jinga tuu!. Mwalimu Nyerere alitufundisha kumuita mtu mjinga sio kumtukana, bali mjinga ni kutojua, akielimishwa akajua, ujinga utakuwa umemtoka hivyo anakuwa sio mjinga tena, lakini mjinga ukimuelimisha halafu ujinga haujamtoka, huyo sasa sio mjinga bali ni mpumbavu, mpumbavu haelimishiki hata umuelimishe vipi, ndio maana humu jf kulikuwa na slogan, ficha upumbavu wako kwa kukaa kimya!.

Mimi bado naamini wewe ni lijitu lijanga tuu, yaani kubwa jinga, hivyo bado nachukua tena fursa hii kukuelimisha ili kukutoa huo ujinga wako, usipoelimika, then nitajiridhisha kuwa na wewe kuba jinga sio mjinga bali ni mpumbavu, then sitapoteza tena muda wangu kukujibu!.

Biashara ya utumwa ilipigwa marufuku karne ya 17 wakati mkutano wa Berlin ni mwaka 1884!, kama ulidhani lengo la scramble na partition ni ili kujitwalia watumwa, wewe ni lijitu lijinga kabisa!.

Nani amesimama kuwatukuza wazungu?!. Nimesisitiza tangu mwanzo kuwa mada yangu ni biashara ya utumwa Unguja na Pemba! iliyofanywa na Waarabu, nimewaletea ripoti hapa, A report on slavery and the slave trade in Zanzibar, Pemba ...haijapingwa na waliokuwepo, nyie mnalazimisha niuzungumzie utumwa wa wazungu. Kama na wewe unayo ripoti ya wazungu walivyowafanya watumwa ulaya na marekani, ilete uianzishie uzi tuijadili, huu uzi ni kuhusu
Udhalimu wa Waarabu Unguja na Pemba: Jinsi Ndugu zetu walivyoteswa na Waarabu, walihasiwa, wanawake walibakwa, na watumwa kuuawa kinyama!.

Huu nyama unaofanywa na IS unaonekana ni unyama sana kwa sababu watu wanaona!, unyama kama huo, walifanyiwa mababu zetu ili hakukuwepo video na picha kutuonyesha, bali walikuwepo watu walioshuhudia, wakaandika walichokiona na hakuna aliyepinga!.

Pasco
 
Sorry but the whole post is pile of garbage. Someone with his right mind will never copy and paste another person work or research. Most research were done in biased.
Kwa Kiswahili mabaya waliyo yafanya wazungu wa Magharibu hutoyasoma hadharani.
Africa ilitawaliwa kinguvu na Wazungu, waArabu walikuja kama kibiashara. Yes Utumwa waliufanya.
Lakini usisahau, Bible ilitangulia mwanzo 6000yrs before Islam. Na Bible imeeleza utumwa na maauji mengi yaliyofanywa na mitume iliyopita.
In FACT, utumwa ulikuwepo even before the Jesus was born. Utumwa ulikuwepo wakati wa Roman Empire to Vikings.

Naomba uandike maisha kabla ya mapinduzi 1964.
Shida gani zilikuwepo? Madawa hospitalini, Kazi, MAISHA kwa wananchi, Elimu?
Mapinduzi yamefanywa, je Zanzibar imegain kitu gani?
As far as I am concern ZANZIBAR IS DEAD country. Ni mkoa katika Tanzania.
Hakuna maendeleo hata katika jambo moja. Watoto wanamaliza school hawajui hata kiswahili wacha kingereza.
Mahospitali hakuna dawa, Barabara mbovu, Mitaro yote inavuja maji machafu. Kunanuka.
Yapi ni matunda ya Mapinduzi????
Nimeandika mengi kuhusu Zanzibar, karibu.
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa, Walikimbia Wenyewe!.
[URL='https://www.jamiiforums.com/threads/miaka-50-ya-mapinduzi-matukufu-ya-zanzibar-bado-kuna-maswali-bila-majibu-1.573187/']Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Masw

Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kil
[URL='https://www.jamiiforums.com/threads/je-wajua-kuwa-kuna-uwezekano-tanzania-sio-nchi-halali-kisheria-de-jure-bali-ni-de-factor.578003/']Je, wajua kuwa kuna uwezekano Tanzania sio nchi halali Kisheria
[/URL]

Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua ..
[URL='https://www.jamiiforums.com/threads/miaka-50-ya-mapinduzi-matukufu-ya-zanzibar-bado-kuna-maswali-bila-majibu-1.573187/']Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Masw
https://www.jamiiforums.com/threads/kumuepushia-aibu-ya-kushindwa-ccm-isimsimamishe-dr-shein.807695/
Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. S
Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar? |
[/URL]
[/URL]

Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima
Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa M
Mbowe Alipua Bomu la Siri ya Ushindi Wa CCM Zanzibar!. W
[URL='https://www.jamiiforums.com/threads/inawezekana-vipi-zanzibar-hakuna-div-i-div-ii-wala-div-iii-wao-ni-div-iv-na-div-zero-tuu.409812/']Inawezekana Vipi Zanzibar Hakuna Div I, Div II, wala Div III ,

Live Star Tv: Mkutano wa CUF uzinduzi wa Kamati za Uchaguzi
Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar ...
Kumbe Rais wa JMT ni Nobody Zanzibar!. Waziri Mkuu Pinda ..
Uchaguzi wa Marejeo Zanzibar ni Huru na Haki! Tuyasubiri Matok
Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuw
Zanzibar: Japo SMZ ya SUK sio de jure tena bali ni de facto ...
[URL='https://www.jamiiforums.com/threads/je-abedi-amani-karume-alikuwa-na-wake-6-ana-watoto-wangapi.577081/']Je, Abedi Amani Karume alikuwa na Wake 6?

Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana
Bunge Maalum Lapigwa Changa la Macho!? Lapewa"Act of Uni
'Karume Hakuyakimbia Mapinduzi ya ZnZ'-Karume Jn

Pasco[/URL]
[/URL]
 
Nimeandika mengi kuhusu Zanzibar, karibu.
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa, Walikimbia Wenyewe!.
Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Masw
Jee Wajua Kuwa Tanzania Hatuna Mkataba wa Muungano?. Kil
Je, wajua kuwa kuna uwezekano Tanzania sio nchi halali Kisheria
Zanzibar Issue: Kwanini watu wanapiga kelele tu bila kuchukua ..
Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Masw
Kumuepushia aibu ya Kushindwa, CCM isimsimamishe Dr. S
Kuna haja ya kuhofia kurudiwa Uchaguzi Zanzibar? |
Dr. Shein Mfute Kazi Haraka, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar
Iwapo CCM itashindwa Zanzibar, Nini Majaaliwa ya Muungano
CUF kushiriki Uchaguzi wa Marudio Zanzibar si hiyari, Ni lazima
Hatimaye CUF 'Wameridhia' Rasmi, Kushiriki Uchaguzi Wa M
Mbowe Alipua Bomu la Siri ya Ushindi Wa CCM Zanzibar!. W
Inawezekana Vipi Zanzibar Hakuna Div I, Div II, wala Div III ,
Live Star Tv: Mkutano wa CUF uzinduzi wa Kamati za Uchaguzi
Imethibitishwa pasi na shaka kuwa ni kweli kabisa, Zanzibar ...
Kumbe Rais wa JMT ni Nobody Zanzibar!. Waziri Mkuu Pinda ..
Uchaguzi wa Marejeo Zanzibar ni Huru na Haki! Tuyasubiri Matok
Je, kunahitajika affirmative action ili Mzanzibari aweze tena kuw
Zanzibar: Japo SMZ ya SUK sio de jure tena bali ni de facto ...
Je, Abedi Amani Karume alikuwa na Wake 6?
Je, wajua kuwa Zanzibar haikuridhia Muungano? Ina Maana
Bunge Maalum Lapigwa Changa la Macho!? Lapewa"Act of Uni
'Karume Hakuyakimbia Mapinduzi ya ZnZ'-Karume Jn
https://www.jamiiforums.com/threads...cto-lakini-ipo-na-hakuna-aliyejiuzulu.981476/
Pasco
Pasco,
Kuna kuandika na kuandika.
 
PASCO
Baraghashia ni kofia na Baraghash ni jina.

Nimekubali kuwa PASCO si kipofu lakini ana makengeza yasiorekebishika. Anauona ukweli kwenye pembe ya mra ba uliopinda. Haduthi ulioiandika hapo juu haitafauyani na Alfu- leila ulela

Mjakazi wakati ule alijuulikana kama suria, na si MTUMWA. Baba yake TipTip alikuwa Gavana wa Sultan wa Zanzibar kule Tabora. Baba yake huyu alioa katika ukoo wa chifu Fundikira ( si mama wa TipTip) na kuishi nae uhai wake wote.

TipTip ni mfanya biashara ambae alikuwa anachukua pesa kutoka matajiri wa kiarabu na wakihindi kuja kuwa nunulia watumwa na meno ya tembo. Tiptip alikuwa anachukuwa wapagazi wa kinmyamwezi kumbebea meno ya tembo kwa ujira na watummwa hawakutumika kwa kazi hiyo kwa vile walitakiwa wafike Zanzibar kamili na afya bora ili wapate soko na kwa mauzo na bei ya juu. Wakati mwengine Tiptip ilibidi aiaharishe safari ya kurudi pwani mpaka msimu wa mavuno umalizike kwa vile inakuwa si rahisi kupata wapagazi wa kinyamwezi kubeba meno ya tembo mpaka Bagamoyo. Hapa ndipo ulipopatikana ule usemi maarufu wa " mzigo mzito mpeni mnyamwrzi"

Pasco elewa kwamba Mnyamwezi sawa na mzanzibari hawajawahi kufanywa watumwa. Tabora ilikuwani sehemu ya himaya (Mamlaka) ya Sultan wa Zanzibar. Wanyamwezi tokea karne hizo wanaingia Zanzibar na kabila lake ndio paspoti yake. Mpka hii leo kabila linalokubalika kutoka Zanzibar kutoka bara ni wanyamwezi tu.

Mateso na madhila waliopata watumwa ni wakati wa ukamataji na huo ulikuwa wanafanyiana watanganyika kwa watanganyika. Ukiangalia michoro yako ho juu watumwa wote walikuwa wamevishwa nguo za kujistiri mwili. Nani aliwapa nguo zile wakati huo bara walikuwa hawavai nguo na walikuwa wanakamatana uchi na vigozi au ukindu kiunoni tu.

PASCO ukibahatika kuja Zanzibar pitia museum na kusoma kitabu alichoandika mwenywe umelewe Tippu tip na utumwa. Tatizo utakalolipata na kiswahili kilichotumika, nia cha kale na fasaha na tofauti kabisa na kiswahili hiki cha kitanganyika tunachowasiliana. Ima kitafute kitabu kinachoitwa "TIPPU TIP The story of his career in Zanzibar & Central Africa"
Asante kwa uelimishaji.
Pasco
 
Back
Top Bottom