Wanabodi,
Lengo la uzi huu sio ubaguzi, au kuwakumbusha machungu ya Waarabu, bali ni kujikumbusha tuu historia na kuwaelimisha baadhi ya wenzetu, wasiowajua hawa Waarabu wa Unguja na Pemba waliwafanya nini mababu zetu!.
Ila pia naomba kutoa Maangalizo muhimu yafuatayo:
1. Tuwe makini sana na watu waliofilisika kiakili ambao watachanganya Uarabu na dini ya Kiislam simply because, Dini ya Kiislamu inatumia lugha ya Kiarabu!. Masikini muflisi hawa, hawajui kuwa hata Ukiristo umeanzia Arabuni. Wakristo na Waislamu ni watoto wa baba mmoja, Ibrahim, Waislamu ni uzao wa mwanae wa kwanza Ismail, aliyezaa na mjakazi wa ki Misri, na Wakristo ni uzao wa Isaka aliyezaa na mkewe Sara. Hata Yesu Kristo, licha ya kuzaliwa Israel, alikulia Misri na alizungumza lugha ya Kiarabu!. Hapa mimi nazungumzia udhalimu wa Waarabu kama jamii na sio dini ya Kiislamu.
Udhalimu ni udhalimu tuu hauna dini, wala kabila, wala jamii, kwa sababu kwenye udhalimu sio Waarabu tuu peke yao ndio madhalimu, watu wa mataifa mbalimbali wamefanya udhalimu kwa watu wa mataifa mengine, na mfano mzuri ni udhalimu wa Wajerumani kwa Mayahudi chini ya Hitler ulioitwa Halocust ambapo Hitler aliwaua Wayahudi zaidi ya milioni 6 kwa ukatili wa ajabu!, ila kwenye biashara ya Utumwa Unguja, Pemba, na Arabuni, watumwa hawa walihasiwa hivyo kufanyiwa genoside na wahusika sii wengine bali ndugu hawa hawa ndugu zetu Waarabu ambao leo tunakula nao, tunakunywa nao na kufurahi nao kwa vile tumeisha samehe na tumeishasahau, yaliyopita sii ndwele.
Hawa Waarabu wa leo, ni vizalia vya Waarabu wale wale, ila hawa wa sasa, ni Waarabu wema, wastaarabu kama Waarabu wa sasa, wenye roho nzuri, sio wakatili, sio wadhalimu na wanawapenda watu weusi na kuwaoa kwa mapenzi, huku wanawake wao, wakiwapenda weusi na wakiolewa nao japo mwanzo ilikuwa ni kwa kulazimishwa na Karume, hivyo nashauri, kwa siku zijazo, hata Waarabu hawa, ama machotaa wao, wakishiriki tena uchaguzi, wakashinda kwenye uchaguzi huru na wa haki, wapewe tuu nchi watawale kwa sababu Waarabu hawa sii wale, wasinyimwe kutawala eti kwa sababu tuu ni Waarabu.
Waarabu wa enzi za utumwa, walikuwa madhalimu, hivyo kuendelea kudhani hata hawa wazaliwa wao pia ni lazima watakuwa ni madhalimu!, kwa kanuni ya mwana wa nyoka ni nyoka!, hivyo wanashinda uchaguzi lakini hawapewi, sio kuwatendea haki.
Japo mwana wa nyoka nyoka lakini si lazima kila mwana wa nyoka awe ni nyoka mwenye sumu kali, nyoka wengine ni kama joka la mdimu, halina madhara, hivyo Waarabu hawa wa leo wamebadilika, kwa sababu hata shetani mwanzo alikuwa malaika, hivyo Waarabu hawa wa sasa ni Waarabu wema, ni wenzetu na ni sehemu yetu, ukifanyika uchaguzi tena, wakishinda, wapewe tu nchi.
Paskali