pasco,
Hadithi za chuki zisiokuwa na mashiko na kubabaisha watu. Wazanzibari wanaijua historia yao vizuri lakini kwa kifupi na kueleza kuwa.
1. Hakuna mzanzibari aliewahi kufanywa mtumwa! wazanzibari, walikuwa wanajuulikana kama "Sultan's Subjects" na kulikuwa na Decree ya hata kunyanyaswa na mtu yeyote seuze kufanywa mtumwa. Wazanzibari kama vile Mwinyi Mkuu wa Dunga (currently, kirembwe chake ni mwakilishi kwa tiketi ya CCM) alikuwa anamiliki watumwa sawa na virembwe vya maseneta wa Marekani walivyokuwa wanahodhi watumwa wa Kiafrika.
2.Wazanzibari hata waliochanganya damu na wanyamwezi walifanya biashara za utumwa na mfano wa wazi ni TipTip ( the great slaverer) aliotoka kwenye tumbo la kinyamwezi kabila la akina Fundikira.
3. Warabu hawakuvamia visiwa vya Zanzibar lakini walikwenda kuombwa na wazanzibari kuja kuwasaidia kuondoa utawala wa kidhalimu wa kireno uliokuwa ukiwaadhibu watu na kuwafanyia kila ufirauni unaojua na hata kuwalazimisha watu kuwa wakiristo kwa nguvu kama walivyokuwa wanafanya huko Oman. Ngome Kongwe waliijenga kwanza wareno na ndio iliokuwa gereza na ngome ya kutesa, kuua na ufirauni mwengine.Watu kama Pasco wanaona aibu hata kuzungumzia utawala wa Kireno Zanzibar kana kwamba hawajawahi kuvivamia na kuvikalia kwa mabavu kwa zaidi ya miaka 200
4. Missionari hawakuondowa utumwa kama unavyojidanganya na kutaka kuudanganya umma. Utumwa ulianzza kuondolewa na wamarekani, baaada ya vuguvugu ya watumwa weusi kujitambua na kuanza kudai haki zao. Vuguvugu hili lilionekana kuwa ni tishio kwa utawala wao, hasa ongezeko la watu weusi wanaoingia marekani kama watumwa ilikuwa inaongezeka kwa kasi. Ni woga huo ndio uliozaa azimio ya kuzuia utumwa na hivyo kumaliza ongezeko la watu weusi Marekani.
5.Udhalimu pekee ninanoujua dhidi ya wazanzibari ambao waliteswa, kubakwa, kuuwawa na kufanywa wawe wakimbizi ni ule ulio fanywa 2001 na mtawala mweusi, mkoloni mambo leo.
5 Picha ulizozibandika kuwa kama kielelezo (sijui zimeibiwa museum Zanzibar) ni sawa na picha za watumwa wa kiafrika waliopelekwa Marekani na wamissionari