Wanabodi,
Katika karibu kila jambo, kuna mazuri na mabaya yake, kama ilivyo kwa ukoloni, japo wakoloni walitunyonya, pia kuna mazuri, walituachia, ikiwepo elimu ya kisasa, walileta maendeleo mbambali ya kisiasa, kiuchumi na kijamii vikiwemo viwanda, miundombinu, maendeleo ya kilimo, ila pia walituletea dini za Kikristo, vivyo hivyo pamoja na mazuri ya Waarabu kuvivamia visiwa vya Zanzibar na Pemba na kuvitwaa kama mali yao, miongoni mwa mazuri waliyoyaleta Waarabu hawa, ni pamoja na kilimo cha karafuu, miundombinu ya ma kasri, pia Waarabu walileta dini ya Kiislamu visiwani Zanzibar.