DustBin
JF-Expert Member
- Jun 3, 2021
- 609
- 604
Viongozi na watawala wakijitahidi kufanya haki, uadilifu na usawa, wanaharakati watakosa kazi ya kufanya.
Wanaharakati ajira yao kubwa inayowakalisha mjini ni udhalimu unaofanywa na viongozi au watawala.
Ukiona hali ya hewa ipo kimya na wanaharakati hawana cha kusema, basi ujue viongozi wametekeleza majukumu yao na wanatenda haki, uadilifu na usawa wanafuata misingi ya utawala bora.
Lakini ukiona matamko, maandamano, na chokochoko vimeshamiri kwa wanaharakati hiyo ni ishara kubwa kwamba kuna tatizo kwa upande wa viongozi wao.
Na sio viongozi tu, hata watendaji wa ngazi za kawaida wanaposhindwa kufuata maadili na miongozo ya kazi zao, ikawa kuna mahali hapajakaa sawa huchochea kufufuka kwa wanaharakati.
Lakini pia kuna wanaharakati mimi napenda niwaite wanaharakati uchwara au wanaharakati wa maji taka, ukipenda wewe waite wanaharakati michongo.
Wao kila uchao watasikika hata katika jambo ambalo halina kichwa wala miguu ya kutembelea utaona wakilishupalia.
Hawa hupoteza hadhi na ladha ya uanaharakati. Harakati huleta mabadiliko chanya yanayochochea maendeleo.
Na hasa wengi wa aina hii ya wanaharakati ni hawa wanaojihusisha na mambo ya kisiasa.
Nimemaliza, mapovu ruksa.