UDSM Alumni
JF-Expert Member
- Jan 25, 2015
- 2,530
- 1,370
Shukrani kwa historia nzuri mzee
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wandugu...Sh Mohamed
Mwenyeezi Mungu awasamehe waliotangulia na sisi atujaaliye mwisho mwema InshaAllah
UDSM...Shukrani kwa historia nzuri mzee
Mzee Said na ukoo wa kina Sykes ni Tanga na Mombasa kwa kifupi 😅🤣🤣Unaona ulivyokuwa ukimnyenyekea! Umefunga mikono wakati yeye yupo kawaida. Ni kama Bwana na Mtwana wake mwenye miwani
njumu za kosovo said:Mzee Said na ukoo wa kina Sykes ni Tanga na Mombasa kwa kifupi 😅🤣🤣
Duh wazee mmetoka mbali aisee,Narumk,
Nimecheka sana.
Bwana na Mtwana.
Kitu gani kinachokughadhibisha kiasi hiki?
Kipi kibaya nilichofanya?
''Bwana'' Mzulu na ''Mtwana'' ni Mmanyema.
Angalia na hii nyingine tumepiga tulivyokuwa wadogo mwaka wa 1968.
Kleist alikuwa na miaka 18 mimi miaka 16:
View attachment 2996072
Kulia waliosimama wa kwanza ni mimi, Yusuf Zialor, Kleist Sykes Bubby Bukhari, Abdallah Tambaza.
Kulia wa kwanza waliochutama Abdul Mtemvu, Wendo Mwapachu na Kais
Tatizo lake ni moja tu...hana muda na Watanganyika wa asili wa miaka hiyo, muda wake wote ni wale walowezi, babu zake Wamanyema na wajomba zake Wazulu.Asante sana kwa historia nzuri.
Mag,Tatizo lake ni moja tu...hana muda na Watanganyika wa asili wa miaka hiyo, muda wake wote ni wale walowezi, babu zake Wamanyema na wajomba zake Wazulu.
Chama cha AA ilipoundwa mwaka 1930 na Gavana Donald Charles Cameron, hamtaji kabisa Rais mwasisi wa hicho chama, Mwalimu Cecil B. Matola, Myao na Mtanganyika.
Hata kwenye picha hasemi huyo mwasisi na Rais wa kwanza wa AA kasimama wapi. Anapokuja kukosea ni kudai ni historia ya Tanganyika badala ya historia ya mababu zake.
Tusisahau kuwa nyakati hizo hayo makabila mawili hayakuwepo kwenye orodha ya makabila ya Tanganyika bali walikuwa ni walowezi waliotoka Congo na Afrika Kusini.
Unanikumbusha mengi uchezaji unaousilimulia pia ulituhusu hata sisi. Ilikuwa kawaida miaka hiyo ya 1960-1980 kwa kuundwa kwa vikundi vya jiving shuleni hasa katika shule za sekondari. Uvaaji ni kama unavyosimulia shati jeupe lenye mikono mirefu suaruali nyeupe viatu vyeuse na bow tie. uchezaji ulikuwa wa kuvutia sana, kweli umenikumbusha mbali.UDOGONI DAR ES SALAAM 1960s
Kila nipitapo Maktaba hukutana na picha zinazonikumbusha mengi.
Picha hii alinipa Abdallah Mgambo miaka mingi ilioyopita.
Ilipigwa kwenye picnic mwaka wa 1965.
Kulia ni Adam Kingui, Abdallah Mgambo na Kleist Sykes.
Hawa wote walikuwa wanafunzi wa sekondari.
Adam Kingui na Abdallah Mgambo wakisoma St. Joseph's Convent na Kleist Aga Khan.
Nakumbuka nini kwa hawa rafiki zangu?
Vipaji vyao.
Hawa wote walikuwa watoto wa Gerezani.
Adam Kingui alijaaliwa kipaji kikubwa sana cha muziki.
Nakumbuka akiwa Kitchwele Boys siku ya Parent's Day kulikuwa na maonyesho.
Adam na wenzake kama wanne walipanda kwenye jukwaa wamevaa mashati meusi bow tie nyeusi, suruali nyeusi na viatu vyeusi.
Kikundi hiki kikawa kinaimba na kucheza.
Walikuwa wanaimba nyimbo gani?
Walikuwa wanaimba nyimbo za Kizulu kutoka Afrika Kusini huku wanacheza.
Walikuwa wanacheza kwa steps yaani choreography.
Wanainama kwa pamoja na kuinuka hivyo hivyo.
Wanakwenda kulia na kushoto kwa pamoja.
Utapenda.
Hizi nyimbo zilikuwa za Manhattan Brothers kundi kutoka Johannesburg, Afrika Kusini, nyingine za Dorothy Masuka, Miriam Makeba na Spokes Mashiane.
Hii ilikuwa mitindo ya Jive na Kwela.
Nyimbo hizi zilikuwa maarufu zikipigwa Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC) toka miaka ya 1950.
Sisi kama watoto tuliathirika sana na mambo haya kama walivyoathirika wazee wetu.
Wazee wetu hapa Dar-es-Salaam wakivaa suti kama walizokuwa wakivaa vijana wenzao katika mitaa ya Johannesburg.
Adam namuona kwa macho yangu akicheza na kuimba pale jukwaani.
Nakumbuka siku moja Adam anatoka shule Kitchwele anakwenda kwao Mtaa wa Kipata na Sikukuu na mbele Livingstone.
Kanikuta mimi nimesimama duka la Mwarabu nyumbani kwa Mama Kilindi.
Radio ilikuwa inapigwa rekodi, "Young World."
Adam akasimama akawa anaimba ile nyimbo anafatisha neno kwa neno.
Adam tukicheza mpira pamoja uwanja wa Shule ya Nanaki.
Hii ilikuwa shule ya Masingasinga kabla ya uhuru 1961.
Adam alikuwa na kipaji cha mpira akicheza Fullham timu iliyokuwa Mtaa wa Kipata.
Lakini Adam alipenda muziki zaidi na akaanzisha bendi yake The Rifters yeye akipiga lead guitar.
Rifters waliondoka Dar-es-Salaam na wakahamia Mombasa katika miaka ya katikati 1970s.
Adam Kingui akiweza kuiga guitar la Steve Cropper, Bobby Womack, Bavon Marie na wapigaji wengine wengi.
Abdallah Mgambo alikuwa Pele wetu katika mpira - key player na star.
Alicheza Cosmopolitan toka yuko shule na ndiye alikuwa Head Prefect St. Joseph's Convent wakati wetu.
Abdallah alikuwa mtu mpole sana na nadhifu.
Kleist akicheza mpira mzuri.
Kuna kisa Kleist alinihadithia.
Alipewa hela akanunue viatu vya shule yeye akaenda Dar-es-Salaam Music and Sports House akanunua Puma viatu alivyokuwa akivaa Pele.
Hili duka lilikuwa maarufu sana kwa kuuza vyombo vya muziki pamoja na santuri na vifaa vya michezo yote.
Asubuhi Kleist na nduguze wanaingia kwenye Mercedes ya baba yao kwenda shule Kleist akaonekana kuvaa viatu vya zamani.
Kuulizwa akasema kanunua viatu vya mpira Puma.
"Sikupi hela nyingine kununua viatu vya shule utavaa hizo Puma zako kama Pele."
Nini kilikuwa kipaji cha Kleist?
Akikimwaga Kiingereza vuzuri sana utapenda kumsikiliza akizungumza.
Ndugu zangu hawa wote wametangulia mbele ya haki.
Tulibakia marafiki ndugu kwa mapenzi ya dhati hadi mwisho ukubwani na tukazikana.
Mwenyezi Mungu awasamehe dhambi zao na awatie peponi.
View attachment 2995987
Kulia Adam Kingui, Abdallah Mgambo na Kleist Sykes 1965