Udogoni Dar es Salaam 1960s

Udogoni Dar es Salaam 1960s

Mzee Said na ukoo wa kina Sykes ni Tanga na Mombasa kwa kifupi 😅🤣🤣
njumu za kosovo said:
Mzee Said na ukoo wa kina Sykes ni Tanga na Mombasa kwa kifupi 😅🤣🤣

Njumu...
Wala hujasema uongo.

Hakika namshukuru Allah kwa kunileta duniani kipindi kile, kuzaliwa na wazee hawa na katika mitaa ile.

Vinginevyo nisingeweza kuijua histori hii ya ukoo wa Sykes na kupata uaminifu wa kufunguliwa hazina ya nyaraka zao zilizoniwezesha kuandika kitabu cha historia ya uhuru wa Tanganyika kwa uhakika na ushahidi wa nyaraka na picha.

Kitabu hiki kimenifikisha Library of Congress Washington DC, Northwestern University, Chicago, University of Iowa, Iowa City, Zentrum Moderner Orient, Berlin na vyuo vingi Afrika.

Kote huko nazungumza na kukutana na wasomi wa sifa katika historia ya Afrika.

Wengi katika hawa wamekuwa marafiki zangu.

Kitabu hiki kimenijumuisha katika machapisho makubwa katika historia ya Afrika ndani ya Cambridge Journal of African History, Dictionary of African Biography na miradi ya uandishi ya Oxford University Press.

Nimehojiwa na vituo vikubwa duniani vya habari: BBC, VoA, DW, Radio Tehran, SABC.

Hapa nyumbani: TBC, AZAM, ITV, CLOUDS na vituo vingine vidogo na Online TV na FM Station nyingi.

Hapa JF nimeshinda Mwandishi Bora mara mbili mfululizo 2022 na 2023.
Nimepewa nishani tano jumla kwa uandishi wangu.

Haya ningeyapataje kama nisingeandika kitabu cha Abdul Sykes?

Umejiuliza kwa nini historia hii imevutia wengi kiasi hiki ndani na nje ya Tanzania?

Baba yangu alipokuwa akinihadithia maisha yake ya utotoni mitaa ya Gerezani na shule ya Al Jamiatul Islamiyya, na ujana wake Dar es Salaam ya 1950s hata yeye hakujua kuwa alikuwa akinipa elimu ambayo itakuja kuandika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Wakati huo mimi mdogo sana.

Baba yangu amemuona Nyerere kwa mara ya kwanza 1952 nyumbani kwa Abdul Sykes.

Huu ndiyo mwaka mimi nazaliwa.

Kwani ndugu yangu elimu hii ninayotoa hapa ya ukoo wa Sykes, Dossa, Plantan, Chaurembo na masheikh waliokuwa na Nyerere katika kupigania uhuru wa Tanganyika wewe inakukera?

Hukupendezewa ukoo wa Sykes kuwa sehemu ya historia ya ukombozi wa Tanganyika na sehemu ya historia ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere?

Baada ya kuandikwa kitabu cha maisha ya Abdul Sykes, Abdul na Ally Sykes wametunukiwa na Rais Jakaya Mrisho Kikwete Medali ya Mwenge wa Uhuru kwa mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hii ilikuwa katika sherehe za kuadhimisha miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

Afisa wa Ikulu alipokwenda ofisini kwa Ally Sykes kumfahamisha kuwa taifa limetambua mchango wa kaka yake na yeye katika kupigania uhuru yule afisa alitaka kujua nini wamefanya.

Ally Sykes alimpa kitabu cha Abdul Sykes akamwambia, "Yote tuliyofanya mimi na Bwana Abdul yamo ndani ya kitabu hiki."

Namshukuru Allah kuwa mimi ni sehemu ya historia hii.

1716455345850.jpeg

Siku ya Eid 2009
1716454209256.jpeg

Kushoto Kleist Abdul Sykes, Misky Abdul Sykes, Mwandishi nimeshika Medali ya Mwenge wa Uhuru ya Abdul Sykes, Aisha Abdu ''Daisy'' Sykes na Ilyaas Abdul Sykes
1716455738559.jpeg

Prof. Michael Lofchie Rafiki wa Ally Sykes University of Iowa, Iowa City
1716455914279.jpeg

VoA Washington DC
 
Duh huyu sykes ajengewe sanamu..sema hawa wamekula good time sana
Mema ya nchi wamekula

Ova
 
Narumk,
Nimecheka sana.
Bwana na Mtwana.

Kitu gani kinachokughadhibisha kiasi hiki?
Kipi kibaya nilichofanya?

''Bwana'' Mzulu na ''Mtwana'' ni Mmanyema.
Angalia na hii nyingine tumepiga tulivyokuwa wadogo mwaka wa 1968.

Kleist alikuwa na miaka 18 mimi miaka 16:

View attachment 2996072
Kulia waliosimama wa kwanza ni mimi, Yusuf Zialor, Kleist Sykes Bubby Bukhari, Abdallah Tambaza.
Kulia wa kwanza waliochutama Abdul Mtemvu, Wendo Mwapachu na Kais​
Duh wazee mmetoka mbali aisee,
 
Asante sana kwa historia nzuri.
Tatizo lake ni moja tu...hana muda na Watanganyika wa asili wa miaka hiyo, muda wake wote ni wale walowezi, babu zake Wamanyema na wajomba zake Wazulu.

Chama cha AA ilipoundwa mwaka 1930 na Gavana Donald Charles Cameron, hamtaji kabisa Rais mwasisi wa hicho chama, Mwalimu Cecil B. Matola, Myao na Mtanganyika.

Hata kwenye picha hasemi huyo mwasisi na Rais wa kwanza wa AA kasimama wapi. Anapokuja kukosea ni kudai ni historia ya Tanganyika badala ya historia ya mababu zake.

Tusisahau kuwa nyakati hizo hayo makabila mawili hayakuwepo kwenye orodha ya makabila ya Tanganyika bali walikuwa ni walowezi waliotoka Congo na Afrika Kusini.
 
Tatizo lake ni moja tu...hana muda na Watanganyika wa asili wa miaka hiyo, muda wake wote ni wale walowezi, babu zake Wamanyema na wajomba zake Wazulu.

Chama cha AA ilipoundwa mwaka 1930 na Gavana Donald Charles Cameron, hamtaji kabisa Rais mwasisi wa hicho chama, Mwalimu Cecil B. Matola, Myao na Mtanganyika.

Hata kwenye picha hasemi huyo mwasisi na Rais wa kwanza wa AA kasimama wapi. Anapokuja kukosea ni kudai ni historia ya Tanganyika badala ya historia ya mababu zake.

Tusisahau kuwa nyakati hizo hayo makabila mawili hayakuwepo kwenye orodha ya makabila ya Tanganyika bali walikuwa ni walowezi waliotoka Congo na Afrika Kusini.
Mag,
HISTORIA YA TANU IKO KATIKA KOO ZILIZOKUWA MSTARI WA MBELE KATIKA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA

Hebu tuanze kusoma historia ya TANU kuanzia mkutano wake wa kwanza Ukumbi wa Arnautoglo tuanangalia watu waliohudhuria mkutano ule.

NATAFUTA NA NATAFITI HISTORIA YA RASHID ALI MELI NA SAFARI YA NYERERE UNO 1955

Tafadhali nitafutie watoto au ndugu wa Rashid Ali Meli hapo Zanzibar.
Kijana wa Kingazija.

Aliishi Dar katika 1950s akifanya kazi Dar es Salaam Municipal Council kama Bwana Fedha.

Ana kisa cha kusisimua sana kati yake yeye, Iddi Faiz Mafungo Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) na TANU na Ali Mwinyi Tambwe katibu wa jumuiya hiyo katika historia ya TANU na safari ya kwanza ya Julius Kambarage Nyerere UNO February 1955.

Akiishi Mtaa wa Tandamti nyumba yake ikiangalia Soko la Kariakoo.
Alikuwa mume wa Bi. Bihuri.

Kwa miaka mingi nimekuwa nikitafuta habari zake na picha yake bila mafanikio.

Rashid Ali Meli ni kati ya watu wasiozidi 20 waliohudhuria mkutano wa kwanza wa TANU Arnautoglou Hall mwezi August 1954.

Miongoni wa waliohudhuria mkutano ule walikuwa: Julius Nyerere, Abdulwahid na Ally Sykes, Dossa Aziz, John Rupia, Mshume Kiyate, Makisi Mbwana, Jumbe Tambaza, Juma Waziri, Clement Mtamila, Rajabu Diwani, Schneider Plantan, Marsha Bilali, Rashid Ali Meli, Frederick Njiliwa, Iddi Faiz Mafongo, Iddi Tulio, Denis Phombeah na wengineo.

KISA CHA RASHID ALI MELI NA SAFARI YA NYERERE UNO 1955

Wakati mwingine waandishi wakigongana Maktaba kidogo inakuwa vurugu patashika nguo kuchanika.

Angalia zogo hilo:


View: https://youtu.be/51ks2tqezsA?si=-9rRQTHJg7HeOi7I

SELEMANI DITOPILE NA KISA CHA RASHID ALI MELI

Selemani Ditopile kaniandikia baada ya kusoma makala ya Rashid Ali Meli.

"Sheikh Mohamed ulichokieleza ni sawa na kweli kabisa Bw. Rashid Ali Meli alikuwa swahiba mkubwa wa marehemu baba yangu mzazi Bw. Ramadhani Mwinshehe yeye pamoja na Bw. Iddi Faizi Mafungo.

Baba yangu mzazi alitoa baadhi ya pesa ili swaiba wake asipate matatizo.

Bw. Rashid Ali Meli alikuwa anaishi Ilala Mtaa wa Kilosa ambapo sasa ndiyo makao makuu ya NCCR- Mageuzi.

Bw. Rashid Ali Meli amezikwa Bunguruni kwenye Makaburi ya Wahiyao."

SELEMANI DITOPILE ANAKAZIA KUHUSU RASHID ALI MELI

Selemani Ditopile kaniandikia tena:

"Rashid Ali Meli alikuwa na mtoto mmoja aitwae Ali Rashid Ali Meli ambae alikuwa anafanya kazi Government Stores nae amefariki miaka ya 1980.

Nitamtafuta mjukuu wake Bw. Rashid.

Pia habari zaidi au taarifa zaidi unaweza kuzipata kwa mtoto wa marehemu Bw. Iddi Faizi Mafungo anaitwa Faizi ambae kwa sasa anaishi Dodoma.

Nitakupatia Number zake za simu.

Marehemu Mzee lddi Faizi Mafungu alikuwa anaishi Ilala Mtaa wa Moshi karibu na Habibu Punja Primary school au kwa sasa ni Shule ya Msingi Amana.

Nina uhakika ukimpata Faizi aweza kukupatia picha na taarifa zote za watu hawa."

Picha hiyo ya kwanza alinipa Faiz huyu ambae Selemani Ditopile amemtaja.

Ilikuwa katika miaka ya 1980.

Hiyo picha nyingine ya pili alinipa Araf Sykes kutoka Maktaba ya Picha ya Sykes.

Picha hii ya pili nimeipata hivi karibuni.

Kushoto ni Iddi Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramiyya, Julius Nyerere Saadan Abdu Kandoro na Haruna Iddi Taratibu, Dodoma Train Station.

1717164087724.jpeg
1717164152579.jpeg


Mag,
Tafuta katika vitabu vyote vya historia ya uhuru wa Tanganyika vilivyoandikwa: KImambo na Temu (1969), Olotu (1981), Chuo Cha CCM Kivukoni (1977).

Hakuna hata kitabu kimoja kilichotaja waasisi wa African Association.

Waasisi wa AA wametajwa kwa mara ya kwanza na Aisha ''Daisy'' Sykes mtoto wa Abdul Sykes kwenye Seminar Paper: AD Sykes, The Life of Kleist Sykes'' Ref. No. JAN/HIST/143/15, East Africana, University of Dar es Salaam, (1968).

(Daisy alikuwa mwanafunzi University of East Africa).

Waasisi hawa ni: Cecil Matola (President), Kleist Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Zibe Kidasi, Selemani Majisu, Rawson Watts na Raikes Kusi.

Hawa ndiyo waasisi wa AA mwaka wa 1929 wala si Gavana Donald Cameron.

Naijua historia yote ya wazee wangu.

Hawa wazee wangu Kleist Sykes, Mzee bin Sudi na Ali Jumbe Kiro wakaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika mwaka wa 1933.

Vyama hivi viwili vikashirikiana katika kupambana na ukoloni wa Muingereza.

1950 wakaunda TAA Political Subcommittee: President Dr. Vedasto Kyaruzi, Secretary Abdulwahid Sykes, Hamza Mwapachu, Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.

Tusimame hapa.
 
UDOGONI DAR ES SALAAM 1960s

Kila nipitapo Maktaba hukutana na picha zinazonikumbusha mengi.
Picha hii alinipa Abdallah Mgambo miaka mingi ilioyopita.

Ilipigwa kwenye picnic mwaka wa 1965.
Kulia ni Adam Kingui, Abdallah Mgambo na Kleist Sykes.

Hawa wote walikuwa wanafunzi wa sekondari.
Adam Kingui na Abdallah Mgambo wakisoma St. Joseph's Convent na Kleist Aga Khan.

Nakumbuka nini kwa hawa rafiki zangu?
Vipaji vyao.

Hawa wote walikuwa watoto wa Gerezani.
Adam Kingui alijaaliwa kipaji kikubwa sana cha muziki.

Nakumbuka akiwa Kitchwele Boys siku ya Parent's Day kulikuwa na maonyesho.

Adam na wenzake kama wanne walipanda kwenye jukwaa wamevaa mashati meusi bow tie nyeusi, suruali nyeusi na viatu vyeusi.

Kikundi hiki kikawa kinaimba na kucheza.
Walikuwa wanaimba nyimbo gani?

Walikuwa wanaimba nyimbo za Kizulu kutoka Afrika Kusini huku wanacheza.

Walikuwa wanacheza kwa steps yaani choreography.
Wanainama kwa pamoja na kuinuka hivyo hivyo.

Wanakwenda kulia na kushoto kwa pamoja.
Utapenda.

Hizi nyimbo zilikuwa za Manhattan Brothers kundi kutoka Johannesburg, Afrika Kusini, nyingine za Dorothy Masuka, Miriam Makeba na Spokes Mashiane.

Hii ilikuwa mitindo ya Jive na Kwela.

Nyimbo hizi zilikuwa maarufu zikipigwa Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC) toka miaka ya 1950.

Sisi kama watoto tuliathirika sana na mambo haya kama walivyoathirika wazee wetu.

Wazee wetu hapa Dar-es-Salaam wakivaa suti kama walizokuwa wakivaa vijana wenzao katika mitaa ya Johannesburg.

Adam namuona kwa macho yangu akicheza na kuimba pale jukwaani.

Nakumbuka siku moja Adam anatoka shule Kitchwele anakwenda kwao Mtaa wa Kipata na Sikukuu na mbele Livingstone.

Kanikuta mimi nimesimama duka la Mwarabu nyumbani kwa Mama Kilindi.
Radio ilikuwa inapigwa rekodi, "Young World."

Adam akasimama akawa anaimba ile nyimbo anafatisha neno kwa neno.
Adam tukicheza mpira pamoja uwanja wa Shule ya Nanaki.

Hii ilikuwa shule ya Masingasinga kabla ya uhuru 1961.

Adam alikuwa na kipaji cha mpira akicheza Fullham timu iliyokuwa Mtaa wa Kipata.

Lakini Adam alipenda muziki zaidi na akaanzisha bendi yake The Rifters yeye akipiga lead guitar.

Rifters waliondoka Dar-es-Salaam na wakahamia Mombasa katika miaka ya katikati 1970s.

Adam Kingui akiweza kuiga guitar la Steve Cropper, Bobby Womack, Bavon Marie na wapigaji wengine wengi.

Abdallah Mgambo alikuwa Pele wetu katika mpira - key player na star.

Alicheza Cosmopolitan toka yuko shule na ndiye alikuwa Head Prefect St. Joseph's Convent wakati wetu.

Abdallah alikuwa mtu mpole sana na nadhifu.

Kleist akicheza mpira mzuri.
Kuna kisa Kleist alinihadithia.

Alipewa hela akanunue viatu vya shule yeye akaenda Dar-es-Salaam Music and Sports House akanunua Puma viatu alivyokuwa akivaa Pele.

Hili duka lilikuwa maarufu sana kwa kuuza vyombo vya muziki pamoja na santuri na vifaa vya michezo yote.

Asubuhi Kleist na nduguze wanaingia kwenye Mercedes ya baba yao kwenda shule Kleist akaonekana kuvaa viatu vya zamani.

Kuulizwa akasema kanunua viatu vya mpira Puma.

"Sikupi hela nyingine kununua viatu vya shule utavaa hizo Puma zako kama Pele."

Nini kilikuwa kipaji cha Kleist?
Akikimwaga Kiingereza vuzuri sana utapenda kumsikiliza akizungumza.

Ndugu zangu hawa wote wametangulia mbele ya haki.

Tulibakia marafiki ndugu kwa mapenzi ya dhati hadi mwisho ukubwani na tukazikana.

Mwenyezi Mungu awasamehe dhambi zao na awatie peponi.

View attachment 2995987
Kulia Adam Kingui, Abdallah Mgambo na Kleist Sykes 1965​
Unanikumbusha mengi uchezaji unaousilimulia pia ulituhusu hata sisi. Ilikuwa kawaida miaka hiyo ya 1960-1980 kwa kuundwa kwa vikundi vya jiving shuleni hasa katika shule za sekondari. Uvaaji ni kama unavyosimulia shati jeupe lenye mikono mirefu suaruali nyeupe viatu vyeuse na bow tie. uchezaji ulikuwa wa kuvutia sana, kweli umenikumbusha mbali.
 
Back
Top Bottom