KERO UDOM – Department ya Foreign Language and Literature Inaharibu Future za Wanafunzi!

KERO UDOM – Department ya Foreign Language and Literature Inaharibu Future za Wanafunzi!

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Hii Department ya Foreign Language na Literature ya University of Dodoma kuna tatizo kubwa sana.

Wanawafelisha wanafunzi bila msaada wowote. Mfano hai ni LG 102 (Communication Skills)—hili somo limekuwa kama “filter” ya kuangusha watu. Wengi wanakwama hapo, hakuna msaada, hakuna majibu.

Mimi ni mhanga, Nimefatilia ofisini kwa mkuu wa idara nimeambulia majibu ya hovyoo, nimefatilia kwa walimu majibu yaleyale, Mwisho wa siku wakanambia niandike barua lakini Nimeandika karibu barua 10 kwa miaka 2—hakuna hata moja iliyojibiwa. Mwisho? Nimekata tamaa kwa sababu ya somo moja tu.

Ukimfuata Mkuu wa Department, hupati msaada—anakaa kujisifia elimu yake na nyadhifa zake, na anaenda mbali mpaka kukuambia hata ukiandika barua ikifika kwake atakufanya uishie kudisco tu.

Inauma kuona ndoto ya mtu inaishia kwenye somo moja wakati system imekataa kusaidia.
 
Back
Top Bottom