TUNTEMEKE
JF-Expert Member
- Jun 15, 2009
- 4,587
- 580
Udom ni janga la taifa,kwa kipindi kirefu tumekuwa tukifuatilia mambo yanavyoendelea chuo kikuu cha Dodoma(udom),kiukweli chuo hiki kimekuwa kikiendesha kibabe,kisiasa na ni chuo pekee Tanzania ambacho hakifuati haki za binadamu wala maazimio ya kimataifa kuhusiana na haki za wanafunzi na wanataaluma.Katika kipindi cha mwaka mmoja chuo kikuu cha dodoma kimewafukuza wanafunzi wasiopungua 800 bila ya kujitetea.Pale college of humanities and social science wanafunzi 511 walisimamishwa masomo tar 13/06/2011 na hadi hii leo vijana hao hawajarudishwa kuendelea na masomo.Tukijaribu kuangalia muda waliokaa vijana hawa nyumbani ni mwingi sana na wengine wamekata tamaa na hawana tena matumaini ya kuendelea kupata haki yao ya kimsingi ya elimu.Wengi wao wamekuwa waangaikaji mitaani na kwa upande wa akina dada wameamua kuolewa au kujiuza.College ya education wanafunzi 89 wametimuliwa,natural science 108 na infomatics ni wanafunz 66.Mzaz usimpeleke mwanao Udom hapafai kabisa,vijana wanafukuzwa kama mbwa na hakuna wa kuwatetea,wanafukuzwa hata bila kusikilizwa na maamuzi yote yanakuwa influenced na mtu mmoja anayeitwa Shabani Mlacha.vijana wanaosoma udom hivi sasa wamekuwa waoga na hawana ujasiri hata wa kuhoji mambo ya kawaida ambayo wao kama wasomi wana haki na niwajibu wao kuhoji na kudadisi.Kwa udom ikionekana umehoji tu kitu chochote basi unapewa barua ya kufukuzwa chuo. Vijana wanakufa udom na maumivu yao,hali imekuwa mbaya hivi sasa hata wahadhili wanafukuzwa bila utaratibu.Nitaendelea kuwaletea mengi yanayoendelea Udom ili muweze kuepukana na janga hili la taifa.Mh rais Jk tunakuomba uingilie kati suala la Udom vinginevyo taifa litakuwa limekula hasara pale Udom.Tunaomba vijana hawa waliokaa nyumbani kwa muda wa mwaka mzima warudishwe kuendelea na masomo na wahadhili wote waliofukuzwa bila utaratibu wapatiwe haki zao.Mungu ibariki Tanzania.