UDOM kuna tatizo! Ndani ya mwaka mmoja wanafunzi 890 watimuliwa chuo, JK walijua hili?

UDOM kuna tatizo! Ndani ya mwaka mmoja wanafunzi 890 watimuliwa chuo, JK walijua hili?

TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Joined
Jun 15, 2009
Posts
4,587
Reaction score
580
Udom ni janga la taifa,kwa kipindi kirefu tumekuwa tukifuatilia mambo yanavyoendelea chuo kikuu cha Dodoma(udom),kiukweli chuo hiki kimekuwa kikiendesha kibabe,kisiasa na ni chuo pekee Tanzania ambacho hakifuati haki za binadamu wala maazimio ya kimataifa kuhusiana na haki za wanafunzi na wanataaluma.Katika kipindi cha mwaka mmoja chuo kikuu cha dodoma kimewafukuza wanafunzi wasiopungua 800 bila ya kujitetea.Pale college of humanities and social science wanafunzi 511 walisimamishwa masomo tar 13/06/2011 na hadi hii leo vijana hao hawajarudishwa kuendelea na masomo.Tukijaribu kuangalia muda waliokaa vijana hawa nyumbani ni mwingi sana na wengine wamekata tamaa na hawana tena matumaini ya kuendelea kupata haki yao ya kimsingi ya elimu.Wengi wao wamekuwa waangaikaji mitaani na kwa upande wa akina dada wameamua kuolewa au kujiuza.College ya education wanafunzi 89 wametimuliwa,natural science 108 na infomatics ni wanafunz 66.Mzaz usimpeleke mwanao Udom hapafai kabisa,vijana wanafukuzwa kama mbwa na hakuna wa kuwatetea,wanafukuzwa hata bila kusikilizwa na maamuzi yote yanakuwa influenced na mtu mmoja anayeitwa Shabani Mlacha.vijana wanaosoma udom hivi sasa wamekuwa waoga na hawana ujasiri hata wa kuhoji mambo ya kawaida ambayo wao kama wasomi wana haki na niwajibu wao kuhoji na kudadisi.Kwa udom ikionekana umehoji tu kitu chochote basi unapewa barua ya kufukuzwa chuo. Vijana wanakufa udom na maumivu yao,hali imekuwa mbaya hivi sasa hata wahadhili wanafukuzwa bila utaratibu.Nitaendelea kuwaletea mengi yanayoendelea Udom ili muweze kuepukana na janga hili la taifa.Mh rais Jk tunakuomba uingilie kati suala la Udom vinginevyo taifa litakuwa limekula hasara pale Udom.Tunaomba vijana hawa waliokaa nyumbani kwa muda wa mwaka mzima warudishwe kuendelea na masomo na wahadhili wote waliofukuzwa bila utaratibu wapatiwe haki zao.Mungu ibariki Tanzania.
 
Ni dili kwauongozi wa Chuo kwani pesa iliyotengwa sio ajabu ilishalambwa ndio maana wanaona wakiwarudisha kashfa itaibuka ya pesa ziliyotengwa kwa ajili yao. Ninavyojua katika ranking ya vyuo vikuu bora duniani UDOM chaweza kuwa cha mwisho kwa ubora wa elimu duniani; hiki kingefaa kiwe Somalia, Pakistan au Nigeria kutoa taaluma ya kutega mabomu ya kujitoa muhanga kwani serikali imekisahau kabisaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa hadi basi.
 
kwa kosa gani? makosa hayalingani inawezekana wapo ambao ni halali kufukuzwa
 
kwa kosa gani? makosa hayalingani inawezekana wapo ambao ni halali kufukuzwa

walitimuliwa bila kupewa charges zozote.,cha kushangaza baada ya kukaa nyumbani wakatotewa charges zinazofanana kwenye magazeti.,waliondolewa chuo bila hata kuhojiwa.
 
kwa kosa gani? makosa hayalingani inawezekana wapo ambao ni halali kufukuzwa

Wanafunzi ni halali kufukuzwa, ila mafisadi na majizi ya mali za umma yanakenuliwa meno...
 
Udikteta na udhalilishaji umezidi udom.Mlacha ndo anakiua HIKI CHUO EE Mhe. RAIS DR. JAKAYA KIKWETE CHUKUA MAAMUZI YA HARAKA KUKINUSURU CHUO HIKI MAANA KITAKOSA WANAFUNZI.Hadi sasa nasikia kuna kijana amefariki dunia hapo chuoni kwa kukosa hela ya chakula alikuwa anaumwa ulcers!.HADI SASA WATU WANAISHI MAISHA MAGUMU KWA MAANA BOOM HALIJATOKA NA NJAA NI KALI SANA CHUONI HAPO,WANAFUNZ WANASHINDWA KUHOJI KISA WATAFUKUZWA CHUO.Hivi sasa muda wowote ule kuna kutokea MAANDAMANO NA MGOMO AMBAO HAUJAWAHI KUTOKEA HAPA TANZANIA KWA ELIMU YA JUU.Waziri wa elimu SHUKURU KAWAMBWA LAZIMA ATANG'OKA KWA VYOVYOTE VILE KWA MGOMO WA WANAFUNZI HAWA MAANA DEMOKRASIA HAIPO HAPO CHUONI.MY TAKE:WANAEUNZ HAWA WAPENI HELA ZAO ZA KUJIKIMU NDANI YA WIKI HII LA SIVYO MTAKIONA CHA MOTO.ACHENI KUSINGIZIA WANASIASA ETI KUWA WANACHOCHEA MIGOMO SABABU KUBWA NI UFISADI NA UZEMBE WA UONGOZI WA CHUO KWA KUCHELEWESHA pesa ya wanafunzi.Halafu WANAKATA SHILINGI ELFU TATU KWA KILA MWANAFUNZI BILA KUJUA ZINAENDA WAPI?Majibu yote anayo MLACHA.Huu ni wizi mtupu TUNAOMBA SERIKAL IFANYE UKAGUZ WA KINA KUPITIA CAG ILI WAZIRI WA ELIMU AWAJIBISHWE!
 
hakika udom ni zaidi ya janga la taifa.
 
duh!mabomu 800+ yametegwa mitaani!
Hii ni hatari sana.
 
Huyo mlacha ni m2 mwenye cheo kipi hapo udom?

Mlacha Shaaban aliyeoa sehemu moja na JK kwa akina Salma, aliwahi kuwaeleza wahadhiri kuwa wanachomzidi yeye labda ni UREFU NA UMASKINI!!! Ndo UDOM na ndiyo Tz yetu. Wanafunzi waliofukuzwa hamia Ekenford maana wenyewe hawafukuzi wanahitaji wanafunzi zaidi. Walioko majumbani waombe tena TCU baada ya Nkunya u never know!
 
Huyo mlacha ni m2 mwenye cheo kipi hapo udom?

anafahamika kama naibu makamu mkuu wa chuo anayehusika na mipango,fedha na utawala yaani DEPUTY VICE CHANCELLOR-PLANNING FINANCE AND ADMNISTRATION) CHA KUSHANGAZA KASOMEA KISWAHILI ETI ANAPEWA KITENGO HCHO!,kama sio kujuana n nini?.MLACHA NI MCHWA KWA UDOM KWA WANAFUNZI NA WAFANYAKAZI.HAFAI HATA PUNJE NA ANADHARAU SANA KWA BINADAMU WENZAKE.HANA UTU ANA MOYO WA CHUMA.Ni mchwa zaid ya MALKIA WA MCHWA.
 
Kama kufukuzwa ilifaaa atangulie kilanja wa mawaziri, maana yeye ndiye chanzo cha mgogoro kwa kusaini makubaliano na wanafunzi ili hali akijua anadanganya, na hakuna utekelezaji kwa hilo, unawahidi watu field practical, unawaacha wanafanya maandalizi, chuo kinagharamia gharama zote za kutafutia watu field, then zinabaki wiki mbili chuo kifungwe mnagoma kuotoa hela, unahis wanataaluma wa chuo kikuu wangefanya nin? ni lazima mgome. sema magamba hawakubaligi kushindwa.
 
Tena ni mpare jeuri asiyepimika, ndo shida za kuteuana kindugu katika madaraka. Profesa wa Vishazi huru na tegemezi. unaenda kumpa ofisi ya maswala ya finance ni tatizo ati.
 
Huyo mlacha ni m2 mwenye cheo kipi hapo udom?

ni dvc arc. Ni mtwasi wa jk kama mwema! Kuna yule dogo aliwakomoaga baada ya kusambaza waraka wao ili serikali ya wanafunzi itawaliwe na dini moja,wakamharibia pasport yake na dogo akaibukia uhamiaji wakiwa na pengo. Cjui bado yupo!
 
Back
Top Bottom