Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Baada ya Mdau wa JamiiForums.com kudai kuwa kuna changamoto ya Maafisa Usalama wanaosimama katika geti la kuingia Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kuwasumbua wanaopita hapo hasa Boidaboda na baadhi kuwataka watoe fedha taslim, ufafanuzi umetolewa kutoka chuo hicho.
Mdau alihoji uhalali wa fedha taslimu wanazotozwa Madereva Pikipiki na Bajaj na kueleza zinaelekezwa wapi na je ni halali au kuna mazingira ya 'upigaji'?
Hoja ya awali ~ SUMA geti la UDOM wanakamata vyombo vya usafiri na kuvitoza pesa. Je, zinaenda wapi?
UFAFANUZI WA UDOM
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Rose Mdami anafafanua:
Hizo ni tuhuma ambazo tumeona na tayari tumeanza kuchukua hatua kufuatilia kuhusu ukweli wake, pia suala hilo limekabidhiwa kwa mamlaka zinazohusika ikiwemo Vyombo vya Usalama kwa ajili ya kufanya uchunguzi.
Geti ambalo limezungumzwa na mtoa hoja linatumiwa na watu wengi wanaoingia kuelekea katika taasisi mbalimbali ikiwemo ya kwetu, na tumekuwa na kawaida ya kufanya mabadiliko mara kwa mara ya walinzi wanaosimamia eneo hilo ili kukwepa mwanya wa wao kuzoea na kufanya matukio kama hayo.
Mpaka sasa hatuwezi kukanusha au kukubali kuhusu tuhuma hizo, kama nilivyosema uchunguzi unafanyika, tunashauri mtu au watu wanaokutana na changamoto kama hizo ni vema wakawa wanatoa taarifa kwa mamlaka husika ili hatua zifanyiwe kazi, kwani kukaa kimya kisha kwenda kulalamika kwingine inamaanisha wanalea tabia hiyo.
Kilicholalamikiwa ni rushwa, Sheria inasema anayetoa na anayepokea wote wana makosa, kama mtu anaona amelazimishwa kutoa rushwa anatakiwa kuripoti na hata hapo getini kuna Kituo cha Polisi ambacho kinaweza kutumiwa kutoa taarifa.
Geti hilo limekuwepo kwa miaka mingi na limehudumia watu wengi, kwa nini tuhuma hizo zinakuja sasa? Inawezekana kuna kitu na ndicho tunakifuatilia.