Nimegundua hapa JF hakuna cha great thinker wala intellectual. Michango mingi niliyoisoma inaonesha jinsi gani wana JF wengi wana mawazo finyu na wala hawatumii bongo zao kufikiri. Watu mmekalia JK kupewa PhD na Udom, kuchangiwa pesa za kuchukulia fomu, na tamko la wasomi wa dodoma kulaani walkout ya chadema. Nasema wote mliozungumzia mambo hayo matatu mna mawazo "FINYU" na uwezo wenu wa kufikiri ni zero. Am sorry to say that but i have been bothered by such contribution from people who call themthelves great thinkers while in reality they are slow thinkers. Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo. Kwanza, wanafunzi wa udom hawahusiki kwa namna yoyote ile katika utoaji wa PhD za heshima, hivyo kuwalaumu kwamba wamempa JK digrii ya heshima halafu leo wanamgomea ni kichekesho... Pili lazima wewe umayejiita great thinker uutambue vizuri mchezo wa siasa jinsi unavyochezwa. Unatakiwa ufahamu kuna kitu kinaitwa "political propaganda". CCM wamepandikiza watu wao katika vyuo vyote kikiwemo UDSM hilo halina ubishi hata kidogo. Itakua ni kitu cha ajabu endapo kikundi kidogo cha wana ccm NDANI YA UDOM watapewa pesa na uongozi wa ccm mkoa ili wamchangie JK kwa jina la UDOM halafu baadae wewe unayejiita great thinker ukaamini kwamba pesa zimechangwa na wanafunzi wa UDOM.. Huwezi kua great thinker kwa kudanganywa kirahisi hivyo. Tatu, tamko lililotolewa na wale waliojiita wasomi wa dodoma kulaani wabunge wa chadema kumsusia kikwete ilikua ni kazi nzuri iliyofanywa na kitengo cha propaganda cha CCM kwa kutumia makada wake wachache waliopo chuoni hapo nasikitika kuona kwamba hata wewe unayejiita great thinker umeingizwa choo cha kike na kukubaliana na propaganda hiyo. Kumbuka siasa ni mchezo mchafu na wanasiasa hutumia njia zozote zile ili kutimiza malengo yao. Huo ndio mchezo wa siasa. Naomba tuwaunge mkono vijana kuliko kutoa kauli za kuwakatisha tamaa. Hiyo DARUSO mnayoisema ilishachakachuliwa siku nyingi limebaki jina tu wanafunzi wa UDSM walinwea tangu ulipoanzishwa utaratibu wa wanafunzi kusajiliwa kila mwaka.