UDOM: MGOMO wa wanafunzi warindima

UDOM: MGOMO wa wanafunzi warindima

Post nyingi za hii thread zimeshikamana na propaganda za ccm za kutaka udom ionekane ni chuo cha ccm.Nilishawahi kusema humu kuwa image ya udom inavyoonwa na wengi walio nje yake.Wengi wa watu hawa wanaamini wanachokisikia na kusoma kwenye vyombo vya habari.Sio kweli kwamba wanafunzi wa udom walimchangia kikwete hela ya fomu ya uraisi.Sio kweli wanafunzi wa udom wamempa shahada JK.Sio kweli kwamba wanafunzi wa udom walilaani kitendo cha wabunge wa chadema kususia hotuba ya kikwete.Sio kweli kuwa wanafunzi wa udom wamewahi kuandamana kumuunga mkono Pinda kuhusu mapambano ya mauaji ya albino.Sio kweli kuwa wanafunzi wa udom walikabidhiwa kazi ya kumtafutia wadhamini mgombea uraisi wa ccm kabla ya kampeni za uchaguzi mwaka huu.Sio kweli kwamba wanachuo wengi wa udom ni wanaccm.Wanayoyafanya yote hayo isipokuwa hilo la shahada ya kikwete ambalo wanafunzi hawahusiki,ni wanafunzi wanachama wa ccm wa udom ambao kwa namna ya ajabu wameendelea kugeneralize ishu zao za kichama huku utawala wa chuo ukifumbia macho.Kuna mtu alishaandika thread humu akielezea hali halisi ya kisiasa udom.Alieleza ukweli mtupu na watu humu waliunga mkono sana tu.Inashangaza leo kutokea hili badala ya watu kuendelea kuamini kuwa udom sio CCMlized kama mnavyojua,mnazidi kukatisha tamaa harakati za vijana wanazozifanya kudhihirisha kwenu kuwa sio kweli mnayo/mliyoamini.Tupo pamoja na nyinyi wana Udom endeleeni kupigania stahili zenu.
mbona unawatetea, hata matendo yao yalionyesha kuna ukweli kwa kila jambo ulilokanusha.
 
acha wachachachuliwe,next time watumie pesa zao kula kiti moto cha goat na gongo badala ya kumchangia JK watapata akili labda!
 
Nimegundua hapa JF hakuna cha great thinker wala intellectual. Michango mingi niliyoisoma inaonesha jinsi gani wana JF wengi wana mawazo finyu na wala hawatumii bongo zao kufikiri. Watu mmekalia JK kupewa PhD na Udom, kuchangiwa pesa za kuchukulia fomu, na tamko la wasomi wa dodoma kulaani walkout ya chadema. Nasema wote mliozungumzia mambo hayo matatu mna mawazo "FINYU" na uwezo wenu wa kufikiri ni zero. Am sorry to say that but i have been bothered by such contribution from people who call themthelves great thinkers while in reality they are slow thinkers. Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo. Kwanza, wanafunzi wa udom hawahusiki kwa namna yoyote ile katika utoaji wa PhD za heshima, hivyo kuwalaumu kwamba wamempa JK digrii ya heshima halafu leo wanamgomea ni kichekesho... Pili lazima wewe umayejiita great thinker uutambue vizuri mchezo wa siasa jinsi unavyochezwa. Unatakiwa ufahamu kuna kitu kinaitwa "political propaganda". CCM wamepandikiza watu wao katika vyuo vyote kikiwemo UDSM hilo halina ubishi hata kidogo. Itakua ni kitu cha ajabu endapo kikundi kidogo cha wana ccm NDANI YA UDOM watapewa pesa na uongozi wa ccm mkoa ili wamchangie JK kwa jina la UDOM halafu baadae wewe unayejiita great thinker ukaamini kwamba pesa zimechangwa na wanafunzi wa UDOM.. Huwezi kua great thinker kwa kudanganywa kirahisi hivyo. Tatu, tamko lililotolewa na wale waliojiita wasomi wa dodoma kulaani wabunge wa chadema kumsusia kikwete ilikua ni kazi nzuri iliyofanywa na kitengo cha propaganda cha CCM kwa kutumia makada wake wachache waliopo chuoni hapo nasikitika kuona kwamba hata wewe unayejiita great thinker umeingizwa choo cha kike na kukubaliana na propaganda hiyo. Kumbuka siasa ni mchezo mchafu na wanasiasa hutumia njia zozote zile ili kutimiza malengo yao. Huo ndio mchezo wa siasa. Naomba tuwaunge mkono vijana kuliko kutoa kauli za kuwakatisha tamaa. Hiyo DARUSO mnayoisema ilishachakachuliwa siku nyingi limebaki jina tu wanafunzi wa UDSM walinwea tangu ulipoanzishwa utaratibu wa wanafunzi kusajiliwa kila mwaka.
 
...Duh yaani wewe ilimu yako ndiyo inakufanya uone kinyume cha great thinkers ni slow thinkers... !! Yeah rite... talk about exposing r ignorance... lol (themthelves great thinkers while in reality they are slow thinkers...)

Na join date ni Novv 2010 mmmhh...
 
Walisahau shukrani ya punda ni mateke hao.. shen***y kabisa watumie hata za moto

wasomi gani wanashabikia upuuzi...? kuna msomi anaweza kumchangia jk hela ya form?
halafu wakajidai eti na waraka wa kupinga movt za cdm kutoka bungeni...
 
UPUMBAVU mtupu, na wewe unajiita great thinker!!! Very poor level of analysis....jitu zima unaongea upuuzi. UDOM ni chuo kipya ndio kwanza kina miaka 3 eti unataka kukifananisha na udsm na sua. Wewe unaamini hizo pesa za Jk za kuchukulia fomu zimechangwa na udom?? Au unafikiri tamko la kupinga walkout ya wabunge wa chadema lilitolewa na wana udom! Ni kikundi cha wapuuzi wachache ambao hata udsm wapo. Mimi nimeshuhudia nilipokua nasoma udsm wanafunzi kibao wanarubuniwa kwa sh. 5000 na tishirt za kijani na njano na chakula kwenda kuwasikiliza viongozi wa ccm ubungo plaza na maeneo mengine....WE KILAZA unatakiw ujue jinsi propaganda za kisiasa zinavyofanya kazi sio kulaumu tu na kutetea uovu wa polisi.
 
Waeleze afisa,ila kumbuka pia humu JF lugha 'ngumu' haziruhusiwi...
 
udom walitakiwa kuendelea kudai madai yao kwa kutumia njia za busara. kugoma ni njia mojawapo lakini sio njia pekee na ya mwisho.
jambo la msingi ni kuwa serikali itafute ufumbuzi wa kudumu na isikie madai ya wanafunzi
 
Kweli kua uyaone. Elimu haitakiwi kuchanganywa na siasa hata siku moja. Kama elimu inashindwa kutufanya tuwe free thinkers, politics ndiyo itaweza kweli?
UDOM wanafunzi wanatakiwa wajue kuwa lengo lao la kuwa pale ni kusoma ili tusaidie kulisukuma hili Taifa liende mbele, na sio kujiingiza kwenye siasa za maji taka ambazo wala hazina mvuto. Mwisho wake ndio huu.
 
Nimegundua hapa JF hakuna cha great thinker wala intellectual. Michango mingi niliyoisoma inaonesha jinsi gani wana JF wengi wana mawazo finyu na wala hawatumii bongo zao kufikiri

Naomba tuwaunge mkono vijana kuliko kutoa kauli za kuwakatisha tamaa.

hata mimi nimeliona hilo. Watu wanachangia kiushabiki. Nyie watu wa wapi mnarudi nyuma badala ya kusonga mbele. Mambo ya mkwere na forms za mchango mlishajidili wee hadi basi.
Utafikiri nyie ni watakatifu sana na hakuna makosa mnayoyafanya!
Nyoyo zenu zina kutu, kila kinachofanyika kwenu ni kibaya. Halafu nimegundua wengi humu sio wapenda maendeleo wa ukweli.
Mngekuwa wana cdm wa ukweli kitendo walichofanya vijana mngekipongeza kama mlivyopongeza walkout ya wabunge kwasababu kwenu nyie jambo zuri ni kuwa against na ccm.
 
Nakuunga mkono...hata ma-lecturers wao wengi baadhi yao tunawajua..maghumashi matupu, kuna tunaowafahamu Under graduate walikua wanajikongoja..GPA ndogo kuliko set standards..Walikua wanawachukua tuu eti mtoto wa shangazi, ba mdogo nk.
Tutegemee nini kutoka kwa wanafunzi wao hasa uwezo wa kupambanua mambo...sikushangaa eti wanachanga pesa ya JK kuchua form...Sasa habari ndo hao. Wametumia. Akili mukichwa.
 
Nasikia leo kulikuwa na maandamano UDOM. Ni kweli? Yalikuwa ya nini? Nani ana Taarifa atujulishe?
 
kashakufa mmoja. Endelea kucheka.

No what, no who, no nini, pigaaaaaaaaaaaaa hawa wapuuzi si ndio walijifanya washabiki wa CCM, wajue now are just scrapers, they are used hawana value tena, pigaaaaaaaaaaaa, pigaaaaaaaaaaaaa, wanaleta kusupport CCM ili wapate akili, pigaaaaaaaaaaaaaaaa, don't stop pigaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, until they wake up waje CDM wenyewe, pigaaaaaaaaaaa na huyu huku anakimbia pigaaaaaaa
 
UDOM nyie si mabingwa wa kutoa matamko kuiunga mkono CCM. Mimi naunga mkono hoja ya nyie kupigwa mabomu tena kama FFU wameishiwa nawaomba wakaombe Morogoro. Na hicho chuo wengi walio soma hapo uelewa wao umepungua baada ya kujiunga na chuo hicho.Hivyo mabomu ni muhimu kuuzibua ubongo wao. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Nimegundua hapa JF hakuna cha great thinker wala intellectual. Michango mingi niliyoisoma inaonesha jinsi gani wana JF wengi wana mawazo finyu na wala hawatumii bongo zao kufikiri. Watu mmekalia JK kupewa PhD na Udom, kuchangiwa pesa za kuchukulia fomu, na tamko la wasomi wa dodoma kulaani walkout ya chadema. Nasema wote mliozungumzia mambo hayo matatu mna mawazo "FINYU" na uwezo wenu wa kufikiri ni zero. Am sorry to say that but i have been bothered by such contribution from people who call themthelves great thinkers while in reality they are slow thinkers. Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo. Kwanza, wanafunzi wa udom hawahusiki kwa namna yoyote ile katika utoaji wa PhD za heshima, hivyo kuwalaumu kwamba wamempa JK digrii ya heshima halafu leo wanamgomea ni kichekesho... Pili lazima wewe umayejiita great thinker uutambue vizuri mchezo wa siasa jinsi unavyochezwa. Unatakiwa ufahamu kuna kitu kinaitwa "political propaganda". CCM wamepandikiza watu wao katika vyuo vyote kikiwemo UDSM hilo halina ubishi hata kidogo. Itakua ni kitu cha ajabu endapo kikundi kidogo cha wana ccm NDANI YA UDOM watapewa pesa na uongozi wa ccm mkoa ili wamchangie JK kwa jina la UDOM halafu baadae wewe unayejiita great thinker ukaamini kwamba pesa zimechangwa na wanafunzi wa UDOM.. Huwezi kua great thinker kwa kudanganywa kirahisi hivyo. Tatu, tamko lililotolewa na wale waliojiita wasomi wa dodoma kulaani wabunge wa chadema kumsusia kikwete ilikua ni kazi nzuri iliyofanywa na kitengo cha propaganda cha CCM kwa kutumia makada wake wachache waliopo chuoni hapo nasikitika kuona kwamba hata wewe unayejiita great thinker umeingizwa choo cha kike na kukubaliana na propaganda hiyo. Kumbuka siasa ni mchezo mchafu na wanasiasa hutumia njia zozote zile ili kutimiza malengo yao. Huo ndio mchezo wa siasa. Naomba tuwaunge mkono vijana kuliko kutoa kauli za kuwakatisha tamaa. Hiyo DARUSO mnayoisema ilishachakachuliwa siku nyingi limebaki jina tu wanafunzi wa UDSM walinwea tangu ulipoanzishwa utaratibu wa wanafunzi kusajiliwa kila mwaka.

Poleni sana Vijana wenzetu huko Dodoma. Haki zenu mtazipata wala msianze kuona kana kwamba kushoto kulia mmekataliwa. Tunawapenda sana ila tabia ya baadhi yenu hapo nyuma kidogo yalitunyima raha kupita kiasi.

Naamini JF imesikia misononeko yenu na maonevu tele tu hapo chuoni. Naomba sasa muamini ya kwamba hapa JF Uwezo Tunao na tutayafanyia kazi hayo yanayowasibu kwa sasa kwa kutumia njia zetu wenyewe humu ndani. Nyie mtajionea tu matokeo huko.

Hata hivyo siku nyingine MSIDIRIKI KUPINGANA NA UMMA WA TAIFA ZIMA WANAVYOTAKA. Wana-JF nawaombeni sana, sasa yametosha na kama ni kujifunza na basi somo walipata vijana na kupata kutambua kuwa CCM ya leo si ile ya miaka ile. Tujiunge nao, tuwatie nguvu na tuhamasishe kupata haki zao watoto wa walipa kodi wa vijijini kama tulivyo sisi hawa. Nadhani badala ya kuona rangi za Ki-CCM muda wote wataanza kuona Utaifa zaidi tangu sasa.

Chonde!!
 
Mkuu hapo uko sahihi nakukubali sana tuwasamehe na tuwakaribishe hapa Jf kutetea haki.
 
Back
Top Bottom