UDOM: MGOMO wa wanafunzi warindima

UDOM: MGOMO wa wanafunzi warindima

Inasikitisha sana kwa jinsi ambavyo polisi walivyotuliza ghasia kupiga mabomu saa moja hadi tano asubuhi. Pia naushangaa ungozi wa chuo hasa utawala kushindwa kutafuta njia ya amani kutuliza mgomo, huwa wanakurupuka kuita polisi ktk mazingira ya chuo hata pasipo stahili.
Naiomba ofisi ya mipango, fedha na utawala, Udom waombe wapewe semina toka chuo kikuu cha Udsm jinsi ya ku handle migomo, wamtafute Prof. Mkandala na Mgaya watawapa shule ya kutosha kuondoa ujinga walio nao jinsi kutatua kero za wanafunzi. Pia wajifunze toka kwao jinsi migomo inavyotokea udsm hata wk nzima pasipo kuingiliwa hata na Auxiliary police! Sembuse wao mgomo kidogo tu msururu wa FFU na mabomu na upupu wao wa maji.

TCU nao wanashangaza kuidhinisha kozi za elimu ya juu zisizo na field work. Uhalali na ubora wa mhitimu wa namna hii ya Udom uko wapi? "This is just a new version of Advanced level sec. education"!

Pia ningependa kumuuliza Prof. Idris Kikula kulikoni? Kwa ujumla uongozi wake kama mkuu UCLAS na mkurugenzi IRA Udsm ulikuwa umetutuka. Alikuwa mtu msikivu, mwadilifu na mchapakazi. Iweje kwa uzoefu alionao haya yote yatokee Udom? Wanafunzi wanalia kero, na walimu nao ndo usiseme! Nahisi kuna nguli au kiwavi 1 kaingilia utawala wa chuo cha dodoma!

Mkapa ka chancelor, Bilali ka mwenyekiti wa bodi na JK ka mkuu wa mradi wa Udom chunguzeni ni wapi penye mushikeli na hima mparekebishe.
MUNGU IBARIKI TANZANIA, ITAKASE NA UFISADI KTK KILA NYANJA!
 
Nimegundua hapa JF hakuna cha great thinker wala intellectual. Michango mingi niliyoisoma inaonesha jinsi gani wana JF wengi wana mawazo finyu na wala hawatumii bongo zao kufikiri. Watu mmekalia JK kupewa PhD na Udom, kuchangiwa pesa za kuchukulia fomu, na tamko la wasomi wa dodoma kulaani walkout ya chadema. Nasema wote mliozungumzia mambo hayo matatu mna mawazo "FINYU" na uwezo wenu wa kufikiri ni zero. Am sorry to say that but i have been bothered by such contribution from people who call themthelves great thinkers while in reality they are slow thinkers. Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo. Kwanza, wanafunzi wa udom hawahusiki kwa namna yoyote ile katika utoaji wa PhD za heshima, hivyo kuwalaumu kwamba wamempa JK digrii ya heshima halafu leo wanamgomea ni kichekesho... Pili lazima wewe umayejiita great thinker uutambue vizuri mchezo wa siasa jinsi unavyochezwa. Unatakiwa ufahamu kuna kitu kinaitwa "political propaganda". CCM wamepandikiza watu wao katika vyuo vyote kikiwemo UDSM hilo halina ubishi hata kidogo. Itakua ni kitu cha ajabu endapo kikundi kidogo cha wana ccm NDANI YA UDOM watapewa pesa na uongozi wa ccm mkoa ili wamchangie JK kwa jina la UDOM halafu baadae wewe unayejiita great thinker ukaamini kwamba pesa zimechangwa na wanafunzi wa UDOM.. Huwezi kua great thinker kwa kudanganywa kirahisi hivyo. Tatu, tamko lililotolewa na wale waliojiita wasomi wa dodoma kulaani wabunge wa chadema kumsusia kikwete ilikua ni kazi nzuri iliyofanywa na kitengo cha propaganda cha CCM kwa kutumia makada wake wachache waliopo chuoni hapo nasikitika kuona kwamba hata wewe unayejiita great thinker umeingizwa choo cha kike na kukubaliana na propaganda hiyo. Kumbuka siasa ni mchezo mchafu na wanasiasa hutumia njia zozote zile ili kutimiza malengo yao. Huo ndio mchezo wa siasa. Naomba tuwaunge mkono vijana kuliko kutoa kauli za kuwakatisha tamaa. Hiyo DARUSO mnayoisema ilishachakachuliwa siku nyingi limebaki jina tu wanafunzi wa UDSM walinwea tangu ulipoanzishwa utaratibu wa wanafunzi kusajiliwa kila mwaka.

Mkuu unachosema kwa upande mmoja sahihi, japo choice yako ya maneno yanaweza yakaleta hasira, maana kwa mtu kuwa na mawazo tofauti a yale uliyoyafikiri hayamfanyi mtoa hoja kuwa na mawazo finyu.

Tukirudi kwenye hoja, binafsi nakubaliana na wewe kuwa ccm waligeneralize na kufanya u-DOM ionekana kuwa ni ya kwao.
Lakini swali ni kuwa kwa nini viongozi wa serikali ya wanafunzi walikaa kimya na kuwaruhusu hao unaowaita makada wa CCM kuzungumza kwa niaba yao??
1. walipotoa ile mil.1 ya fomu ya urais wa JK, kwa nn viongozi wa serikali ya UDOM hawakutoa kauli kuwa ule ulikuwa ni mchango wa wana CCM na sio wa jumuia ya udom?
2. wakati wa lile tangazo la kuiaani walk out ya CHADEMA ambalo lilitolewa kwa niaba ya wanafunzi wa udom wote hao viongozi walikuwa wapi wasiongee?? au ni woga?
kwa sabb wao walikaa kimya na wanakuja kulia lia sasa hv wasitegemee kupata public sympath wawe wapole tu sbb walishaharibu huko nyuma.
 
Yule Thobias Mwesiga aliyetoa tamko la kuwapinga Chadema kwenye walk out mbona sasa hajaita vyombo vya habari? Ivi UDOM cha kata ehe?kuna mkuu mmoja alikiita VODA FASTA! Mi nilikubaliana nae maana walimu wa sekondari ndo walipata ajira ya U Lecturer pale mfano mwl.wa Loyola sec. kama mwl.KAPINGA,walimu wa BreakThrough sec.pale Bagamoyo yan aibu tupu!
Aisee ndugu umeniacha hoi kwa uwezo wako mdogo sana wa kupambanua mambo, Hebu fikiria mwalimu kufundisha loyola au Breakthrough amabako hata mimi nimewahi kufundisha kwa wiki mbili wakati nasubiri mambo yangu yaninyookee ndiyo kutokuwa na sifa?

Kuwa mhadhiri Chuo kikuu hapa Tanzania kwa vyuo vya umma ni GPA ya 3.8, kwa mujibu wa TCU ni 3.5. Kwa upande wa UDOM hauwezi kupata mtu mwenyeGPA ya chini ya 3.8. Walimu wengin walioajiriwa hapa kwa mfano wale walioingia 2008 hakuna mwenye chini ya GPA YA 4.

Ninaomba nikueleze tu kwamba hapa UDOM kuna vijana wanajua nini wanafanya na wanauwezo mkubwa, ambacho kinakusumbua ni wao kukuacha huko Brearough au Loyola na kutokana na kuwa katika shule moja ulidhani mnalingana uwezo.Nitaomba katika hizo shule wawe wanawaonesha matokeo ya walimu ili mshiriki katika kumhurumia kwamba hastahili kubakia hapo.

Mwalimu Kapinga huenda humfahamu vizuri, Huyu ni mwalimu mkongwe ambaye amenifundisha UDSM nikiwa mwaka wa tatu kozi ya historia ya Afrika magharibi, je tatizo lake ni kuja UDOM? Labada nikuambie jambo moja kwamba kuna walimu wen wapo hapau walipewa offer na UDSM lakini katika maisha kila mmoja analengo yake. Pia wapo walimu wengi Udsm tuliosoma nao hata wao wanaukubali uwezo wetu, tuliwazidi darasani katika mijadala mpaka katika Transcript, lakini hii haiwaondolei uwezo wa kufundisha kwani wana sifa zinazotakiwa

Mawazo hayo hayatofautiani na mawazo ya walimu fulani wa shule moja ya kata huko mkulanga ambao waliletewa walimu kadhaa wenye digrii, wao waliwaona hao walimu kama ni watu waliopigika tu na wasiokuwa na sifa zozote za ziada mpaka baada ya hao walimu wenye digrii kuanza kupata kazi nyingine kubwa mmoja baada ya mwingine nakaiona hiyo tofauti. Ushauri wako kwangu usikate tamaa hata kama bado upo Loyola au breaough ongeza bidii ya kazi na uende shule hiyo ni njia pekee ya kuushinda wivu ulio nao.
 
No what, no who, no nini, pigaaaaaaaaaaaaa hawa wapuuzi si ndio walijifanya washabiki wa CCM, wajue now are just scrapers, they are used hawana value tena, pigaaaaaaaaaaaa, pigaaaaaaaaaaaaa, wanaleta kusupport CCM ili wapate akili, pigaaaaaaaaaaaaaaaa, don't stop pigaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa, until they wake up waje CDM wenyewe, pigaaaaaaaaaaa na huyu huku anakimbia pigaaaaaaa

ama kweli mchawi sio hadi apae na ungo.
Unachekelea kifo?!
Kweli mioyo inatofautiana.
 
Wanafunzi wa Kile chuo kikuu kinachojulikana kwa wengi kama chuo cha CCM, UDOM wameanzisha mgomo tangu jana usiku na kuendelea asubuhi hii.

Mgomo huo ambao hasa unafanyika katika chuo cha sayansi za jamii (social science) una madai makuu mawili moja likiwa ni madai ya kufanya mafunzo kwa vitendo na la pili ni kudai miundombinu bora. Taarifa zaidi zinadai kua wanafunzi wa social science wamekua wakibaguliwa linapokuja suala la mafunzo kwa vitendo. Mtoa taarifa anasema wanafunzi wameanza kuamshwa sa kumi alfajiri kwa viboko ili kuungana na wenzao na wanajipanga kuandamana kwenda ofisini kwa waziri mkuu....

WAKATI HUOHUO MABOMU YAMEANZA KURINDIMA KUTOKA KWA FFU.,.kumbe na chuo cha CCM WANAGOMA..

Mkuu nasri heshima kwako! Ninakufahamu fika kwammba wewe ni mdau mkubwa wa harakati hapa Udom. Tatizo ambalo limejitokeza katika thread yako ni namna ambavyo umeiandika hii thread, kwani badala ya Kupambana na propaganda ya CCM dhidi ya sauti za wanaharakati hapa Udom, umejikuta ukiziendeleza na ninaamini umelifanya hili kwa bahati mbaya kwani thread zako za baadaye zimeonesha kukerwa na wote wanaowashambulia vijana hawa waliogoma. mbinu ya kipropaganda uliyoiendeleza na inayotumiwa sana na CCM ni ile inayojulikana kwa kiingereza kma "Name calling" hapa majina mabaya yote huelekezwa kwa yule anaye onekana kwamba ni adui, mfano chuo cha kata, chuo cha CCM na mengine yanayofanana na hayo.
Lengo kuu la majina hayo ni kumfanya dui achukiwe na umma, kwa sasa wanajamii forum wameaminishwa kwamba Udom ni adui wao kutokana na propaganda hizi chafu. Huu ni mkakati wa kimakusudi unaofanywa na CCM ili kuwakatisha tamaa wanaharakati waliopo UDOM na wengine waliopo nje ya chuo ili wasitoe ushirikiano kwa wanaharakati wa ndani.

Sina sababu yakuelezea tuhuma moja baada ya nyingine inayoelekezwa kwa Udom kwani ninadhani nilijitahidi kutoa maelezo ya kina katika thread yangu "isemayo kufungua tawi la chadema udom".

Pamoja na mambo mengine kinachonishangaza nai kwa wanaharakati wa jamii forum kushindwa kuibaini janja ya CCM kuwagombanisha wanaharakati wa UDOM na watu wa maeneo mengine, hebu jiulizeni kunasababu gani kwa watu wote hata wale mashabiki wakubwa wa CCM katika thread zao kuiponda UDOM- harakati za vijana kupambana na mfumo huu mbovu, wanauchungu gani watu hawa.

Wengine wanasema kwa nini hamkukanusha taariza za kuchafua jiana la chuo? Jamani kwa wale tunaoishi dodoma hasa wanajumuiya ya Udom, hatuna imani na wawakilishi wa vyombo vya habari katika mkoa huu kwani asilimia kubwa wamewekwa mfukoni na viongozi wakuu wa Udom. ukipeleka jambo lolote unajikuta umeitwa katika ofisi za utawala. hali hii inakwamisha sana vijana kutumia vyombo vya habari kwa ufanisi.

Unaweza ukajiuliza mbona vijana wa ccm wanaweza? ni swali rahisi tu kwamba vyom bo vingi vya habari vinamilikiwa na maka wa CCM ambao hawako tayari kuona taswira ya Udom na ccm zikiandikwa kinyume cha matarajio yao.

Njia ambayo tunaiona rahisi ni kutumia jamii forums au mtusaidie kuunganishwa na Mwanahalisi , Tanzania Daima na Raia mwema. tunawahakikishia kabisa hatuwezi kuto taarifa za majungu ambazo hazina ukweli, bali tutawahakikishia taarifa za kina juu ya uozo wote wa Udom Pasipo kumuonea mtu yeyote na tutakuwa tayari kwenda mahakamni kama mashahidi wa magazeti hayo iatakapobidi.

Rai yenu kwenu wanaharakati wenzetu ni kwamaba tunaomba mtuungew mkono wana jumuiiya ya UDOM katika kuleta mabadiliko ya kweli huu ni mwanzo tu tunaomba mtarajie makubwa zaiodi kutoka kwetu.

Samahani, kunajambo nyeti nisipoligusia sitatenda haki nalo linahusu, JK kupewa udaktari wa Heshima. Kwa wale wanaojua utaratibu wa kutunuku, si kila mwalimu au mwanafunzi anahusika na jukumu hili, kimsingi ni kazi inayofanywa na jopo maalumu hasa kitu kinachoitwa baraza la chuo, na wengine wanobebeshwa lawama ni seneti ya chuo, vyombo hivi kimsingi vinaongozwa na viongozi waandamizi wa chuo ambao kimsingi kwa sababu chuo hiki ni kipya wateule wengi ni wa kikwete mwenyewe, kutokana na hali hii kipi ni kipya kwa jk kupewa? Ninawasilisha
Kuna wanafunzi wa social science ambao sasa wako mwaka wa mwisho lakini hawajawahi kufanya mafunzo kwa vitendo na hivyo wanahoji kua ni chuo gani kikuu ambacho hakina mafunzo kwa vitendo.??

MKuu tatizo kubwa ni pale nyinyi wenyewe mnaposhindwa kuanzisha mapambano......kabla ya wanaharakati kuwasidia inabidi nynyi muanze kwanza.

Wakati wale wenzenu walipopeleka ile mil.1 kama mchango wa wanafunzi wa Udom, wanaharakati mlikaa kimya, ilitakiwa muweke bayana kuwa huo ni mchango wa wana ccm wa udom, na hata pale wale wenzenu walipowasemea kwa niaba yenu kulaani walk out ya CHADEMA nynyi hamkujitokeza kuwapinga. kwa mazingira haya ni rahisi sana watu kuwagenerize.........But umeeleweka!
 
Mkuu hapo uko sahihi nakukubali sana tuwasamehe na tuwakaribishe hapa Jf kutetea haki.

Kuwasamehe ni sawa! Lakini WANAJUA KOSA WALILO LIFANYA? waulizwe kama hawajui waelimishwe Kwa sababu Yuko jamaa miongoni mwetu anaelaumu wa jf Sio great thinkers eti kwa kuwaambia wana UDOM kuwa sasa mmbwa kala mwanae: Mimi naongeza kwamba wanavuna walicho kipanda Wote wanaUDOM walijua hakika wanasafiri baharini wakamchekea panya aliyekuwa anatoboa mtumbwi badala ya kukemea ufisadi wa PANYA sasa umesha toboka na wanazama wote wakuzomewa ni nani kama si wana UDOM NASEMA UKIANGUKA USIGALEGALE CHINI JITAHIDI UINUKE PIA UNG'OE KISIKI ULIPO JIKWAA USONGE MBELE BILA HOFU TENA UTAFIKA! IDUMU UDOM IKIWA NA FIKRA MPYA
 
Aisee ndugu umeniacha hoi kwa uwezo wako mdogo sana wa kupambanua mambo, Hebu fikiria mwalimu kufundisha loyola au Breakthrough amabako hata mimi nimewahi kufundisha kwa wiki mbili wakati nasubiri mambo yangu yaninyookee ndiyo kutokuwa na sifa?

Kuwa mhadhiri Chuo kikuu hapa Tanzania kwa vyuo vya umma ni GPA ya 3.8, kwa mujibu wa TCU ni 3.5. Kwa upande wa UDOM hauwezi kupata mtu mwenyeGPA ya chini ya 3.8. Walimu wengin walioajiriwa hapa kwa mfano wale walioingia 2008 hakuna mwenye chini ya GPA YA 4.

Ninaomba nikueleze tu kwamba hapa UDOM kuna vijana wanajua nini wanafanya na wanauwezo mkubwa, ambacho kinakusumbua ni wao kukuacha huko Brearough au Loyola na kutokana na kuwa katika shule moja ulidhani mnalingana uwezo.Nitaomba katika hizo shule wawe wanawaonesha matokeo ya walimu ili mshiriki katika kumhurumia kwamba hastahili kubakia hapo.

Mwalimu Kapinga huenda humfahamu vizuri, Huyu ni mwalimu mkongwe ambaye amenifundisha UDSM nikiwa mwaka wa tatu kozi ya historia ya Afrika magharibi, je tatizo lake ni kuja UDOM? Labada nikuambie jambo moja kwamba kuna walimu wen wapo hapau walipewa offer na UDSM lakini katika maisha kila mmoja analengo yake. Pia wapo walimu wengi Udsm tuliosoma nao hata wao wanaukubali uwezo wetu, tuliwazidi darasani katika mijadala mpaka katika Transcript, lakini hii haiwaondolei uwezo wa kufundisha kwani wana sifa zinazotakiwa

Mawazo hayo hayatofautiani na mawazo ya walimu fulani wa shule moja ya kata huko mkulanga ambao waliletewa walimu kadhaa wenye digrii, wao waliwaona hao walimu kama ni watu waliopigika tu na wasiokuwa na sifa zozote za ziada mpaka baada ya hao walimu wenye digrii kuanza kupata kazi nyingine kubwa mmoja baada ya mwingine nakaiona hiyo tofauti. Ushauri wako kwangu usikate tamaa hata kama bado upo Loyola au breaough ongeza bidii ya kazi na uende shule hiyo ni njia pekee ya kuushinda wivu ulio nao.

we bwana mdogo miradi bubu acha kupotosha!mimi nina rafiki zangu watatu wanafundisha UDOM,wawili kati yao wana GPA 2.7-2.9 .ikiwa waliajiri lecturers feki kutoka kenya watashindwa kuchukua watu wenye G .P .A ndogo?
Chuo hiki kimeanzishwa kisiasa zaidi.hata hivyo ninashukuru kwa sababu baada ya miaka kama mitano hivi tutakuwa na wazururaji na majambazi yaliyopita chuo. yani ccm inajichimbia kaburi kilaini.
 
POle wewe kijana ninaona unatafuta umaarufu wa haraka, Kwa taarifa yako hapa mhadhiri kutoka kenya ni mmoja tu naye ni Prof. Anangwe, huyu prof ni kichwa kwelikweli. Hao jamaa zako wanaokudanganya kwamba ni walimu ni waongo kuna watu wengi sana wanatamani kuwa walimu lakini sifa haziruhusu, waulize vema huenda ni mawarden, administrative officers. Ninajua wewe ni mdogo wangu hivyo nitaendelea kukupa shule ya bure, waulize vizuri wanafundisha kozi gani? kama watakutajia , wakijitahidi watataja walizo soma huko, utwakamata katika misimbo ya kozi (code) sawa dogo??????????????

Back
Top Bottom