UDOM: Mwakibinga hana kosa, wanafuzi wagoma kuingia darasani mpaka wamuachie huru

Joined
Oct 8, 2014
Posts
21
Reaction score
2
Jambo ambalo lililopo UDOM ni kumuondo Philipo Mwakibinga ambaye ana mlengo wa CHADEMA na jambo hili linaonekana tokea wiki iliopita utawala walipanga katika kikao cha siri na viongozi wa Chama Cha Mapinduzi.

Wanafunzi wameamua kutoingia madarasani mpaka hapo watakapomuona waziri mkuu wao huyo wa kitivo cha sayansi na sana kwani wanajua hana kosa kwa ni mgogoro wake na Rais wa Federation ambaye ni UVCCM aliompigia kampeni asimu wake na kupelekea kushinda na kuamua kuchakachua.

Hii ikiratibiwa vyema na Mracha vice Chancellor wa Chuo cha Dodoma na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma.
 
Mleta mada unaongea upuuuz mtupu,watu tupo Darasani kama kawaida na vipindi vinaendelea nani akae nje na wakati UE inakaribia??usidanganye watu tymia akili zaidi hakuna mtu anaweza mbeba huyu jamaa anatafuta umaarufu wa kijinga saaaana
 
Duu huyu jamaa bado anasoma? Yuko vizuri saana huyu dogo nnakumbuka tulimuacha akiwa Rais wa kitivo cha social, maisha sio vyeti ajipange akachukue jimbo huko mbeya. ...hapo wanampotezea mda
 
Mleta mada unaongea upuuuz mtupu,watu tupo Darasani kama kawaida na vipindi vinaendelea nani akae nje na wakati UE inakaribia??usidanganye watu tymia akili zaidi hakuna mtu anaweza mbeba huyu jamaa anatafuta umaarufu wa kijinga saaaana

Mbona siye tumegoma?
 
Hivi hizo UVCCM na ukada wa CHADEMA na CCM vinaingilianaje na kuingia au kutoingia darasani? Gomeeni matatizo yenu ya msingi katika kudai elimu bora acheni siasa
 
Jambo ambalo lililopo udom ni kumuondo Philipo Mwakibinga ambae anamlengo wa chadema na jambo hili linaonekana tokea wiki iliopita utawala walipanga katika kikao cha siri na viongozi wa chama cha mapinduzi na katika mgomo huo imepelekea mwanafunzi mmoja kuaga dunia.


wanafunzi wameamua kutoiingia madarasani mpaka hapo watakapo muona waziri mkuu wao huyo wa kitivo cha sayansi na sana kwani wanajua hana kosa kwa ni mgogoro wake na Rais wa Federation ambaye ni uvccm aliompigia kampeni asimu wake na kupelekea kushinda na kuamua kuchakachua.

Hii ikiratibiwa vyema na Mracha vice Chancellor wa Chuo cha dodoma na Mwenyekiti wa ccm mkoa wa dodoma
 
Nyie watu wa UDOM lazima
mtambue kuwa hicho ni chuo cha
kata hivyo mnapotaka posho ya
10000 hatuwaelewi.
 
huyo mwakibinga naona mbowe am taftie jimbo haraka sana hapo dodoma watamuua...huyu jamaa ni mtu wa ajabu sana anapambana na ccm yote dodoma.

akishinda hii vita na mlacha sijui.

anahitaji msaada wa wanasheria.
 
Chuo cha CCM hicho,so mtajuana wenyewe,mm na watoto wangu baadae ni mwiko kabisa kusoma hicho chuo,hovyo sana udini na uccm upo hapo,:banghead:
 
Pamoja na kuwa tunatymia identy zetu,lakini kupitia mchango unawezajua uwezo na uelewa wa mtu vizuri,sasa MTAKA YOTE anaoneka ana ver low thinking capacity suala la chuo cha kata na demanding ya 10,000 kwa siku vina uhusiano gank???pili,wanafunzi wa udom wa diploma wanadai fesha zao hawajalipwa hadi sasa Mimi ni Administrator hapa sasa hizi kelele zako ndg.wazitoa wapi??Ama kweli Mjinga kazi kweli kumuelimisha!!
 
kwa jinsi ninavyoifahamu UDOM hilo haliwezi kufanyika UDOM jasiri ni Mwakibinga Pekee ............pole kaka
 
Tulioko mtaani tunaelewa thaman ya 10000 kwa siku ni nin wewe bado ni mwanafunzi kaa kimya
 
Nyie vitoto, Wazazi wenu waliwapeleka UDOM kusoma na si vinginevyo. Inatakiwa Kabla hujafanya lolote uwaulize wazazi wako maana ndio waliofanya uwe hapo na si vinginevyo. Mambo ya kufuata mkumbo mtakuja kujuta.
 
Tumesikia hundi ilishapelekwa benki kulipwa na wakielezwa kama wanataka nyongeza wapeleke madai yao kunakohusika. Sasa yote hayo ya nini. Acheni ulimbukeni
 
Hivi hizo UVCCM na ukada wa CHADEMA na CCM vinaingilianaje na kuingia au kutoingia darasani? Gomeeni matatizo yenu ya msingi katika kudai elimu bora acheni siasa
Kweli kabisa masomo kwanza siasa waende majimboni wakagombee.
 

hao wanafunzi wa diploma wamejitakia wenyewe, badala ya kujiunga na kozi za maana wakatapeliwa kirahisi, kwa taarifa yao maisha ya chuoni hapo ni rahisi kuliko hayo wanayojiandaaa kukumbana nayo, hayo ni mazoezi tu.
 
Hivi hizo UVCCM na ukada wa CHADEMA na CCM vinaingilianaje na kuingia au kutoingia darasani? Gomeeni matatizo yenu ya msingi katika kudai elimu bora acheni siasa

Taasisi za Elimu ya juu ni uwanja mzuri wa kuonyesha hisia na ujenzi wa hoja kwani husaidia kuandaa viongozi wa kisiasa na kijamii wa sasa na baadaye. Sio ushauri mzuri kuwaonya wasizungumze au kushiriki siasa kwani mfumo wa uendeshaji wa nchi yetu umejengwa katika mfumo wa siasa kama eneo muhimu katika uibuaji na upangaji wa malengo na usimamizi wa rasilimali.
Sikubaliani na ushauri wako kuwa vijana waachane na siasa. Naamini kuwa sio wote wenye misuli ya kufanya siasa na kusoma lakini wapo walio na huo uwezo na uzoefu unaonyesha kuwa vyuo vikuu vimekuwa chachu ya kuzalisha wanasiasa makini duniani kote. Angalia mfano wa akina Zitto, Halima Mdee, Samwel Sitta na wengine wengi unaweza kuongeza.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…