UDOM na PhD kwa wanasiasa. Nini chanzo cha mchezo huu katika elimu ya nchi hii?

duh!!! Sioni umuhimu wa elimu hapa TZ, nawahurumia vijana walioteseka kusoma kindagaten mpaka chuo kikuu bila kazi, huku wakiteseka mitaani bila kulipwa fidia ya muda waliopoteza darasani na gharama walizotumia kusomea.

Heri Mungu ashuke aichukue dunia. Tuachane na upuuzi wa dunia hii.
 
SUA huwa wako strictly na huwa hawajipendekezi kwa wanasiasa ma orof wamejikita kwenye kuandika miradi na tafiti so hawana njaa ya kujipendekeza kwa wanasiasa Ili wateuliwa, Mimi mwanasiasa aki graduate SUA, nitaamini hyo PhD yake
Mwanasiasa gani akasome SUA? Yaani aisha Dodoma akasome SUA?
 
Wengi wanaokoment hapa ni vilaza na wasiojua nini maana ya PhD. Kama unaona PhD wanaichukua tu si nenda na wewe ukaichukue.
 
Mi binafsi kama mwanazuoni wa chuoni nasema kama vyuo hivyo vimeamua kuwazawadia PhD wanasiasa kama njugu zinavyogawiwa acha wagawiwe tu.

Sometimes kipofu akiamua kumuongoza kipofu mwenzake acha wote wadumbukie shimoni. Mi sinaga huruma na mtu au taasisi ya kipumbavu. Kwani chuo kikuu cha Dar es Salaam kilikuwa nafasi ya ngapi kwa ubora Afrika miaka ya 90 na leo hii kipo nafasi ya ngapi? Leo hii VC wa UD na genge lake wanahangaika kuiokoa UD isiendelee kuporomoka lakini wapi....ukifanya upumbavu mmoja wa msingi utakugharimu milele.

UD walianza hivi hivi, kudharau mambo ya misingi: mfano degree zilizopaswa kuwa miaka minne kuzifast track kuwa miaka mitatu ili kukidhi matakwa ya wanasiasa, kutoboresha miundombinu ya kufanyia tafiti, n.k. Madhara yake wamekuja kuyaona miaka 20 baadaye, I swear elimu inayotolewa UD leo hii yaani ni bora mtoto akaende straight veta after form six.

Ni suala muda tu hivi vyuo vyetu kupuuzwa kabisa kabisa na jamii.
 
... "kila chuo kina utaratibu wake"; hicho ndio kiini cha tatizo!
Jibu ni ndio na hapana. Utaratibu wa chuo lazima uendane na matakwa na vigezo vinavyowekwa na tume ya vyuo vikuu (TCU).
 
Hiyo ndio CCM ya Magufuli na Samia
 
Hahaaa, eti alikuwa evening classes
 
Biteko na Jaffo kutwa wako kwenye kazi za uwaziri, na kwa kipindi cha Mwendazake wizara zao(madini na TAMISEMI) pamoja na ya Nishati zilikuwa ndiyo mawaziri wako "on the move 24/7". Wanapata wapi muda wa kufanya utafiti chini ya Magufuli?

Labda kwa vile Magufuli naye PhD yake ilikuwa ya hivyo hivyo pengine alibariki UHUNI huu wa PHD mchongo. Wananunua tu, hamna namna wanaweza kufanikisha kwa miaka 4.

Ni bora usome Master's degrees hata 2 kwa sasa kuliko PhD kwa watu wasio vyuoni au kwenye tafiti. Hizi PhD zimepoteza hadhi na ndiyo maana hata yule mjinga wa darasa la Saba kutoka Geita ameagiza ya kwake kwa USD 500 na kapewa.

Nashauri ikiwezekana TCU ifanye academic audit ya haya matakataka ya UDOM na ikikuta kuna mianya iwachukulie hatua stahiki
 
SUA huwa wako strictly na huwa hawajipendekezi kwa wanasiasa ma orof wamejikita kwenye kuandika miradi na tafiti so hawana njaa ya kujipendekeza kwa wanasiasa Ili wateuliwa, Mimi mwanasiasa aki graduate SUA, nitaamini hyo PhD yake
Hata muhas..hakuna huu upuuzi..ila vyuo vya vilaza udsm na udom njaa tupu.

#MaendeleoHayanaChama
 
Nadhani hoja kuu hapa ni mustakabali wa ubora wa elimu yetu kuanzia chini hadi juu...
Haya mengine ni matokeo tu!
 
Ndiyo maana mleta mada kasema kila kitu ni siasa,na bahati mbaya vijana wengi hawataki kufuatilia siasa.
 
SUA huwa wako strictly na huwa hawajipendekezi kwa wanasiasa ma orof wamejikita kwenye kuandika miradi na tafiti so hawana njaa ya kujipendekeza kwa wanasiasa Ili wateuliwa, Mimi mwanasiasa aki graduate SUA, nitaamini hyo PhD yake
I agree [emoji1666][emoji1666] wako very strict.
 
Kuna jamaa anaitwa Msemakweli alishtukia hizo PhD za mchongo akatoa na kitabu wahusika hawakuchukuliwa hatua zozote.Sasa watanzania wameona kuwa ili upate uteuzi au madaraka makubwa ya kisiasa na kiserikali basi lazima jina lako lianze na Dr of Professor .Hata kwenye vikao vyetu vya mtaani ni ujiko sana mtu kuitwa Doctor .Tuseme ukweli nani hataki kuitwa Doctor.Big up wenye PhD za kweli na za mchongo.Kwahiyo Mzee Mwandosya atulie pale wazee waliopoanzia vijana wanamalizia nao wanataka kula keki ya Taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…