Udom: Tabia ya kuwaongezea coursework wanafunzi waliofeli inakatisha tamaa

Udom: Tabia ya kuwaongezea coursework wanafunzi waliofeli inakatisha tamaa

UDOM SR

Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
47
Reaction score
26
Naomba nijitambulishe kwanza mimi ni mwanafunzi wa UDOM ambaye nilidisco UDSM. Sasa tokea nimeanza kusoma hapa UDOM kuna mambo nayaona hayako sawa. kama inavyojulikana wanafunzi wa hapa wengi uwezo wa darasani ni mdogo hivyo tunawaburuza tu darasani.

Sasa kuna tabia ambayo ni common kwa karibu vyuo vishiriki vyote vya udom ya kuwaongezea maksi za coursework wanafunzi ambao wanakuwa na maksi ndogo ili wasifeli.

Mara ya kwanza nilipoiona nikajua labda ni kwa somo moja tu, baadae nikaona kila somo, baadae nikaona na course nyingine nao wanafanyiwa hivyo hivyo, baadaye nilipowauliza na wa vyuo vingine naambiwa hiyo ni kawaida hapa udom.

Kwa mfano kuna somo mwanafunzi wa kwanza ana c/w ya 35 out of 40 na wa mwisho ana 1 out of 40, mwalimu alichofanya ni kumpa 20 yule mwenye 1 ili awe na 21 na kumpa 1 mwenye 35 ili kuondoa lawama asijelalamika kuwa yeye hajaongezewa.

Yaani wote waliokuwa chini ya 10 wameongezewa kati ya 15 - 20, bila fomula yoyote. Yaani mwalimu kapanga kuwa course work ya wanafunzi ianzie 20.

Mimi sikatai wanafunzi magarasa wasisaidiwe ila ninachopinga ni namna wanavyosaidiwa, kwa kuwaongezea maksi wanazidi kulemazwa ndio hawatasoma kwa kuwa wanajua kuwa wataongezewa tena.

Nafikiri njia bora ilitakiwa wapewe extra hours za kufundisha especially tutorials na baadaye wapewe make-up test hata kama zitatungwa below standard lakini at least ni njia inayokubalika katika vyuo vyote duniani.

Ila hili la kugawa free marks linadidimiza elimu halafu linawakatisha tamaa wale wanaojituma kwa juhudi zao. The whole examination process becomes pointless, its even hardly worth the effort to make a success out of it because it leads you nowhere.

Hili zoezi la kugawa maksi linafanywa na walimu mmoja mmoja huko madarasani, Hiyo yote ni tisa, kumi ni pale malecturer ambao hawaamini kwenye kugawa maksi wanapo-submit matokeo ya UE kwenye uongozi wa chuo.

Chuo kinaanza kugawa maksi kwa wanafunzi waliofeli sana na kupunguza maksi kwa wanafunzi waliofaulu sana. Hili lilitokea semester iliyopita karibu vyuo vishiriki vyote vya UDOM ndio maana matokeo yalichelewa sana kutolewa.

Wenyewe wanadai eti wana-standardize, eti matokeo yoyote yale lazima ya-reflect the so called "Normal distribution curve". waliosoma statistics wanaelewa maana yake ila literally inamaanisha kuwa katika darasa lazima kichwani wawepo wachache tumboni wengi bila kukosa mkia.

Sasa kwa kutumia hii style hamuwezi kujua kama somo watu wamefeli sana tatizo ni mtaala au mwalimu anayefundisha haeleweki au delivery methodology au kuna tatizo gani.

Sasa kwa kutumia hii style ya kuongeza maksi matatizo mengi ya kielimu UDOM yanajificha yanakuja kuonekana huko makazini ambako mtu aliyesoma UDOM tena kwa ufaulu mzuri anakuja kuonekana ana uwezo mdogo at its best.

Kuna taarifa zisizothibitishwa kuwa walimu wa UDOM wameambiwa wahakikishe wanafunzi hawafeli ili chuo kisikose ada kwa kuwa hakipati ruzuku serikalini ambayo itawalipa wao mishahara.

Hii inamaanisha kuwa mwanafunzi kufeli UDOM ni mpaka aamue yeye mwenyewe kuondoka chuo na mabegi yake maana hata kama husomi ila upo around maksi utapata tu labda uende kuwashitaki kwa nini wamekupa maksi wakati wewe mwenyewe hutaki, of which is impossible.

Now I was asking myself, are we still having a university at UDOM or a breeding center for fake proffessionals? Please, I know some of Administrators visit this site, try to work on these concerns for the betterment of our colleges.

If anyone disputes these facts, he/she can pm and i will forward the copies of some of the tempered coursework with respective names of their lecturers.

Ni hayo tu
 
Udom kuna matatizo mengi sana ila at least hayo mengine unaweza kuyavumilia kwa kuwa hayagusi moja kwa moja academic affairs ila hili la kugawa maksi limenifika shingoni siwezi kulivumilia. Nitavumilia mengine kama ya

Udini - Pale education watu wa dini ile inayotukuzwa udom wamepewa jengo zima la madarasa walitumie kuswalia wakati pana uhaba wa madarasa. Sio kama wa dini nyingine ambao wanasali kwenye madarasa jumamosi na jumapili lakini siku za wiki wanafunzi wanayatumia kusomea. Ma-ustaadhi wao wanadai jengo lina "UDHU" hivyo wanafunzi hawawezi kusomea baada ya wao kuswali. Sasa busara ilikuwa kuwapa eneo wajenge msikiti lakini sio kuwamilikisha jengo zima lenye madarasa karibia sita eti ndio uwe msikiti, my foot!!

Siasa - Hiki chuo kinatumiwa kimkakati na chama cha kijani, yaani ajenda zote zinazotakiwa kupenyezwa kwenye elimu ya juu na magamba wanakitumia chuo hiki. Anyway haya nitayaandikia thread yake.
 
Tuvumilie tu, atakuja Makamu Mkuu wa Chuo mwingine na Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo mwingine wenye mitazamo ya kitaaluma zaidi kuliko kidini, bila shaka mambo yatabadilika, hata kama ni miaka mitano ijayo
 
Udom kuna matatizo mengi sana ila at least hayo mengine unaweza kuyavumilia kwa kuwa hayagusi moja kwa moja academic affairs ila hili la kugawa maksi limenifika shingoni siwezi kulivumilia. Nitavumilia mengine kama ya

Udini - Pale education watu wa dini ile inayotukuzwa udom wamepewa jengo zima la madarasa walitumie kuswalia wakati pana uhaba wa madarasa. Sio kama wa dini nyingine ambao wanasali kwenye madarasa jumamosi na jumapili lakini siku za wiki wanafunzi wanayatumia kusomea. Ma-ustaadhi wao wanadai jengo lina "UDHU" hivyo wanafunzi hawawezi kusomea baada ya wao kuswali. Sasa busara ilikuwa kuwapa eneo wajenge msikiti lakini sio kuwamilikisha jengo zima lenye madarasa karibia sita eti ndio uwe msikiti, my foot!!

Siasa - Hiki chuo kinatumiwa kimkakati na chama cha kijani, yaani ajenda zote zinazotakiwa kupenyezwa kwenye elimu ya juu na magamba wanakitumia chuo hiki. Anyway haya nitayaandikia thread yake.

ilitakiwa uangalie mazingira ya ibada zinazofanywa na waislamu kabla ya kulalamika. kwa siku wanatakiwa kuswali si chini ya mara tano. hivi ingekuwaje kama kila baada ya masaa matatu wanakutoeni darasani ili wao wapate nafasi ya kufanya ibada. jambo lingine lipo hivi kwa upande wa waislamu hususani mashuleni na vyuoni hawana utengano wa kimadhehebu hivyo basi waislamu wote huswali sehemu moja hali inayopelekea kuwa na uhitaji wa sehemu kubwa ya kufanya ibada kwa pamoja tofauti na wakristo mara utasikia wasabato wapo darasa hili casfeta kule na waroma darasa lao pia. Tunahitaji uvumilivu wa kiimani ili tuweze kusonga mbele kama Taifa.
 
My concern does not base on their prayer's time table, The issue here is how can they be allowed to hold the building intended for classes indefinitely while there is a shortage of classrooms? Can we give in to any religious demand at the expense of the academic routine? Afterall the main purpose of the institution is to offer education and not faith based activities. Any activity around the college should not interfere with the main purpose.
 
ilitakiwa uangalie mazingira ya ibada zinazofanywa na waislamu kabla ya kulalamika. kwa siku wanatakiwa kuswali si chini ya mara tano. hivi ingekuwaje kama kila baada ya masaa matatu wanakutoeni darasani ili wao wapate nafasi ya kufanya ibada. jambo lingine lipo hivi kwa upande wa waislamu hususani mashuleni na vyuoni hawana utengano wa kimadhehebu hivyo basi waislamu wote huswali sehemu moja hali inayopelekea kuwa na uhitaji wa sehemu kubwa ya kufanya ibada kwa pamoja tofauti na wakristo mara utasikia wasabato wapo darasa hili casfeta kule na waroma darasa lao pia. Tunahitaji uvumilivu wa kiimani ili tuweze kusonga mbele kama Taifa.

My concern does not base on their prayer's time table, The issue here is how can they be allowed to hold the building intended for classes indefinitely while there is a shortage of classrooms? Can we give in to any religious demand at the expense of the academic routine? Afterall the main purpose of the institution is to offer education and not faith based activities. Any activity around the college should not interfere with the main purpose. Btw unaposema "waisilamu wanatakiwa kuswali si chini ya mara tano" wanatakiwa na nani? na chuo au? ni part ya curricullum yao au? Ebu tuache kuendekeza imani kwenye mambo ya msingi. Kila mtu na dini yake tukisema tumsikilize dini yake inataka nini na haitaki nini tutapoteza mwelekeo ndio maana kuna vyuo wasabato wamekataa kufanya mtihani jumamosi wamedisco. kuna shule wasabato wamekataa kuimba wimbo wa taifa wamefukuzwa. By the way mambo ambayo dini yao maustaadhi inawataka wafanye mbona ni mengi tu ikiwepo na kutozini na mengineyo mbona hawayafuati?

Wanafanya haya kwa kuwa wameona administration inawa-favor, na ipo religios bias.
 
Hawa ndio wasomi wetu wa "chuo kikuu"

Yes hawa ndio wasomi wetu kuna kitu hujakielewa tukueleweshe sisi wasomi? Poor girl, you are so delusional. Unafikiri kuna siku utapigiwa filimbi kuwa ni msomi. Msomi anaweza kuwa hata darasa la saba kama atatumia akili yake kutatua matatizo yanayomkabili yeye na jamii inayomzunguka. Kama umesoma halafu huwezi kutatua matatizo yako na jamii yako huna tofauti na i-d-i-o-t, ndio maana wanaojua msomi ni nani waliamua kuwapa degree watu walioumiza kichwa kutatua matatizo katika jamii bila kwenda shule.

and FYI degree za heshima zinaheshimika kuliko za darasani. we ulitaka tumalize chuo kwanza ndio tuanze kufikiria kutatua matatizo ya UDOM, poor girl.
 
Mtoa mada unalizungumziaje suala la wanafunzi Ku carry course, na je hujawahi kusikia mtu amecarry course? Na kama jibu ni ndio ulishawahi kujiulza kwanini wasiongezewe maksi? In reference to your post umesema uliwahi kuwauliza watu wakakuambia hiyo ni kawaida ya Udom, so nijibu plz maswali yangu hayo, Mi naona umepost kishabiki eti kwamba wewe ulidisco Udsm alafu Udom unawaburuza is this statement true? Unataka kuniaminishaje Mimi ambaye ni product nzur ya Udom!?
 
How fool you're ?

Back then you sound like a real insane !

:closed_2:

Wewe unaijua udom??

Huyo anaejiita udom sr atakuwa na bifu tu na udom ndo maana ppst zake nyingi anaiponda udom.

Ngoja ntakupigia picha baadh ya course work za wanafunzi ujionee wenyewe, carry over zilivo nyingi
 
Back
Top Bottom