Udom: Tabia ya kuwaongezea coursework wanafunzi waliofeli inakatisha tamaa

Udom: Tabia ya kuwaongezea coursework wanafunzi waliofeli inakatisha tamaa

Ukiweka kozi na idara iliyopo utakuwa na mantiki so far unabwabwaja tu!!!
Unataka ufuatwe PM ili iwe nini????!!!!

Kama wewe una facts tuma kwa PM yangu hizo courses zilizochakachuliwa!!!!!!!Au mpe Rais wa college husika then nipe namba yake PM Acha longolongo!!!!!

Kuhusu dini ni maneno yapo miaka nenda rudi ila hayana proof. Principal wa hiyo college unamjua???!!!
If yes mmempelekea hili kiwa vyumba havitoshi???!!!
DVC-ARc mmempelekea haya????!!!!
Serikali ya wanafunzi????!!!
 
Naomba nijitambulishe kwanza mimi ni mwanafunzi wa UDOM ambaye nilidisco UDSM. Sasa tokea nimeanza kusoma hapa UDOM kuna mambo nayaona hayako sawa. kama inavyojulikana wanafunzi wa hapa wengi uwezo wa darasani ni mdogo hivyo tunawaburuza tu darasani. Sasa kuna tabia ambayo ni common kwa karibu vyuo vishiriki vyote vya udom ya kuwaongezea maksi za coursework wanafunzi ambao wanakuwa na maksi ndogo ili wasifeli. mara ya kwanza nilipoiona nikajua labda ni kwa somo moja tu, baadae nikaona kila somo, baadae nikaona na course nyingine nao wanafanyiwa hivyo hivyo, baadaye nilipowauliza na wa vyuo vingine naambiwa hiyo ni kawaida hapa udom.

Kwa mfano kuna somo mwanafunzi wa kwanza ana c/w ya 35 out of 40 na wa mwisho ana 1 out of 40, mwalimu alichofanya ni kumpa 20 yule mwenye 1 ili awe na 21 na kumpa 1 mwenye 35 ili kuondoa lawama asijelalamika kuwa yeye hajaongezewa. yaani wote waliokuwa chini ya 10 wameongezewa kati ya 15 - 20, bila fomula yoyote. Yaani mwalimu kapanga kuwa course work ya wanafunzi ianzie 20.

Mimi sikatai wanafunzi magarasa wasisaidiwe ila ninachopinga ni namna wanavyosaidiwa, kwa kuwaongezea maksi wanazidi kulemazwa ndio hawatasoma kwa kuwa wanajua kuwa wataongezewa tena. Nafikiri njia bora ilitakiwa wapewe extra hours za kufundisha especially tutorials na baadaye wapewe make-up test hata kama zitatungwa below standard lakini at least ni njia inayokubalika katika vyuo vyote duniani. Ila hili la kugawa free marks linadidimiza elimu halafu linawakatisha tamaa wale wanaojituma kwa juhudi zao. The whole examination process becomes pointless, its even hardly worth the effort to make a success out of it because it leads you nowhere.

Hili zoezi la kugawa maksi linafanywa na walimu mmoja mmoja huko madarasani, Hiyo yote ni tisa, kumi ni pale malecturer ambao hawaamini kwenye kugawa maksi wanapo-submit matokeo ya UE kwenye uongozi wa chuo, chuo kinaanza kugawa maksi kwa wanafunzi waliofeli sana na kupunguza maksi kwa wanafunzi waliofaulu sana. Hili lilitokea semester iliyopita karibu vyuo vishiriki vyote vya UDOM ndio maana matokeo yalichelewa sana kutolewa. Wenyewe wanadai eti wana-standardize, eti matokeo yoyote yale lazima ya-reflect the so called "Normal distribution curve". waliosoma statistics wanaelewa maana yake ila literally inamaanisha kuwa katika darasa lazima kichwani wawepo wachache tumboni wengi bila kukosa mkia. Sasa kwa kutumia hii style hamuwezi kujua kama somo watu wamefeli sana tatizo ni mtaala au mwalimu anayefundisha haeleweki au delivery methodology au kuna tatizo gani. Sasa kwa kutumia hii style ya kuongeza maksi matatizo mengi ya kielimu UDOM yanajificha yanakuja kuonekana huko makazini ambako mtu aliyesoma UDOM tena kwa ufaulu mzuri anakuja kuonekana ana uwezo mdogo at its best.

Kuna taarifa zisizothibitishwa kuwa walimu wa UDOM wameambiwa wahakikishe wanafunzi hawafeli ili chuo kisikose ada kwa kuwa hakipati ruzuku serikalini ambayo itawalipa wao mishahara. Hii inamaanisha kuwa mwanafunzi kufeli UDOM ni mpaka aamue yeye mwenyewe kuondoka chuo na mabegi yake maana hata kama husomi ila upo around maksi utapata tu labda uende kuwashitaki kwa nini wamekupa maksi wakati wewe mwenyewe hutaki, of which is impossible.

Now I was asking myself, are we still having a university at UDOM or a breeding center for fake proffessionals? Please, I know some of Administrators visit this site, try to work on these concerns for the betterment of our colleges. If anyone disputes these facts, he/she can pm and i will forward the copies of some of the tempered coursework with respective names of their lecturers. Ni hayo tu

Wewe unasoma college gani?

Kama uko education hebu pita maeneo ya cafe uone koz zilivyo kuna carry over za kutosha kwa wote wasiofikisha kiwango husika.

Mim nasoma udom niko education , hayo ulioandika hakuna kabisa hapa.

Bahati mbaya niko mbali ila ningekuwekea ushahid baadh ya walioshindwa kufikisha hizo course work na wamecarry kozi.
 
Naomba nijitambulishe kwanza mimi ni mwanafunzi wa UDOM ambaye nilidisco UDSM. Sasa tokea nimeanza kusoma hapa UDOM kuna mambo nayaona hayako sawa. kama inavyojulikana wanafunzi wa hapa wengi uwezo wa darasani ni mdogo hivyo tunawaburuza tu darasani

Unajua udom inachukua mwisho point ngapi?

Hivi umewahi hata kusoma tcu guidebook ukaona udom mwisho inachukua ngapi.

Unapata wap ujasiri wa kusema wanafunzi uwezo wao ni mdogo?

Njoo na facts acha mipasho.
 
Mimi nilisoma udom, hicho kitu sijawahi kukitana nacho hata siku moja. Sio wote wanao disco hawana uwezo, ila nina mashaka na uwezo wako. Na hapo udom pia Utadisco
 
Kwa great thinker yoyote atatilia mashaka hii hoja yako. Kwanza kwa kutumia hiyo id ya UDOM na ulichokiandika, nina mashaka na wewe. Inawezekana kabisa wewe ni mfanyakazi pale udom na kuna ugomvi ndani ya taasisi. Ukisoma thread kwa umakini utagundua wewe si mwanafunzi ila upo hapa kumchafua fulani kupitia hiyo taasisi. Ngoja niangalie umejiunga lini humu jf kuhakiki nikifikiriacho.
 
Hayo ni baadhi ya matokeo kama yanavyoonekana kuna walipass na waliofeli

Haya thibitisha kuwa wanafunzi hawafail na wanaongezewa max.
 
Attachments

  • 1403196849644.jpg
    1403196849644.jpg
    89.5 KB · Views: 256
Kwa great thinker yoyote atatilia mashaka hii hoja yako. Kwanza kwa kutumia hiyo id ya UDOM na ulichokiandika, nina mashaka na wewe. Inawezekana kabisa wewe ni mfanyakazi pale udom na kuna ugomvi ndani ya taasisi. Ukisoma thread kwa umakini utagundua wewe si mwanafunzi ila upo hapa kumchafua fulani kupitia hiyo taasisi. Ngoja niangalie umejiunga lini humu jf kuhakiki nikifikiriacho.

Dont i sound like a student? I am, but also independent intellectual, always thinking out of the box
 
Hayo ni baadhi ya matokeo kama yanavyoonekana kuna walipass na waliofeli

Haya thibitisha kuwa wanafunzi hawafail na wanaongezewa max.

Ngoja nilete ushahidi sasa wa walimu wanaofanya huu mchezo
 
Ngoja nilete ushahidi sasa wa walimu wanaofanya huu mchezo

Leta ushahidi hapa kama unaweza, wewe si mwanafunzi kuna mtu unataka umchafue, hiyo kitu udom hakuna,

Na ushahidi nimekuwekea hapo , ukifaulu umefaulu na ukifeli umefeli.
 
Mkuu udom kuna uhaba wa madarasa??

Wewe kweli sijui wa wapi, mfano education kuna badhi ya lecture room hazitumiki mf ile inayotumika kuhifadhia teaching media.

We kama kuna mtu kakutuma uichafue udom bas jitahidi utafute facts.

Kuhusu udin mbona hata wakristo wamepewa lecture theatre zote huzitumia kila siku usiku na j2.

Narudia tena njoo na facts hapa sio unaaandika tu

Kuhusu wakristo kupewa theatre wazitumie jioni na sikuza jumamosi na jumapili hiyo siyo hoja iliyopo mezani, hoja ni waisilamu kutumia madarasa mojakwa moja yaani siku za wiki hayo madarasa huwezi kusomea, kwa lugha nyingine wamegeuza madarasa kuwa msikiti. Hizo theatre wanazotumia wakristo wewe mwenyewe umesema ni jumamosi na jumapili mbona siku za wiki tunazitumia kusomea. Jikite kwenye hoja
 
Kwa great thinker yoyote atatilia mashaka hii hoja yako. Kwanza kwa kutumia hiyo id ya UDOM na ulichokiandika, nina mashaka na wewe. Inawezekana kabisa wewe ni mfanyakazi pale udom na kuna ugomvi ndani ya taasisi. Ukisoma thread kwa umakini utagundua wewe si mwanafunzi ila upo hapa kumchafua fulani kupitia hiyo taasisi. Ngoja niangalie umejiunga lini humu jf kuhakiki nikifikiriacho.

Nimemuwekea na ushahidi wa picha hapo ikionesha matokeo
 
Kuhusu wakristo kupewa theatre wazitumie jioni na sikuza jumamosi na jumapili hiyo siyo hoja iliyopo mezani, hoja ni waisilamu kutumia madarasa mojakwa moja yaani siku za wiki hayo madarasa huwezi kusomea, kwa lugha nyingine wamegeuza madarasa kuwa msikiti. Hizo theatre wanazotumia wakristo wewe mwenyewe umesema ni jumamosi na jumapili mbona siku za wiki tunazitumia kusomea. Jikite kwenye hoja

Mkuu unaijua misingi ya uislamu? Mm si muislam lakini wale iman yao hairuhusu nyumba ya ibada kufanyika kwa mambo mengine.

Turudi kwenye hoja umesema udom kuna uhaba wa madarasa naomba uthibitishe hilo.

Mim nimekupa mf wa lecture room moja ambayo haitumiki hata kidogo yenyeww huhifadhia media tu.
 
Back
Top Bottom