UDOM yatwaa Tuzo ya ITU kwa Ubunifu wa AI inayokabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi

University of Dodoma (UDOM)

Public Institution
Joined
Feb 24, 2024
Posts
50
Reaction score
55
b431901e-cb37-460d-8aac-6ad030db5859.jpeg

Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) kimeendelea kuipeperusha bendera ya Tanzania katika jukwaa la kimataifa, baada ya kutunukiwa cheti “AI for Good Innovate for Impact Winner” na Taasisi ya International Telecommunication Union (ITU) kupitia mpango wa AI for Good, kufuatia ubunifu wake unaotumia Akili Bandia (Artificial Intelligence – AI) kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.

Katika mashindano ya Innovate for Impact 2026, takribani Suluhisho la matumizi ya Akili Bandia 400 kutoka kwa watafiti, wabunifu na taasisi mbalimbali duniani ziliwasilishwa na kufanyiwa tathmini kwa kuzingatia vigezo vya ubunifu, ubora wa kiufundi, athari kwa jamii, uwezo wa kupanuka (scalability) na mchango katika kufanikisha Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs).

Kati ya mawasilisho hayo, 267 yalichaguliwa kujumuishwa katika mkusanyiko rasmi wa Innovate for Impact 2026, huku 59 pekee yakitambuliwa kama washindi na kutunukiwa Innovate for Impact Winner Certificate.

UDOM ilipata mafanikio hayo kupitia kazi ya watafiti wake, Dkt. Florence Rashidi na Bw. Emmanuel Mkina, waliowasilisha ubunifu wenye kichwa “Climate Change Monitoring via ISAC- and AI-Enabled Cellular Networks: A Case Study in Tanzania.”

Ubunifu huo unapendekeza matumizi ya teknolojia ya Integrated Sensing and Communication (ISAC) kwa kushirikiana na Akili Bandia ili kutumia miundombinu ya minara ya simu iliyopo kukusanya taarifa za mazingira kwa wakati halisi. Taarifa hizo huchakatwa kwa kutumia mifano ya AI ya Spatio-Temporal Graph Neural Networks (ST-GNN) ili kutabiri uwezekano wa mvua kubwa na mafuriko. Baada ya uchambuzi, matokeo huwasilishwa kwa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa ajili ya uhakiki, na yakithibitishwa, tahadhari hutumwa kwa wananchi kupitia simu za mkononi kwa wakati muafaka.

Mafanikio haya yanathibitisha uwezo wa watafiti wa UDOM kubuni suluhisho za kisasa zinazotumia teknolojia za hali ya juu kutatua changamoto zinazoikabili jamii. Aidha, yanazidi kuimarisha hadhi ya Chuo Kikuu cha Dodoma kama taasisi inayoongoza katika utafiti, ubunifu na matumizi ya Akili Bandia kwa maendeleo endelevu nchini na katika jukwaa la kimataifa.

Tuzo hiyo ilitolewa katika jukwaa la kimataifa la AI for Good Global Summit 2026 lililofanyika Geneva, Uswisi, likiwakutanisha wabunifu, watafiti na taasisi kutoka nchi 51 duniani, zikiwemo Tanzania, Marekani, China, Uingereza, India, Canada, Australia, Ujerumani, Ufaransa, Brazil, Afrika Kusini, Kenya, Nigeria, Singapore na Falme za Kiarabu (UAE). Ushiriki huo mpana unaonesha kiwango kikubwa cha ushindani na hadhi ya mafanikio yaliyopatikana na UDOM katika jukwaa la kimataifa.
 
Hongera UDOM kwa kuzidi kujipambanua! Chuo Kikuu na Kikubwa Tanzania
 
View attachment 3632811

Watu wanawachukulia poa UDOM but they have no idea
 
Waache janja janja wajikite kwenye tafiti, wachapishe research papers nyingi mtandaoni ili chuo kiweze kuwa nafasi nzuri kimataifa.
 
Back
Top Bottom