UDSM-College of Engineering inaomba msaada

UDSM-College of Engineering inaomba msaada

Ukipita mtaani utawakuta wanavyopiga kelele ooh, performance kwenye sayansi imeshuka, sasa hata iwe kubwa, na serikali yenyewe wala haina mpango nayo unafikiri itasaidia? Ndo maana wazazi wengi sasa hivi wamegeuka, wanawaambia watoto wao wasome arts waachane na upumbafu wa sayansi ya tanzania, ambayo haina dira wala mwelekeo.
Ila wakati nampigia kura JK sikufikiria kabisa kama atakuwa mzigo namna hii kwa taifa letu. Ameniboa to the max. Kama hatakuwepo mpinzani mwenye sifa ya kumpigia kura, nafikiri bora tu mwakani nisipige kura, kuliko kuchezea tena kura yangu kwa JK. Anatukatisha tamaa kupita kawaida.
 
Hii inaonyesha ni jinsi gani elimu isivyotiliwa umaanani katika nchi yetu. Leaders are busy after statistics. They want to use them for their political agenda.
Hivi kweli tutaweza kufika salama kwenye knowledge based economy kwa approach hii? I wish Makamba could answer this.Anatetea sana hizi safari na madudu mengine yasiyo na kichwa wala mguu kwenye hii system


Elimu ya UDSM ni mazingaombwe tu. Hakuna shule pale. Ufisadi, siasa, UZINZI, UFUSKA, KUDESA ndo yanayotamba pale. Ukimtoa mtoto wa UD ukimleta ofisini anachofanya ni bora umwajiri form four aliyesoma QT.
 
Elimu ya UDSM ni mazingaombwe tu. Hakuna shule pale. Ufisadi, siasa, UZINZI, UFUSKA, KUDESA ndo yanayotamba pale. Ukimtoa mtoto wa UD ukimleta ofisini anachofanya ni bora umwajiri form four aliyesoma QT.


sasa hiyo ndo inasababisha uchakavu wa miundombinu ya coet???

head if mango!!!!!!!!!!!!
 
Kiongozi,

Suala la sustainability ya mipango yetu ni tatizo sana sana. Nakumbuka kuna thread ya Bw. Zitto kumfagilia Chenge kwamba aliidhinisha funds kwa ajili ya barabara za huko Kigoma, nilijaribu kukataa hili suala la ujenzi wa miundombinu kwenda staili ya kisiasa, kiajaliajali na njia ya ku-lobby badala ya kuwa na roadmap ya kitaalamu hata kama kuna ukosefu wa fedha. Wengi walipinga hoja yangu na najua wataendelea kupinga hili lakini its is fair kusema hatuwezi kuendelea kwa staili hii. This method will never do the trick.

Binafsi nakataa kuwa nchi yetu ni maskini. Wengi wa watu wetu ni kweli wana kipato kidogo lakini si mafukara. Hata ukipita huko na huko majiani, barabara kuu na mitaani unakuta vijana na akina mama wakiwa na bidhaa mikononi n.k. wakitafuta wateja. Wakulima wadogo pamoja na serikali kutokuwa na mipango ya maana bado wanacho cha kuonesha..achilia mbali watu wengine ktk kada mbalimbali za maisha.etc

So it is not like watu wetu hawana kitu kabisa au hawana spirit ya kufanya kazi na kujiletea maendeleo yao.

Nadhani taifa linahitaji mass modernization. Modernization ambayo ni sustainable kama ulivyosema, kwenye shughuli zao za kujiongezea kipato na hata maisha yao binafsi, nia ni kuongeza uzalishaji na kila mtu kufikia surplus. Ikifikia hatua ya watu wa kipato cha kati na kipato cha chini kutengeneza surplus, in 1 and a half to 2 decades taifa litafikia level za nchi kama Malaysia.

Sasa kazi ya kuweka misingi na ku-spark modernization ni lazima tuwe na know-how na kuwapa watu wetu, nayo hakuna njia ya mkato kuipata hiyo knowledge. Taasisi za kutoa hiyo knowledge lazima ziwe sustained na kuchekiwa relevance ya products wanazotoa etc etc..right now it is sad, I don't see the roadmap, and I am sure the way things are we have failed before, we are failing now and we will continue to fail ad infinitum.


Mzalendo:

Huo msemo wako sustainability ni kitu kimoja alichoeleza mwandishi mmoja aliyefanya kazi SIDA (shirika la maendeleo Sweden) kueleza sababu ya kushindwa kwa misaada ya nchi zilizoendelea kwa nchi masikini kama Tanzania.

Huyo Professor anaposema: "The college development partners............ ". ana maana ya wafadhiri ambao misaada yao siku zote sio sustainable.

Ukweli wa mambo kuanzisha kitu kwa kutegemea development partners, serikali sio kazi kubwa. Kazi kubwa ni ku-maintain na kuendeleza. Na hiki ni kitu ambacho watanzania wote kwa ujumla inabidi tujifunze.
 
siyo serikali tu watanzania karibu wote hatujali maintenance na unakuta pesa ya matengenezo ndo inaliwa kwa ajili ya safari za wakubwa na mikutano.
 
Watu wanachekesha kweli.
yani wanasema hili swala lisiingizwe ktk siasa na wakati huo huo baada ya mistari miwili kuandika ktk post hiyo hiyo anasema tusiipigie kura ccm.

Tutakuwa wapumbafu kutoa hukumu kwa kuangalia upande mmoja. Mimi nafikiri hili swala liangaliwe kwa mapana.

Wanafunzi wanalipa ADA ambayo inalipwa na bodi ya mikopo na wengine kujilipia ktk chuo, na bado naamini serikali inatoa luzuku ktk chuo hiki ,hizi fedha zinaenda wapi??
mimi nafikiri tuangalie hili swala kimfumo wa utendaji wa viongozi wenyewe wa udsm.

Pale udsm vyoo sometimes vinanuka ,hii pekee inatia uwalakini.
 
Ukipita mtaani utawakuta wanavyopiga kelele ooh, performance kwenye sayansi imeshuka

This here don't make no sense! Performance ya sayansi imeshuka as if kuna wakati ilikuwa juu. What the hell?
 
Wakuu,
Chuo kuomba michango kwa wananchi ni jambo zuri. Inawezekana kabisa kwamba wandaaji wa kukusanya michango hii hawajaelimisha umma vizuri. Hata Harvard ambacho ni consistently number one college in the world, with billions of dollars in it's coffers, bado wanaomba michango especially kwa wanafunzi waliomaliza pale. Hata vyuo vya umma marekani [state colleges]vinafanya hivyohivyo. vyuo vina vitengo maalum kabisa vya kukusanya michango kutoka kwa alumni waliopita hapo. Mamilioni ya dola yanapatikana kwa njia hii.
Tumpe Prof. Katima hongera kwa kuwa mbunifu na tumuunge mkono.
 
This here don't make no sense! Performance ya sayansi imeshuka as if kuna wakati ilikuwa juu. What the hell?

Juli:

Yeah wakati wa Mpemba effect ilikuwa juu. Subiri aje Companero. Kwi kwi kwi.
 
Juli:

Yeah wakati wa Mpemba effect ilikuwa juu. Subiri aje Companero. Kwi kwi kwi.

Kibaya Companero hana mwingine zaidi ya Mpemba wakati mimi ninayo mizungu ya kumwaga. Ukimbana sana anaanza kukutajia akina Ibn Battuta na Tippu Tip
 
Kibaya Companero hana mwingine zaidi ya Mpemba wakati mimi ninayo mizungu ya kumwaga. Ukimbana sana anaanza kukutajia akina Ibn Battuta na Tippu Tip

Inabidi wafuate mfumo wa viwanja. Ukimaliza college unaanza na entry level, hivyo kazini wanakupa mafunzo muhimu ya practical. Baada ya miaka miwili unakwenda kwenye mid-level na baadaye senior position.

Bongo naona wanataka kutoa injinia aliyekoma pale anapomaliza shule. Hivyo College of Engineering inataka msaada wa kuwa na viwanda.
 
Jamani mimi naona aibu na hiki chuo chetu. Nimejaribu kuwaccess baadhi ya potential professors wa engineering hapa chuoni kwetu ambao wanaaccess na foundation mbali mbali kama National Science Foundation Research na Rockefeller Foundation na kuwaeleza matatizo yetu lakini hii website ya COET na UDSM haifunguki kabisa. Wameshindwa kuona kitu jamani mbona website za Mzumbe, Makerere na Nairobi zinafunguka vizuri tu. Halafu sijui hata kama kwenye website zao wanaonesha research ambazo wanafanya. Tunakazania chuo chetu sijui kina rank kubwa Afrika wakati vitu vidogo vinatushinda.

I am done.

Mwenye hasira na mafisadi wa elimu!
 
Inabidi wafuate mfumo wa viwanja. Ukimaliza college unaanza na entry level, hivyo kazini wanakupa mafunzo muhimu ya practical. Baada ya miaka miwili unakwenda kwenye mid-level na baadaye senior position.

Bongo naona wanataka kutoa injinia aliyekoma pale anapomaliza shule. Hivyo College of Engineering inataka msaada wa kuwa na viwanda.

Tatizo nafikiri UDSM wanawakaba sana wanafunzi wao ,hawawapi fursa ya kuperuzi mengineyo. Nafikir yanayofundishwa darasani kwa asilimia 95 hayatumiki makazini sasa ukimbana sana mwanafunzi asiperuzi mengineyo lazima ataenda kazini ni mtupu.
 
Hivi huyu Prof. Katima si ndiye mkuu wa bodi ya EWURA , ambapo juzi tuu hii bodi ilitumia zaidi ya milioni mia mbili kumi na tano kwa ajili ya vikao. Today is urging alumni et al to donate their money to CoET ....Mmmh Wajinga ndio waliwao.

Even though FOE is my alma mater , I am not going to contribute even a single penny, of my hard earned money, to the aforementioned fund. The reason is simply I don't trust these people. Prof Katima and his colleague are the reason CoET is doomed . They have been in Chuo for decades now, and sadly they don't have anything new to bring to the table.
 
Haitaishia hapo nyambala, tutatafuta means nyingine mfano...pale esce(facult inayoinvovle comp eng, telecom na electrical) wachina walidhamini matengenezo pia kule kijitonyama pale chuo cha ttcl wachina wamedhamini ujenzi wa lab kali kinoma...very classic.

so mungu atawainua wengine tu usiogope mzee!

Mkuu ZionTZ,

Just to keep the records right, hiyo lab imejengwa na South Korea.Pia hiyo ECSE(siyo esce) ni idara SIYO faculty......worse haina internet connection...too sad(Jamani changieni tafadhali)...Hii ni idara inayofundisha,kutafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu katika Uhandisi umeme na mawasiliano!Just imagine...

Jamani eeeh,tujadili ni vema kabisa.Ni vema zaidi na zaidi tukichangia 'fweza'.Hali hapo CoET si nzuri kuna baadhi ya ofisi za lecturers zinavuja...
 
Vyuo vyote Duniani huwa wanaomba fedha kwa ajili ya kuendesha mzee wangu sasa sijaona ajabu hapa kwa ajili ya kukinga bakuli na kuomba fedha
 
This is a good test for Tanzanians. Ukitaka kujua ubabaishaji wa wabongo waombe fedha kwa kitu productive kama elimu. Utasikia takataka zote ambazo hukutarajia. Hii ni aibu.

Michango mingi sana ya kuponda hapa inatolewa na watu ambao ukweli kwenye vikao vya kuchangia arusi wanamwaga malaki kila mwezi bila hata kujiuliza uhalali wa bajeti zake. Utaratibu huu wa kuchangia elimu upo duniani kote ndo maana vyuo vingine vinajiendeleza vizuri.

Sasa kwa wabongo kuwaambia wachangie elimu ni matusi na wataanza ku call for accountability ambazo hawazionyeshi mahali popote.

Kuchangia public cause kunaonesha level yako ya civilization ilipofikia. Hao wajerumani na wascandinavia wanaotuchangia kila siku hawaulizani maswali ninayo yaona humu.

Wazo la kuchangia chuo si jipya na vyuo vingine pote duniani wanafanya hivyo. Ningeshauri wakuu wa CoET waandae public sensitization event na washirikishe makampuni makubwa sana yanayonufaika na products zao. Makampuni hasa ya simu, Viwanda vya Cement, Bia, Migodi, Makampuni ya Ujenzi, N.K. Wanaweza wakakusanya mabilioni yanayotosha hata kujenga chuo kingine cha uhandisi nina uhakika huo.

FoE na sasa CoET ndo imekuwa ikichukua cream ya vichwa vya Tanzania kwa miaka mingi (point tatu za form six nyingi zinaishia hapa) na kusema ukweli waliotoka hapo ndo engine inayoendesha uchumi wa Tanzania (pamoja na kuwa wengi vile vile wamekimbilia nje) kwani they are spining billions kwa Makampuni ya simu kama Vodacom, Zain, Tigo, TTCL, Zantel, n.k; they are also spining billions kwa viwanda vya vinywaji kama TBL, Coca Cola, Pepsi, Serengeti n.k. They are spining billions kwa makampuni ya ujenzi, Migodi ya dhahabu, n.k.

Kusema kweli kinachohitajika ni kujua hilo na kuandaa public event itakayokuwa well publicized. Haya makampuni yatashindana kutoa hela. Tayari yana-contribute billions katika maeneo mengine mengi. Kwenye hili hawatasita.

A billion dollar question would be; baada ya hayo mabilion kuchangwa nini kitatokea?? Tukiwa na concrete plans ikaonekana tunahitaji funds za kufanya a, b, c, d, e, etc money is there. Lots of money. I challenge professa Katima to do this.

The problem to him will be on how to manage the money!
 
Tatizo ni kuwa tunadhani Chuo Kikuu ni glorified shule ya msingi! Tunasahau kuwa Chuo Kikuu ni kitovu cha utafiti na si mahali pa kufundishia peke yake. Badala ya kugeuza Chuo Kikuu kuwa mahali pa kutengenezea ujuzi (knowledge) sisi tumakimbilia kuwekeza kwenye department store uchwra na ukumbi wa harusi!

Mimi hata namna yalivyokuja maombi yenyewe yananitia wasi wasi. Bila kueleza nini hasa kinachokusudiwa kufanywa wanakimbilia kupanga viwango vya michango! Kwani tuko kwenye kikao cha harusi?

Amandla........
 
Back
Top Bottom