udsm na ucheleweshaji wa vyeti

udsm na ucheleweshaji wa vyeti

thehunk

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
529
Reaction score
227
wana jamii wa jf heshima kwenu kwa ujumla....nasikitishwa sana na hiki chuo kikongwe hapa nchini kutumia utaratibu mbovu wa utoaji vyeti kwani vyeti vinachelewa sana takribani zaidi ya mwaka ndio unakuja pata cheti chako tena ukienda pale 'examination unit' wanajibu kwa kebehi kabisa kuwa huo ndo utaratibu uliopo tangu chuo kinaanza kwa hiyo ni jambo la kawaida wakati walitakiwa kuonesha uchungu na kuguswa juu ya hili kwani kuna watu wanavihitaji hivyo vyeti zaidi ya wao wanavyo fikiria
 
Mkuu umenikumbusha mbali sana, yani pamoja na kuchelewesha vyeti lakini wahusika wake ambao ni examination unit pamoja na finance wanasumbua sana.

Kuhusu utaratibu wa kuchelewesha vyeti nadhani utawala uupitie upya ili vyeti viwe vinatolewa mapema zaidi.

Kwa wale wahudumu wanaohusika na hizo ofisi nawaomba wajirekebishe kwani wanawatesa Watanzania wenzao kwa kuwapa majibu ya kebehi, huu si uungwana.
 
Eeh Mungu nisaidie,hii safari yangu ni ndefu sana...

Yaani cheti nakisotea kwa jasho langu,alafu nikikihitaji,naambulia fedheha....
 
Nakwambia we acha tu, kuna mwaka flani nilimsindikiza rafiki yangu kwenda kuchukua cheti chake. Bwana wee! Tulifanya mizunguko siku nzima bila mafanikio hadi siku ya pili ndipo tukafanikiwa tena kwa mbinde sana.

Kwa kifupi examination unit walituelekeza twende finance. Kufika kule muhasibu akatuambia twende baadaye kwa kua alikua anapata kifungua kinywa.

Baadaye tulirudi kwake tena ila akatwambia twende tena kesho yake maana kwa muda ule alidai alikuwa anajisikia vibaya kiafya.

Tulienda tena siku iliyofuata lakini tulizungushwa sana hadi kukata tamaa ila tulifanikiwa baadaye mida ya saa kumi.

Kwa ujumla kuna mizunguko na nyodo sana ktk ofisi za chuo. Cha kushangaza rafiki yangu alisema huo ulikua mwaka wa pili toka ahitim elimu yake pale chuoni ila alisema kua utaratibu wa kupata cheti kwa udsm ni mwaka mmoja toka kuhitim.

Mabadiliko yanahitajika.
 
sio siri mabadiliko yanahitajika mi nilienda na kuwauliza kuwa huu ucheleweshaji si unatokea kila mwaka na usumbufu si mnaupata nyinyi watu wa examination unit sasa kwanini msiongee na uongozi wa juu huu utaratibu ukabadilika alicho nijibu kuwa eti kuna 'suggestions box' hapo nje kama vipi niandike nitumbukize hivi kweli huyu mtu yuko serious kweli? mwengine akaniambia kama vipi pia niandike barua ya malalamiko nitumie kwenye huo uongozi wa juu ninaosema ni kitu cha kustaajabisha sana
 
Mara nyingi imejengeka kwa Watanzania walio wengi kua mtu akiwa ofisini ni bora kuliko watu anaowahudumia huku ikisahaulika kabisa kua mishahara yote ya serikali inatokana na kodi za wananchi. Bila kodi hakuna ofisi ya serikali itatoa huduma kama wengi wasivyofikiria.

Kuna umuhimu watu wakatambua kua huduma kwa wateja ni kitu cha muhimu sana uwapo mahali pa kazi, iwe mtaani kwenye biashara zako ama ofisini kwenye taasisi za umma ama za binafsi.
 
Back
Top Bottom