msovero
JF-Expert Member
- Jun 30, 2019
- 863
- 1,534
Wavuti inayofanya tafiti na kutoa orodha ya vyuo vinavyoongoza kwa ubora duniani 'webometrics' imekitaja chuo kikuu cha dar es salaam 'udsm' kuwa ndio chuo pekee kutokea Tanzania kuwepo kwenye orodha ya vyuo vikuu 50 vinavyoongoza kwa ubora barani Afrika.
Kwa mujibu wa rank za vyuo vikuu iliyotolewa na wavuti ya webometrics mwezi july mwaka huu 2021, udsm kimeshika nafasi ya 42 kwa ubora barani Afrika, nafasi ya 1911 kwa ubora duniani na nafasi ya kwanza kwa ubora kati ya vyuo vikuu 51 nchini Tanzania.
Viwango vya ubora vya sasa vilivyotolewa na webometrics vinaonyesha kuwa chuo kikuu cha Dar es Salaam 'udsm' kimepata maendeleo makubwa ukilinganisha na viwango vilivyotolewa mwezi january mwaka huu ambapo kilitajwa kushika nafasi ya 1971 ulimwenguni.
Aidha, webometrics imeendelea kukitaja 'udsm' kushikilia na kudumisha msimamo wake wa kuwa chuo kikuu cha kwanza kwa ubora nchini Tanzania.
Utafiti huu unapatikana katika wavuti ya webometrics kupitia kiunganishi hapa chini:
www.webometrics.info

Africa | Ranking Web of Universities: Webometrics ranks 30000 institutions
www.webometrics.info