Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 60
Kama kuna migomo mingi iliyokwisha fanikiwa ni vema wakarudia kwenye makablasha ya migomo hiyo ili kuweza kupata mbinu zilizo tumia. Kwani hadi sasa JF imeshindwa kutoa njia ya kuweza kufanikisha mgomo wao.
Wanamlimani kwa kauli yako ya pale juu wamekuwa wakishinda migomo mingi, na huu sio wa kwanza, hivyo kuna idadi kubwa kabisa ya waliopitia mlimani ambao wapo mitaani na bado kuna skandari nyingi tu...!
Mkuu Ben,
Hakuna ugomvi wowote kati yangu na mama. Mama ni mmoja wa memba wanaoheshimika sana hapa forum. Imekuwa tu yeye yuko upande wa kina Mkandala kwenye hii case na mimi niko upande wa wanafunzi.
Nakubaliana na wewe, dada! Tatizo ni kwamba UDSM kwa miaka mingi imekuwa politicized na itaendelea kuwa hivyo kutokana na kuwa:
1. Wanafunzi na vijana wasomi kwa kawaida hupenda sana masuala ya siasa na wanajaribu ku-apply wanayoyafunza darasani including democracy
2. CCMi litambua mapema kuwa chanzo cha dissent duniani ni kwa vijana hususan wanavyuo, kwa hiyo imekuwa ikifanya jitihada makusudi kuhakikisha kuwa wanaingilia uongozi wa wanafunzi. Ndiyo maana kila baada ya miaka kadhaa wanafunzi hutimuliwa (hata akina Sitta walitimuliwa!)
Lakini hii ya leo kuleta FFU naona ni TOO MUCH! Hao wanafunzi walikuwa wanatishia vipi amani? Labda tuendelee kupata habari.
Nimepigiwa simu sasa hivi na mwanafunzi wa mwaka wa pili wa IT,
hakuna kozi hiyo pale mlimani,navyojua kuna Bsc. in Computer science pekee,hauna haja ya kutupa namba.siye wenyewe tutajua.
Invisible fuatilia suala hili kwa ukaribu,
Nina uchungu sana, mjukuu wangu yupo mwaka wa tatu, mitihani kanambia wataanza wiki mbili zijazo, kisha akifukuzwa inakuwaje? Nihangaike tena?
Mjukuu wangu huyu nimehangaika naye tangu vidudu, nimemsomesha, kesho kutwa naiona digrii hile, halafu alete ujinga?
Kuna rafiki yake Aggy kanipigia simu sasa hivi anasema huko polisi wanarusha mabomu na kuwa watu wameumia. Na huyu aggy hajui alipo. Hapa nilipo tumbo linawaka moto. Aggy mjukuu wangu hana simu.
Kuna mtu kanitumia email akini-update na hali ilivyo chuo; inaonekana hali sio shwari. Ni kama vita. I am surprised and shocked maana sijasikia cha kutisha walichofanya hawa wanafunzi hadi waletewe polisi wenye masilaha yote haya. It looks lile the leadership failure in our country is right across the board! Herebelow I share with you some few phrases from the email I received.
Hakuna malumbano mama, unaweza kuhoji chochote unachopenda na ukapata majibu kama kawa ya JF. Ukipata majibu yako basi usiyachukulie kama malumbano. Okay?
Ni makosa makubwa sana kwa uongozi wa chuo kikuu kuingilia uhuru wa wanafunzi wasomi wa kujichagulia viongozi wao. Kikwete sijui anafanya nini badala ya kunyakua simu na kumpigia Mkandala na kumuonya kuwa asimuaibishe.
Siko upande wa Mukandala tafadhali usitoe maneno from u ukayafanya yangu mdomoni mwangu. Nimepita mlimani, I have the feeling and I put myself on the students shoes now. Mimi sina chama jamani. Ninachoweka hapa hakifungamani na mambo ya CHADEMA,CCM, CUF, DP wala UDP.
However, sijasema wanafunzi wamekosea au utawala uko right, what I wanted to see are the explanations from Ant Ufisadi au wanafunzi kueleza kwa uwazi nini walitaka.
Nimepigiwa simu sasa hivi na mwanafunzi wa mwaka wa pili wa IT, wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwamba, baada ya wanafunzi wa UDSM kuamua kuandamana kupinga kwa wenzao 15 kusimamishwa shule na kukamatwa ili kupelekwa mahakamani, mchana wa leo, hali ya amani hapo chuoni iligeuka baada ya askari polisi kutumwa kwenda kuwakamata wanafunzi wote ambao walionekana wakiandamana. Aidha, polisi waliendesha zoezi hilo kwa kuwakamata hata wale wanafunzi ambao hawakuwa wakiandamana, ili mradi walikuwa katika sehemu mbali mbali za wazi (hadharani), wakijikuta wakipigwa bakora na kuswekwa kwenye TZR za polisi!
Habari zaidi zitapatikana kwenye vyombo rasmi vya habari. Ila, habari hizi ni za kweli. Yeyote mwenye kutaka ufafanuzi zaidi apige simu namba +255-786-019019
Kaka Ndege na wewe kwa leo umetokosa. Nina kijitabu hapa alikiletaga mjukuu wangu hata kozi hiyo inayoitaja wewe pia haipo. Kozi za kompyuta ni:-Gembe acha chuki zako binafsi, kuna kozi inaitwa Computer Engineering and Information Technology (CIT) au hauna info nini kaka?
Binafsi pamoja na kwamba napinga sana sababu za hawa vijana kuandamana, naunga mkono haki yao ya kuandamana na zaidi ya yote ninalaani sana na kwa nguvu zangu zote matumizi ya nguzvu yanayotumiwa na polisi. Kwa sababu ni vitisho vya namna hii vimetufanya sisi tuwe taifa la waoga, wanafiki na watu wa kujipendekeza. Nitaunga mkono vitendo vyovyote vya kutuondelea woga na unafiki watanzania.
NDUGU YANGU UNA GUBU!! KWELI KWELI! SASA HUKIMALIZA HIYO KOZI YA COMPUTER SCIENCE UTAKUWA NANI?
AU HAUJUI? KITU KAMA UKIJUI BORA UNYAMANZE MIMI NIPO HAPOHAPO NI IT MTARAJIWA NA PIA NSHAKUWA IT, NIPO FIVE NA WAKATI FFU WANALETA WANAKUJA NILIKUWA NAPATA SAMAKI NA WALI CAFETERIA 1 WALIPO ZIDI KUSOGEA NILIKIMBILIA MAENEO YA HALL 1 ,
WAKATUKIMBIZA IKABIDI NIINGIE KWA AKINADADA PALE HALL1 WAKANIFUNGULIA NIKAPOA NOA KUWASIKILIZIA ,NDIO WAKAANZA KUPIGA MABOMU YAO TUKAWA NA MAJI TUKANAWA MACHO YAKAWA HAYAWASHI ILA SHIDA IKAWA KWENYE PUMZI TU HEWA ILIKUWA NZITO TU!,
MPAKA WALIPO MALIZA KUPIGA HAYO MABOMU YAO NDIO NIMETOKA HAPA,
WAKATI NAKUJA COET NA BASS ZA MABIBO HOSTEL ZIKAWA ZINAINGIA KUWACHUKUWA WANAFUNZI.
PIA NIKAONA DADA MMOJA KABEBWA KUTOKANA MSHITUKO PRESHA IKAPANDA HUYO DADA INAONEKA NI MPISHI WA CAFTERIA 1.
NIPO COET NIMECONNECT WIRELESS NAENDELEA NA MAMBO YANGU.
HAUNA POINT.
SIKUNYINGINE USIBISHIE WATU HOVYO.
MWANAHAKI ASANTE KWAKUTOA INFORMATION.
Muwasaidie vijana, vinginevyo mnakipeleka wapi chuo?? siasa za wanafunzi waachieni wenyewe
Nasikitika sana ninapoona wachangiaji ninaowaamini kama Mama anaposema tuwaache kwa kuwa walienda kupokea t-shirt na kofia kwa Mafisadi. Hivi kama mzazi unawatoto 4 na 1 ni mlevi hivi ni sahihi kwa wale wengine wakija kuomba fedha za karo uwatimue eti wataenda kulewa?
Kwa hali ilivyo sasa hivi pale Mlimani kama wanafunzi watarespond kwa FFU tunaweza kutengeneza tukio kama la Jan 27 pale Zanzibar
Lakini si Kikwete alimpa kazi rafiki yake Mukandala baada ya yeye kumfanyia kazi nzuri na REDET? Tatizo ni kwamba Kikwete kote kaweka washikaji, na anawaamini, hasa wasomi kama mkandala hawezi kum-oppose! Hapo tusitegemee kitu.
Hata mimi nimewasikitika sana wanafunzi kuwa treated kama wahalifu!
Hilo la uongozi wa chuo nalielewa, au kwa vile ni Mtatiro yumo basi nisihoji chochote. Sitaki malumbano period!
Bandugu,
The situation is terrible at UDSM. Yataka ujionee na si kuadisiwa. Kama una gari kwa usalama usiende nalo kupita utawala.
Jamani, masikitiko yangu ni juu ya uwezo wa wasomi wetu watarajiwa. Fikra za watawala wetu juu ya mfumo wa elimu ni kuufanya uzalishe wataalamu wenye fikra mgando. Lakini kwa ulafi uliwafanya pofu wanashindwa kuona ndani ya zao la mfumo huo mbovu wanazalisha pia wapiganaji huku uchumi uzakomaza jeshi la wamachinga. Haya majeshi mawili yanazidi kukomaa na ipo siku yatakuwa "MUNGIKI"
Ushauri wa bure kwa Mkandala-VC: Naomba uweke rasmi MGOMO kama Course mojawapo itolewayo UDSM na wanafunzi wapewe course work marks. Hii itakuwa vema maana naona migomo inachukua sehemu kubwa ya masomo UDSM na kinachopiganiwa ni cha haki kuliko nadharia zisizo na tija zilizojaa ndani ya "MADESA"
Mh. Invisible naomba kutoa hoja.
Kaka Ndege na wewe kwa leo umetokosa. Nina kijitabu hapa alikiletaga mjukuu wangu hata kozi hiyo inayoitaja wewe pia haipo. Kozi za kompyuta ni:-
B.Sc/ M. Sc ( Electronics and Information Technology)
B.Sc./M. Sc (Computer Scinece)
PGD (ICT Policy and Regulations)
Master of ICT Policy and Regulations
Kuna Department ya Computer and Systems Engineering.