Kama hiki ndicho uongozi wa shule unabet on basi nchi imekwisha hiyo. Yaani wanaombea hali iwe ngumu kiasi hiki ili wanafunzi washindwe kudai haki yao?
Ni taifa gani hili wanajenga?
Pamoja na maneno yako kuwa mgomo hauna wafuasi, je kuna sababu ya kupiga wanafunzi kwa mabomu ambao hawagomi?
Hawakuwa na sababu ya kupiga mabomu, hilo lilikuwa na katika kujihami baada ya kusikia vijana kutoka engineering wameamua kuuvalia njuga mgomo. Frankly speaking engineering ni kiboko na chuo kinafahamu fika vijana wa huko (zamani iliitwa FOE).
Hii nchi iko kiubabe ubabe sio leo tuu kama sio kimtandao mtandao. Haki wanayo ya kumchagua kiongozi wao lakini nadhani walikosea kuanza, so wanatakiwa kujipanga upya. Kwa sasa nadiriki kusema wana sababu lakini ni nyepesi ya kuanzisha mgomo, kama wana sababu nzito wailete.