Jamani mimi nadhani hawa wanafunzi sasa wawe serious. Jamani we are dealing with the CREAM OF THE NATUIONS (WHATEVER THAT MEANS!) Ni watanzania wangapi ambao wamefika CHUO KUKUU CHA MLIMANI? jibu ni % ndogo sana. Sasa basi kama wasomi kama hao mpaka leo hawawezi kukaa chini na kujenga hoja, nina walakini na strategy zao. Mkulima atafanya nini?
Kifupi hapa tusiisingizie CCM, otherwise tunaendekeza uzembe wa kufikiri. Ni kweli CCM wanatumia mbinu chafu kufanikisha malengo yao, lakini je, hao wasomi wetu hilo hawalijui? kwa nini na wao wasikae chini wakaja na strategies mbadala? Jamani JF tunawatetea wakulima na wafanyakazi ambao majority ni no-class, la saba na form four, ambao kila siku CCM inawadhulumu haki zao kwa kutumia uelewa wao mdogo. Na wasomi wa Chuo Kikuu kweli? Hao wasomi ni tabaka ambalo taifa linawategemea liwasaidie na strategy za kupambana na mbinu chafu za CCM! hawawezi kukaa na kuanza kulia lia kama watoto wadogo eti Makamba na CCM wanawafanyia mbaya..thats known kwamba CCM ni mafias! Kama wasomi inabidi wakae waje na hoja, wamobilize wenzao kutafuta suluhu! Msomi inabidi awe mtu wa mwisho kutafuta shortcut ya jamabo lolote!
Yes...Kudai haki si lelemama, lakini inavyokuja kwa watu kama mlimani..walimu ni wasomi na wanafunzi ni wasomi ni kushindanisha hoja! Sasa kama wanafunzi walio makini mnashindwa kupambana na akina Makamba FORM FOUR kwa HOJA mtapambana na Makamba mkishaingia street? acheni utani bana. Kwa hili, mnahitaji kuprove kwamba mko academically relevant!
Harafu lazima muwe mnasimamia maslahi ya wananchi. Ni aibu kuona Chuo kama mlimani hakuna efforts zozote zinazofanywa na maintellectuals katika kutafuta muarobaini wa matatizo yetu! Zaidi ya kuvaa kofia na kuisifia CCM Diamond Jubilee! Mnaudhi sana kwa sababu mnakuwa wabinafsi kwa mambo yenu tuu....
Elimu ya Chuo Kikuu lazima iwabadilishe kimawazo na kifikra. Sio kukimbilia kugoma, thats should be the last resort. Na mind you mnadeal na watu rational walioenda shule. Naelewa fika mlimani bila mgomo haki inakuwa shida, lakini you should use all available means kuchallenge maamuzi ya watawala...kuna wanasheria hapo, maengineer, wahandisi etcs....please do us a fovour! Tunawategemea nyinyi..