Ndugu zangu wana JF ni dhahiri tuka conclude kuwa hakuna anayeweza kuiweka kinagaubaga hapa issue ya UDSM, vijana wetu wameshindwa kujieleza, lakini kama ilivyoelezwa awali, wengi wetu tumepitia mlimani, tunaielewa situation, na kwa kwa kutumia uzoefu huo tunaweza kutoa mpendekezo ya suluhu mlimani. Nilikuwa mlimani miaka ya 2000 mwanzoni, enzi za akina Mkili, Zitto, Msando, Rugemalira, Ndaskoi etc.
Kwa ufupi hali ya demokrasia nchini mwetu inashabihiana kwa karibu na ile ya pale mlimani, kuna vitisho,ukandamizaji,rushwa,kubambikizana kesi na kila aina ya ufisadi baina ya wanafunzi wenyewe, ndani ya DARUSO na uongozi wa chuo. Wanafunzi wengi ambao ni potential kuwa viongozi na wenye ushawishi wanatafutwa au wanatafuta support ya makundi fulani ya nje yanayopambana na system nyingine ya utawala wa chuo ambayo imewekwa na system yenye wafuasi ndani ya jamii ya wanafunzi. Wakufunzi wao nao wamekuwa hodari wa kuzungumza kwenye forums za nje ya chuo ingawa wao wenyewe wako kwenye spoiled system ambayo wanaogopa kuisemea. Tutegemee nini sasa? Product ya hawa wakufunzi ndo sisi watanzania waoga na wajinga wa kujieleza. Ni kweli pia kuwa mtazamo kifikra miongoni mwa wanaharakati hawa wanafunzi umetofautiana na wakati mwingine kunakuwa na hoja zisizo na msingi zaidi kuliko zile za msingi, lakini all in all lazima tukubali kuwa kuna tatizo UDSM. Kwa hiyo ni mgogoro unaotakiwa kutazamwa kwa upana. Katika mazingira haya kuna walio neutral, wanaoona hakuna tatizo lakini kuna wanoona kuna tatizo.
Nimewasiliana na baadhi ya vijana waliopo pale, ni kweli vijana wameamua kugoma ili wenzao takriani 25 waliosimamishwa masomo warudi. Kisheria mgomo huo ni batili maana viongozi wa DARUSO hawajaridhia. Kiini cha mgogoro wote huu ni Uchaguzi. Utata wa suala hili la uchaguzi wa rais ulioleta utata. Kumekuwa na matatizo ktk chaguzi nyingi za UD na wakati mwingine kumekuwa kuna attempt za kupindua serikali. imekuwa ikitokana na kupandikizwa kwa viongozi na utawala wa chuo, wengi waliowahi kuwa marais kwa kupandikizwa tumewaona wakipewa zawadi ya ajira na chuo, wapo akina Kusaja, Rugemalira alipewa zawadi ya scholarship, Kayombo alipewa zawadi ya ajira etc. Tuwaponde wanafunzi kwa kutokuwa na hoja lakini kuna tatizo mlimani linalohitaji attention yetu.